Rais Samia kweli umedhamiria kukusanya Kodi za dhuluma hadi kwenye mbolea?

Rais Samia kweli umedhamiria kukusanya Kodi za dhuluma hadi kwenye mbolea?

Achana na kodi ya miamala ya simu. Kuna kodi ya pembejeo ambayo kelele zake hazijasikika. Serikali imepandisha kodi ya pembejeo za kilimo ili kukomoa wakulima. Mbolea ya kupandia mazao aina ya DAP imeongezeka bei kutoka 52,000= hadi 92,000/= Mbolea za kukuzia Mf.UREA kutoka 48,000/=na sasa ni 80,000/= na CAN kutoka 40,000-60,000/=

Bunge la CCM limebariki wakijua hamna kitu cha kuwafanya, mpo mpo tu maana wamewafanya mengi mkibaki mpo mpo tu.

Pengine ongezeko hili litawafundisha wakulima, wafanyabiashara na wafanyakazi wao ni nani?! Siku mkijitambua hamtafanyiwa mambo ya hovyo kama haya.
 
Achana na kodi ya miamala ya simu. Kuna kodi ya pembejeo ambayo kelele zake hazijasikika. Serikali imepandisha kodi ya pembejeo za kilimo ili kukomoa wakulima. Mbolea ya kupandia mazao aina ya DAP imeongezeka bei kutoka 52,000= hadi 92,000/= Mbolea za kukuzia Mf.UREA kutoka 48,000/=na sasa ni 80,000/= na CAN kutoka 40,000-60,000/=...
Natamani wangeongezewa hata mara mbili ya ilivyo Sasa ili ni thibitishe uzalendo waliokuwa nao,au ni umbumbumbu kwa mgongo wa uzalendo.
 
Huko ambako serikali inaheshimu matakwa ya umma, siyo kwa sababu viongozi walikuwa watakatifu bali wananchi walikataa kata kata kuburuzwa.

Huku ambako funguo zote za maisha tumewakabidhi watawala, tuwe tayari kufanya chochote mtawala anachokitaka.

Kuhusu katiba mpya ambayo ingetusaidia wananchi kuwa na nguvu dhidi ya watawala, badala ya kuungana, tumebakia kubishana na kucharuana wenyewe. Basi, tuendelee, na serikali ifanye chochote inachokitaka. Hii kodi waipeleke mpaka kule kwenye ving'amuzi na kwenye luku ili matrilioni yapatikane ya kuhudumia watawala. Uliwahi kumsikia punda akidai pilau japo yeye ndiye anayebeba magunia ya mpunga huko vijijini?
 
Pembejeo zinapanda, uku Bei ya mazao inazidi kushuka.

Kwasasa kilo ya mchele mikoani (bonde la kilombero) imefikia 500 sh kwa kilo[emoji3525]

Sijajua Ni mnyonge gani serikali inayojinasibu kumsaidia[emoji20]
hatari sana mkuu
 
Back
Top Bottom