VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Nasema kwakuwa najua na nimekitumikia ninachokisema. Nimekuwa kiongozi kwenye vyombo vya ulinzi; chamani na serikalini. Najua kuwa yapo mambo ya kusemwa hadharani na yale ya kuhifadhiwa na kumalizwa sirini. Yale ya hadharani ni ya kusakia 'support' kwa wananchi. Wananchi wasikie na waamue...kimaoni.
Kauli fulanifulani za Rais zinapaswa kuwekwa wazi ili kuona wananchi wanachukuliaje maagizo au uamuzi wa Rais. Ni jambo jema kujua mambo hayo kwakuwa nchi hii ni yetu na yote yaliyomo ni kwa ajili yetu. Kama ni jambo la kutufurahisha tuambiwe. Kama ni jambo la kutuchukiza na kutufanya tueleze maoni yetu makalimakali mitandaoni tuambie pia.
Tusifichwefichwe. Na kama imeshaamuliwa tufichwe, tusidokezewe kabisa. Tunapodokezewa, tunaongezea ya kwetu ya uongo na ya kweli. Tunajitengenezea habari za heri na za shari. Si jambo jema. Ni juzi tu Rais Samia umetudokeza kuwa kuna watanzania wenzetu wameweka 'cha juu kwelikweli' kwenye ununuzi wa ndege yetu ya mizigo. Hujatutajia ingawa umewataka watupishe.
Ni akina nani hasa? Wapisheje? Sisi wanatuachaje kama watanzania? Ukasema tena kuwa kuna mfanyabiashara mkubwa mmoja amekopa benki zetu tofauti na kutokomea nje ya nchi. Ni nani? Kwanini hayo yametokea huku vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya kazi usiku na mchana? Mafumbo huleta mafundo. Kutufumba ni kututaka tuambiane vile tunavyofikiri. Tuwekwe wazi.
Karibu tena Tanzania Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam