Rais Samia kuzindua zoezi la ujazaji maji katika Bwawa la Julius Nyerere, Disemba 22

Rais Samia kuzindua zoezi la ujazaji maji katika Bwawa la Julius Nyerere, Disemba 22

Asingekuwa hiyo uliyemtaja kweli pangekuwa na huo ufungaji wa geti? Dah binadamu ni kweli tulilaaniwa sio bure.
tatizo hamsomi historia hii project ilikuwepo tangu mkoloni ndugu mtz. unataka kuniambia asingekuwa yeye SGR isingekuwepo?
 
tatizo hamsomi historia hii project ilikuwepo tangu mkoloni ndugu mtz. unataka kuniambia asingekuwa yeye SGR isingekuwepo?
Hiyo historia ndio ile iliyotaka makao makuu yawe dodoma ila haikuwahi kutekelezwa mpaka magufuli kaingia au unaongelea historian gani!?
 
tatizo hamsomi historia hii project ilikuwepo tangu mkoloni ndugu mtz. unataka kuniambia asingekuwa yeye SGR isingekuwepo?
Ukirudi kwenye historian ni kweli SGR lilikuwa wazo ni sawa na ndoto, nani kaiweka kuwa kweli? Tuna ndoto nyingi watz za toka Uhuru lakini bado ni ndoto, Kama vile Mimi Kila Mara nina ndoto yangu kuwa kesho nitakuwa milionea Kama manji lakini ni kweli kuwa Mimi ni milionea Kama manji? Ndoto tu mwanangu ikitokea mwanangu mmoja akaitimiza Basi atakuwa ameibeba ndoto ya familia. Unayoongea wewe ni uchoyo wa fadhira unavushwa mto Kisha unamtukana aliyekuvusha eti tu kwa kuwa ulikuwa umenuia kuvuka😆😆😆😆
 
Pongezi kwa Serikali yote, kipekee kwa Dr. Samia Suluhu Hassan, wapo baadhi yetu hawafurahii kuona bidii na jitihada anazo zifanya kwa chuki zao za kichawi lakini tunamuomba Mama asonge mbele kutupambania.
 
Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassan kushuhudia ujazaji maji Bwawa Umeme la Julius Nyerere leo 22 December 2022
D30C0BCB-D30D-4683-A197-00DEC655EB07.jpeg

Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba amewaeleza watanzania kuwa, zoezi la kuanza kujaza maji katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) litaanza tarehe leo tarehe 22 December 2022 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Watanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
3748842D-1643-4EB9-9C5B-0D96878BA226.jpeg

Makamba amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Desemba 18, 2022 mkoani Pwani ambapo alisema kuwa hiyo ni hatua kubwa, muhimu na ya kihistoria katika kutekeleza mradi huo.
6B2B7388-ED57-4C54-8324-E6DBA2433FAD.jpeg

Amesema kuwa, mradi huo kwa umefikia asilimia 78 ya utekelezaji wake tangu kuanza kwake.
A6F23814-C5C1-411C-9BE9-A61734B0778A.jpeg

Alisema kuwa, kutokana na ukubwa wa zoezi hilo na umuhimu wa mradi huo kitaifa, ni ishara kuwa ndoto za Taifa katika kutekeleza mradi huo zinatimia ambapo zoezi hilo litazinduliwa na kushuhudiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
53FC22BF-E11F-430B-902E-ACCE5070DF28.jpeg

“Tunayo faraja kubwa kwamba mjadala ambao umekuwa ukiendelea kuhusu dhamira ya Serikali kukamilisha mradi huo angalau utaondoka sasa baada ya kufikia hatua hii, kwa sababu huu ni ushahidi tosha kwamba Serikali, Rais, Wizara ya Nishati, na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tumefanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi huu kwa nguvu, maarifa na juhudi kwa wakati wote, mahali tulipo fika sasa ni pa kujivunia,” alisema Makamba
F3367CAF-6543-45BE-86F3-0D3DF8C8E9F4.jpeg

Alifafanua kuwa, handaki la kuchepusha maji lina urefu wa mita 700, yaani viwanja saba vya mpira wa miguu na lilijengwa miaka mitatu iliyopita kwa gharama ya shilingi takribani Bilioni 235.
CFEAD608-ECFB-47DA-8E42-77FD379981A3.jpeg

Bwawa hilo pia litakuwa ni kivutio cha watalii kwakuwa liko ndani ya hifadhi na litabadili kabisa taswira ya hifadhi hiyo na thamani ya hifadhi hiyo itaongezeka ndani na nje ya Tanzania.

