Rais Samia kweli umedhamiria kukusanya Kodi za dhuluma hadi kwenye mbolea?

Rais Samia kweli umedhamiria kukusanya Kodi za dhuluma hadi kwenye mbolea?

Achana na kodi ya miamala ya simu. Kuna kodi ya pembejeo ambayo kelele zake hazijasikika. Serikali imepandisha kodi ya pembejeo za kilimo ili kukomoa wakulima. Mbolea ya kupandia mazao aina ya DAP imeongezeka bei kutoka 52,000= hadi 92,000/= Mbolea za kukuzia Mf.UREA kutoka 48,000/=na sasa ni 80,000/= na CAN kutoka 40,000-60,000/=

Bunge la CCM limebariki wakijua hamna kitu cha kuwafanya, mpo mpo tu maana wamewafanya mengi mkibaki mpo mpo tu.

Pengine ongezeko hili litawafundisha wakulima, wafanyabiashara na wafanyakazi wao ni nani?! Siku mkijitambua hamtafanyiwa mambo ya hovyo kama haya.
Ww ndio ulimuombea mabaya Magu....
kaa kwa kutulia hatujakusahau
 
Wananchi wa marekani na nchi za ulaya zinawasikia Watanzania kuwa hawataki kulipa kodi eti wanataka wasaidiwe.

Aisee!

Ngoja wanachi wenzetu watusikie! Sijui watatuonaje, kweli tumekomaa au tulidekezwa mpaka ukubwani?
Hakuna anayekataa mhlipa kodi. Wanapinga kodi isoyolipika, inayoumiza
 
Kila tukiimba hapa kuwa CCM ilishafeli kuongoza hili Taifa hamsikii.Sasa mtaelewa kwa matendo yao.
 
Haya yote yanayoendelea nadhani tunayaona na hii itoshe kusema CCM hawana nia tena na kuongoza nchi.

Mmeongeza Kodi sawa, ndio iwe mara mbili? Ongezeko la 100% tena kwa kipindi hiki? HAPANA

Mama hii ni Kodi ya dhulma, haikubaliki. Watanzania wengi wamejiajiri kwenye kilimo lakini napo umeamua kuongeza kodi mara mbili kwenye mbolea.

Kweli tutaisoma namba, sasa hivi kila kitu beini mara mbili ukiuliza unaambiwa kodi mpya. Tutakoma.

Wale wakulima wenzangu kazi tunayo

Nilitegemea mama katika jitihada zako za kukuza uchumi basi ungepunguza haya makodi hasahasa kwenye sekta ya kilimo, Ila imekuwa vice versa

Huyo ndiyo kipenzi cha watu na kodi ya dhuluma.
 
Tulilalamika mwendazake anaharibu uchumi Kwa kuwabana matajiri walipe Kodi, Sasa mama anataka wote tulipe kodi bado tunalalama. Mnataka Kodi alipe nani?
Mama ongeza kuupiga mwingi!
 
Nimekuwa naunga mkono tozo mbalimbali kama miamala na mafuta ila hili la mbolea hapana,hapa sijui Waziri alifikiria nini..kama hafai akae pembeni maana it is too much hiyo bei ni mara 2
 
Tulilalamika mwendazake anaharibu uchumi Kwa kuwabana matajiri walipe Kodi, Sasa mama anataka wote tulipe kodi bado tunalalama. Mnataka Kodi alipe nani?
Mama ongeza kuupiga mwingi!
Hakuna cha maskini wala nini mimi naunga mkono hizi tozo kila mtu alipe
 
Kwa nini wasizalishe ile mbolea ya minjingu ili ipatikane kwa bei nafuu kwa wakulima..
 
Haya yote yanayoendelea nadhani tunayaona na hii itoshe kusema CCM hawana nia tena na kuongoza nchi.

Mmeongeza Kodi sawa, ndio iwe mara mbili? Ongezeko la 100% tena kwa kipindi hiki? HAPANA

Mama hii ni Kodi ya dhulma, haikubaliki. Watanzania wengi wamejiajiri kwenye kilimo lakini napo umeamua kuongeza kodi mara mbili kwenye mbolea.

Kweli tutaisoma namba, sasa hivi kila kitu beini mara mbili ukiuliza unaambiwa kodi mpya. Tutakoma.

Wale wakulima wenzangu kazi tunayo

Nilitegemea mama katika jitihada zako za kukuza uchumi basi ungepunguza haya makodi hasahasa kwenye sekta ya kilimo, Ila imekuwa vice versa

wee unazani huyo samia asipokusanya kodi atakula nini na vibaraka wake? na maisha ya gharama watayatolea wapi?
 
Back
Top Bottom