Rais Samia kweli wewe ni mama

Rais Samia kweli wewe ni mama

lukala

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
594
Reaction score
590
Habari za asubuhi ndugu zangu, hakika kwenye huu ukanda wetu inawezekana huyu mama is a best president Kwa Sasa, nimeangalia mambo mengi kuhusu utawala wake.

Mosi, Kuhusu utumishi Bora na Sheria kwa Sasa hatuwasikii watumishi wakilalamika Sana Kuhusu stahiki zao kama mwanzo, mfano madaraja au stahiki zao zingine. Naona anajitihidi kwenda na Sheria zinazoendana na mikataba ya kazi kama inavyofasema. Zipo changamoto chache za kibinadamu.

Pili, kilimo na viwanda, hapa mama upande umoja amefanya better than other, kwenye kilimo hakika mama amefanya vizuri Sana Kwa msimu huu,. Na hii imetokana na mabadiliko makubwa ya sera. Nafikiri Kwa mara ya kwanza tunaweza kuwa nchi yenye uzalishaji mkubwa agricultural output na hii kutokana pia na ruzuku ya mbolea. Hakika hapa mama kapiga kazi inayooneka.

Changamoto ya hapo juu Kwa fikra zangu uzalishaji huo ukiendana na viwanda vya ndani, kwamaana soko la mazao yetu yasitegemee soko la nje Bali litegemee ndani. Ushauri wangu mama hapa ungeangalia uwezekano wa kumtafuta mtu sahihi kwenye wizara ya biashara na viwanda kuanzia katibu mkuu Hadi waziri Ili kuendana na Kasi ya waziri wa kilimo pamoja na katibu wake. Kwangu Mimi mama nakuomba jaribu kumwangalia Charles Kimea anaweza kukusaidia zaidi kwa hii wizara.

Tatu, kwenye huduma mama umefanya vizuri Sana Kwa miundo mbinu lakini Sina hakika kwenye huduma. Mfano mama amejenga madaraja mengi mashuleni,. Amejenga zahanati nyingi mijini na vijijini pia tunaona miundo mbinu ya maji na umeme lakini hofu yangu IPO Kwa huduma zitolewazo Kwa watu.

Changamoto iliyopo hapa ni baadhi ya ukilitimba Kwa baadhi ya viongozi waliopo chini , mfano mama umepata /umemweka waziri wa elimu Bora kabisa Adolf Mkenda kwangu huyu tulichelewa kumpata aina ya waziri kama huyu. Ninachoomba hapa mama hapa kwenye utoaji huduma uangalie mfumo mpya wa upatikanaji wakuu wa idara mfano engineer wa maji mkoa au wilaya, afisa elimu pamoja na wakuu wa shule na idara zinazoendana katika utoaji huduma.

Pendekezo langu hapa Hawa wakuu wa idara tuondoe mfumo wa uteuzi twende na mfumo wa kutangaza ajira na kwenda kufanya interview na respondents wawe na blue print watafanya nini kibotesha huduma hizo ktk maeneo husika atakayokutana nae pia pawe na mkataba wa muda mfupi mfupi kwenye upimaji wake wa utendaji.

Hii itasaidia kuongeza ufanisi wa kazi Kwa wakuu wa idara lakini pia itapunguza gharama ya kuvunja mkataba.

Asanteeni nawatakia asubuhi njema, karibuni Namanyere Kwa kilimo.
 
Habari za asubuhi ndugu zangu, hakika kwenye huu ukanda wetu inawezekana huyu mama is a best president Kwa Sasa, nimeangalia mambo mengi kuhusu utawala wake.
Kimei hawezi kilimo na umuhimu wa kilimo sio mtu ni uwezekezaji,hivyo ni fedha
 
Back
Top Bottom