Rais Samia kweli umedhamiria kukusanya Kodi za dhuluma hadi kwenye mbolea?

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Haya yote yanayoendelea nadhani tunayaona na hii itoshe kusema CCM hawana nia tena na kuongoza nchi.

Mmeongeza Kodi sawa, ndio iwe mara mbili? Ongezeko la 100% tena kwa kipindi hiki? HAPANA

Mama hii ni Kodi ya dhulma, haikubaliki. Watanzania wengi wamejiajiri kwenye kilimo lakini napo umeamua kuongeza kodi mara mbili kwenye mbolea.

Kweli tutaisoma namba, sasa hivi kila kitu beini mara mbili ukiuliza unaambiwa kodi mpya. Tutakoma.

Wale wakulima wenzangu kazi tunayo

Nilitegemea mama katika jitihada zako za kukuza uchumi basi ungepunguza haya makodi hasahasa kwenye sekta ya kilimo, Ila imekuwa vice versa

 
Wananchi wa marekani na nchi za ulaya zinawasikia Watanzania kuwa hawataki kulipa kodi eti wanataka wasaidiwe.

Aisee!

Ngoja wanachi wenzetu watusikie! Sijui watatuonaje, kweli tumekomaa au tulidekezwa mpaka ukubwani?
 
WANANCHI WA MAREKANI NA NCHI ZA ULAYA ZINAWASIKIA WATANZANIA kuwa hawataki kulipa KODI ETI WANATAKA WASAIDIWE!!!!
AISEE!
NGOJA WANACHI WENZETU WATUSIKIE! SIJUI WATATUONAJE, KWELI TUMEKOMAA AU TULIDEKEZWA MPAKA UKUBWANI?!
Duh ficha ujinga wako basi atakama ww mambo yapo safi
 
"Mama anaupiga mwingi kweri-kweri" 🤣
 
WANANCHI WA MAREKANI NA NCHI ZA ULAYA ZINAWASIKIA WATANZANIA kuwa hawataki kulipa KODI ETI WANATAKA WASAIDIWE!!!!
AISEE!
NGOJA WANACHI WENZETU WATUSIKIE! SIJUI WATATUONAJE, KWELI TUMEKOMAA AU TULIDEKEZWA MPAKA UKUBWANI?!

unataka usaidiwe kila siku, ebo ! hebu mjitegemee sasa, ndio tabu ya kumnyonyesha mtoto bila kumuachisha mapema sasa ona walivyo lemaa! tulizoea kulishwa kwa kijiko, kweli hatuna aibu hata chembe. tumekua sasa tuache kudeka.
 
Huyu mbunge pichani si wa chama chetu kweli! Kolimba si alisema tumepoteza dira!
 
Kodi sio Jambo baya..ushenzi nauona kwenye ukubwa wa serikali tunautitiri wa viongozi wasio na faida, utitiri wa majimbo yaan pesa inayotumika kuendesha serikali ni kubwa mno tutaendelea vipi jamani kwa Hali hii?
 
Kumbe nianze kuuza mbolea yangu ya mavi ya popo.nipige hela namie[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…