08 August 2022
Mbeya, Tanzania
More info :
08 August 2022
Rais, Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji Mbalizi mkoani Mbeya.
Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kuwa, “Wizara ya Kilimo inatakiwa kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika kuwasajili wakulima ambao watapatiwa ruzuku, na kuwataka wahusika kuhakikisha wanajisajili kwani baadaye vitatolewa vitambulisho vitakavyowasaidia kupata huduma.”
Akizungumzia miradi ya Kilimo, Rais Samia Hassan ameungana na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kusema miradi mingi ya kilimo inatakiwa iwanufaishe wakulima katika maeneo husika, na kuwataka maafisa ugani kuwa makini na matumizi ya rasilimali na vitendea kazi vya Serikali walivyopatiwa ili kuwahudumia wakulima.
Wakulima waaswa kuzingatia kilimo chenye tija
5 hours ago
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewataka Wakulima nchini kuendelea kufuata maelekezo ya wataalamu wa Kilimo, ili kuweza kupata mazao yenye tija wakati wa mafuno ambayo yatawanufaisha kiuchumi na kuliingizia Taifa kipato.
Bashe ameyasema hayo hii leo Agosti 8, 2022 katika kilele cha cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane), ambayo yanafanyika katika uwanja wa John Mwakangale Mkoani Mbeya na kusema ulimaji wa mazao bila kuzingatia maelekezo ya wataalamu ni kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Amesema, sambamba na hatua hiyo pia wakulima wanatakiwa kuwa makini na ununuaji wa mbolea zilizothibitishwa na kuanishwa na Serikali, ili kuweza kurutubisha ardhi na hivyo kujiwekea uhakika wa mavuno ya kutosha kwa chakula na biashara.
“Ni lazima kuzingatia maeloekezo ya wataalamu wa Kilimo, hii itasaidia kupata mavuno yenye tija, lakini pia tuzingatie ulimaji wa mbolea ambao utasaidia kutupatia wakulima mazao ya chakula na biashara na tuzingatie viuatilifu vilivyoainishwa na Serikali,” amesema Bashe.
Amesema, msimamo uliopo ni kubadili mifumo ya ununuzi pembejeo za kilimo za ruzuku baada ya Serikali kuja na mpango wa ujenzi wa viwanda vya mbolea nchini na kusema ni vyema kuweka umoja baina ya wakulima kwa kubadilishana taariza zinazolenga kuwasaidia kufikia malengo