Rais Samia kuweka jiwe la msingi SGR Tabora–Kigoma, kufungua ujenzi mpya ya usafiri na biashara

Rais Samia kuweka jiwe la msingi SGR Tabora–Kigoma, kufungua ujenzi mpya ya usafiri na biashara

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma Julai 20, 2026, katika hafla ya kitaifa itakayofanyika mkoani Kigoma, hatua inayotajwa kuwa ya kimkakati katika kuimarisha uchumi na usafiri wa ukanda wa Maziwa Makuu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Julai 19, 2026 , Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, amesema mradi huo unatekelezwa kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga mfumo fungamanishi wa usafiri kwa kuunganisha reli, bandari na njia nyingine za usafirishaji ili kuongeza ufanisi wa biashara na uwekezaji.

Prof. Mbarawa amesema reli hiyo yenye urefu wa kilomita 506 na thamani ya takribani dola za Marekani bilioni 2.74 itaunganisha Kigoma na mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam, huku ikiweka msingi wa kuunganisha Tanzania na Burundi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutapunguza muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Kigoma kutoka zaidi ya saa 30 zinazotumika kwa reli ya kawaida hadi takribani saa nane kwa kutumia SGR, jambo litakalorahisisha usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo.

Vilevile Prof. Mbarawa amebainisha kuwa, reli hiyo itaongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwezesha mizigo kufika haraka Kigoma na kusafirishwa kwenda Burundi, DRC na masoko mengine ya Afrika ya Kati kupitia Ushoroba wa Kati.

Aidha, amesema mradi huo utaunganishwa na kipande cha saba kutoka Uvinza hadi Musongati nchini Burundi kinachotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Burundi, hatua itakayopanua mtandao wa reli ya kisasa na kuifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha biashara na usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Soma pia Rais Samia: Tusikubali kutumika na watu wasioitakia mema nchi yetu, tuepeuke kuwa wasaliti na maadui wa nchi yetu

1784464076717.png

1784464114866.png

1784464174144.png

1784464174209.png
 
Hakukuwa na sabab kabisa kiuchumi kujenga SGR kutoka Tabora kwenda Kigoma..route ya kigoma na mpanda reli ya zamani ingeimarishwa kuja tabora kuunganishwa na SGR, ni ujinga kujenga SGR ukitegemea mizigo ya nje..! sabb wanaweza kuamua kubadilisha route kupitisha mizigo yao..na kutoka tabora hadi kigoma hakuna kitu chochote hapo katikati chenye manufaa kiuchumi..

hata abiria, tofauti na route ya tabora-mwanza, ambayo inaunganisha mikoa 5 ..shinyanga, geita, kagera, simiyu na mara na hapo isaka rwanda wangejenga reli hadi keza kufanya njiapanda moja kwenda burundi na nyingine kwenda rwanda..aliyeanza kujenga SGR ndio aliweka hii plan, baada ya yeye kuondoka wakaja WEZI na mipango mipya, wakageuza plan kuweka SGR ifike kigoma.

Kwanini hawakusema na mpanda iwe na route ya SGR sambamba na ya kigoma..? Halafu unaweka jiwe la msingi sasa wakati SGR yenyewe hata manyoni haijafika..lengo ni nini? KUIBA! Hela zikopwe kwa route mpya ya kigoma wababaishe hapo kuweka weka ushahidi halafu pesa yote iwekwe mifukon mwa watu..! Unatarajia angalau SGR ifike singida ndio uanze hiyo ya kigoma..HARAKA HII YA KUZINDUA SGR YA KIGOMA NI YA NINI..?
 
Well done, Dr Samia Suluhu Hassan,

Unafanya kazi nzuri sana ya kutumikia wananchi mama 🔥
 
Back
Top Bottom