Tanzania (TANESCO), Maharage Chande aliweka wazi kuwa inakadiriwa kuwa misimu miwili ya kipindi cha mvua, itaweza kujaza maji katika bwawa hilo.
54313AAE-D00D-4561-818B-9EB64FFF5E7F.jpeg

“Tunaanza kujaza maji mwezi huu wa Desemba ambapo kuna mvua za vuli, pia tunategemea mvua za masika mwezi Machi 2023, ambazo zitakuwa mvua za msimu wa kwanza, pia tutapata vuli ndani ya kipindi hicho, kisha tutapata zile za masika katika mwaka 2024 pamoja na vuli ya kipindi hicho, hivyo mvua mbili kubwa za masika zinaweza kujaza bwawa kwa hesabu zilizopo,” Alisisitiza Chande.
E1C73997-C1E4-4F01-85FE-57DE4C369C57.jpeg

Zoezi hilo litahudhuriwa na watu takribani 2000 na litatangazwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari ili watanzania wote waweze kushuhudia maendeleo na hatua iliyofikiwa katika kutekeleza mradi huo.
 
Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassan kushuhudia ujazaji maji Bwawa Umeme la Julius Nyerere leo 22 December 2022
View attachment 2454258
Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba amewaeleza watanzania kuwa, zoezi la kuanza kujaza maji katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) litaanza tarehe leo tarehe 22 December 2022 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Watanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
View attachment 2454263
Makamba amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Desemba 18, 2022 mkoani Pwani ambapo alisema kuwa hiyo ni hatua kubwa, muhimu na ya kihistoria katika kutekeleza mradi huo.
View attachment 2454264
Amesema kuwa, mradi huo kwa umefikia asilimia 78 ya utekelezaji wake tangu kuanza kwake.
View attachment 2454266
Alisema kuwa, kutokana na ukubwa wa zoezi hilo na umuhimu wa mradi huo kitaifa, ni ishara kuwa ndoto za Taifa katika kutekeleza mradi huo zinatimia ambapo zoezi hilo litazinduliwa na kushuhudiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
View attachment 2454267
“Tunayo faraja kubwa kwamba mjadala ambao umekuwa ukiendelea kuhusu dhamira ya Serikali kukamilisha mradi huo angalau utaondoka sasa baada ya kufikia hatua hii, kwa sababu huu ni ushahidi tosha kwamba Serikali, Rais, Wizara ya Nishati, na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tumefanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi huu kwa nguvu, maarifa na juhudi kwa wakati wote, mahali tulipo fika sasa ni pa kujivunia,” alisema Makamba
View attachment 2454268
Alifafanua kuwa, handaki la kuchepusha maji lina urefu wa mita 700, yaani viwanja saba vya mpira wa miguu na lilijengwa miaka mitatu iliyopita kwa gharama ya shilingi takribani Bilioni 235.
View attachment 2454270
Bwawa hilo pia litakuwa ni kivutio cha watalii kwakuwa liko ndani ya hifadhi na litabadili kabisa taswira ya hifadhi hiyo na thamani ya hifadhi hiyo itaongezeka ndani na nje ya Tanzania.

Tanzania (TANESCO), Maharage Chande aliweka wazi kuwa inakadiriwa kuwa misimu miwili ya kipindi cha mvua, itaweza kujaza maji katika bwawa hilo.
View attachment 2454271
“Tunaanza kujaza maji mwezi huu wa Desemba ambapo kuna mvua za vuli, pia tunategemea mvua za masika mwezi Machi 2023, ambazo zitakuwa mvua za msimu wa kwanza, pia tutapata vuli ndani ya kipindi hicho, kisha tutapata zile za masika katika mwaka 2024 pamoja na vuli ya kipindi hicho, hivyo mvua mbili kubwa za masika zinaweza kujaza bwawa kwa hesabu zilizopo,” Alisisitiza Chande.
View attachment 2454272
Zoezi hilo litahudhuriwa na watu takribani 2000 na litatangazwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari ili watanzania wote waweze kushuhudia maendeleo na hatua iliyofikiwa katika kutekeleza mradi huo.
Asante sana
 
Asante sana
6B94FA52-F605-42E6-AEAD-BCC5AB298685.jpeg

Katika hafla hiyo itakayofanyika eneo la mradi na kuhudhuriwa na takribani watu 2,000, Dkt. Samia atabonyeza kitufe ambacho kitafunga handaki la kuchepusha maji, hivyo kuruhusu maji kuanza kuingia kwenye bwawa hilo la ujazo wa lita bilioni 32.

