Rais Samia Kuzuru nchini Burundi 16 Julai, 2021

Rais Samia Kuzuru nchini Burundi 16 Julai, 2021

skilled masala

Senior Member
Joined
May 2, 2019
Posts
118
Reaction score
160
Masala Sayi
Chuo Kikuu cha Iringa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwa na ziara ya kikazi nchini Burundi kesho tarehe 16, Julai 2021.

Ziara hiyo imekuja kama mwaliko wa Rais wa Taifa hilo Mh. Evariste Ndayishimiye.Taarifa iliyotolewa na Mkurungezi wa mawasiliano ya Rais ikulu Ndugu, Jaffar Haniu imebainisha kuwa Rais Samia akiwa nchini humo atashiriki shughuli mbali mbali ikiwemo kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Burundi na Tanzania.

"Mh. Rais Samia atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mh. Rais Evariste Ndayishimiye, kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kungumza na vyombo vya Habari, Mh Rais Samia atahudhuria na kuhutubia Jukwaa la wafanyabiashara wa Burundi na Tanzania kwa lengo la kujadili fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na Burundi" ilibainisha taarifa hiyo.

Aidha ziara hiyo itakayodumu kwa siku mbili, itakuwa ziara ya nne kwa Rais Samia kufanya nje ya nchi tangu alipo apishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mama nae mnamsagia kunguni kama Mwendazake hakika nyinyi watu hamjui hata nini mnataka
Kwa hiyo ulipenda tumsifie hata pale anapo vurunda? Hilo ni jambo lisilo wezekana hata kidogo. Bora angewaiga watangulizi wake walioongeza miaka yote kodi kwenye sigara, soda, bia, na baadhi ya bidhaa kutoka nje!

Hii haikuleta athari za moja kwa moja kwa raia wa kawaida kama ilivyo kwa hizo tozo za miamala ya simu na mafuta.
 
Back
Top Bottom