Rais Samia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la wafugaji litakalofanyika mkoani Simiyu

Rais Samia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la wafugaji litakalofanyika mkoani Simiyu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la wafugaji nchini litakalofanyika kitaifa mkoani Simiyu mwezi ujao.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Mrida Mshota, alisema kongamano hilo, litafanyika kuanzia Mei 15 hadi 18, mwaka huu katika Wilaya ya Bariadi mkoani humo.

Mshota, alisema, kongamano hilo litakutanisha zaidi ya wafugaji 200,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Alisema itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kukutana na wafugaji na kusikiliza changamoto zinazowakabili na kujadili namna ya kuboresha sekta ya mifugo nchini na uchumi wao.

“Hii itakuwa ni fursa kwa wafugaji kuwasilisha matatizo yanayowakabili, mafanikio waliyoyapata na kumpongeza Rais Samia kwa mambo mazuri aliyowafanyia,” alisema Mshota.

Aliisifu serikali kwa kuwekeza katika sekta ya mifugo nchini na kuvuka lengo kwa kujenga majosho 754 kutoka 105, kununua lita 52,000 za dawa ya mifugo na chanjo ya mifugo kwa Shilingi bilioni 28.1.

samia ufugaji.png

Alisema hatua hiyo ya serikali, inalenga kukuza mnyororo wa thamani katika mazao ya mifugo.

Alisema kuanzia sasa mifugo ya Tanzania itakuwa na hati safi za viwanda vya kimataifa, kufungua masoko kimataifa ya bidhaa ya nyama, kukuza biashara na kuwa chanzo kikubwa cha ajira nchini.

"Kongamano hili litahamasisha ufugaji wa kisasa na endelevu, kupitia elimu na matumizi ya tekinolojia za kisasa, mbinu bora za ufugaji zinazozingatia tija, ubora wa mazao ya mifugo na uhifadhi wa mazingira kama sehemu ya mpango wa kitaifa wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi," alisema.

Source: Nipashe
 
baada ya hapo anawafukuza Ngorongoro. Wajinga ndio waliwao
 
Back
Top Bottom