Hatua hiyo ni kubwa katika utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 ambazo zitatosheleza mahitaji ya sasa nchi nzima, na kuwa kichocheo cha kuvutia wawekezaji kutokana na kuwa na umeme wa uhakika.
 
kuna mambo mawili yameshtua hapa!!,
1. Walinzi wa Mhe.Rais wako wapi!!??!! hasa yule anayekuwaga nyuma ya rais wakati wote rais anapokuwa jukwaani!!!.
2. Hili bwawa liko limekamilika kweli?!? au maji yatamwaga tena ili kulikamisha!???!. Kingo zake hazijasilibwa kwa cement/saruji kama ndio ufundi wao umeishia hapo si itachukua miaka michache sana tope na mchanga kujaa bwawani?!!?. NISAIDIENI BANDUGU
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza, Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Maharage Chande kuhusiana na Kituo cha kusafirishia umeme (Switchyard) katika Mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere (JNHPP) katika Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022
74E60791-8460-41C6-ACE5-848DA87AD782.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wananchi wa Mikoa ya Pwani na Morogoro kabla ya kuzindua Shughuli ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
33ED3425-E4A3-4112-AFBE-6D07C82C99E8.jpeg

Akizungumza wakati wa zoezi la kujaza maji kwenye bwawa hilo lililofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan leo katika eneo la mradi wilayani Rufiji, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenga amesema ukamilifu wa mradi huo unaenda kichocheo shughuli za uzalishaji mkoani kwake.
63785EE0-5F1E-428C-84AD-66E932447F06.jpeg

WAKUU wa mikoa ya Pwani na Morogoro wamesema wamejipanga kuhakikisha umeme utakaozalishwa kupitia Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), unachochea shughuli za maendeleo na kijamii kwa wananchi wao.

Pia viongozi hao wameahidi kuulinda na kuutunza mradi utakaozalisha megawati 2,115, ambao unagharimu zaidi ya Sh.trilioni 6.5 ili uweze kuwa endelevu.

Kunenga amesema mradi huo utawezesha umeme katika mkoa huo kupatikana kwa asilimia 100 hivyo kuongeza uzalishaji.

“Mheshimiwa Rais sisi Pwani tunashukuru bwawa hili la JNHPP kuwepo hapa Rufiji, tunaamini Watanzania watanufaika ila Pwani itanufaika zaidi, nikiahidi kwa kushirikiana na wenzetu wa Morogoro tutaulinda na kuutunza,”amesema.

Aidha, Kunenga amemuomba Rais kuangalia uwezekano wa kukamilisha ujenzi wa barabara kutoka Mwanarumango hadi kwenye mradi kwa kiwango cha lami, ili kurahisisha kufika eneo husika.

Mkuu huyo wa mkoa amesema barabara kutoka Kisarawe hadi JNHPP ni fupi na rahisi kufikika hivyo anamuomba Rais Samia kutenga bajeti ya ujenzi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa alisema ameomba ujenzi wa bwawa hilo uwe ni neema na kwa wananchi wa mkoa huo kwa kupatiwa huduma za afya, elimu na nyinginezo.

“Sisi tunaomba mradi huu ukianza tupate mgao kupitia CSR ili tuweze kujenga Hospitali ya Rufaa ya kisasa, chuo cha afya na mengine,” amesema.

Mwasa ameungana Kunenga katika kuhakikisha miradi huo inalindwa na kutunzwa.
 
Kweli huyo jamaa alifeli mtihani wa kidato cha sita maana anawapa tuzo watu wasiostahili.

Sasa pale Mwinyi kafanya nini kwenye huo mradi maskini ya Mungu hata kuufahamu hapo alipo haufahamu unahusu nini??
 
Wakati wa Mwendazake mlisema mradi umefika 90%, na mkandarasi mkawa mmemlipa hela yote ya mradi, leo mnasema umefikia 78%.

Tuamini lipi hapo.
Hii niliona yule Kalemani akiongea bungeni 2020 alisema exactly pesa zote zimeshalipwa 100%, hawa watu waongo sana na hata hii ya ujazaji maji naona itakuwa usanii tuu, huu umeme inawezekana kabisa tusiuone for the next 5 years na wanaweza kuja na 50 MW tuu na kiswahili kingi kwa mradi wa trilioni karibu 10
 
Hii ni kwa ajili tu ya kuweka kumbukumbu sawa.

Wakati wa shughuli ya kushusha mageti yanayochepusha maji kwenye mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere ili kuwezesha kujaza bwawa huko Rufiji wiki jana, Mheshimiwa Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan aliweka bayana kuwa bila umahiri na ukakamavu na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ya hayati JPM basi mradi ule usingeanza kutekelezwa awamu tano.
 
Nimeobserve hii tabia kutoka kwake,ndani ya nchi hotuba zake almost zote anamsifia ,lkni akifika kwenye majukwaa ya nje ni kumnanga mtangulizi wake Kila anapopata fursa
 
Timu gaidi wataumia mno na hii video, pamoja na kwamba umeme wanausubiri kwa hamu
 
Hii ni kwa ajili tu ya kuweka kumbukumbu sawa.

Wakati wa shughuli ya kushusha mageti yanayochepusha maji kwenye mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere ili kuwezesha kujaza bwawa huko Rufiji wiki jana, Mheshimiwa Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan aliweka bayana kuwa bila umahiri na ukakamavu na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ya hayati JPM basi mradi ule usingeanza kutekelezwa awamu tano.
Mods imekuwaje tena mme unganisha post yangu na hii; message yangu ni mahsusui tofauti kabisa na general theme. Do the needful
 
Back
Top Bottom