Mjanja M1
JF-Expert Member
- Oct 7, 2018
- 4,058
- 14,382
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho, Ijumaa Aprili 12.2024 anatarajia kuwaongoza Watanzania katika kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine
Akizungumza na wanahabari leo, Alhamisi Aprili 11.2024 Monduli juu, Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda amewaomba wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika maadhimisho hayo
Akimzungumzia Hayati Sokoine, Makonda amemtaja kama mtu aliyekuwa muadilifu na mchapakazi huku akitoa wito kwa Watanzania kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwaenzi viongozi waadilifu na wachapakazi wa sasa wenye sifa na uchapakazi wa kufanana na Hayati Sokoine
Makonda amemtaja Hayati Sokoine kama mtumishi mahiri na mwenye ujasiri wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya Watanzania bila kuogopa na kuhofia vikwazo mbalimbali
Mkuu wa mkoa huyo ametembelea makazi ya Hayati Sokoine eneo la Enguiki Monduli, kukagua maandalizi ya shughuli ya kesho ya kumbukizi ya miaka 40 tangu kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Hayati Moringe alikuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980, tena tangu tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake, alipofariki kufuatia ajali ya gari
Uongozi wake unatajwa kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.