Samahani hapa sioni mantiki. Nani analazimishwa, na nani, kwa njia gani? Wale wanaopiga alarm si "wazungu", ni Waafrika katika kitengo cha Afrika ya WHO.
“It’s a sad day for Africa. Our hearts go out to everyone who has lost friends and loved ones. Deaths have peaked week-on-week on the continent and after a slight dip, COVID-19 cases are surging again. The latest data tells us that Africa is still on the crest of the third wave, still recording more cases than in any earlier peak, and that we cannot take anything for granted,” said Dr Phionah Atuhebwe, New Vaccines Introduction Officer at WHO Regional Office for Africa. Record weekly COVID-19 deaths in Africa
Nakubali kwamba nchi kadhaa waliona wanakili tu chochote kutoka Ulaya, ambayo haikuwa chaguo zuri. Lakini kwa bahati mbaya hapa TZ siasa ilishindwa na hofu-ya-hofu, yaano hofu kwamba watu hawaelewi kitu watapaniki. Labda mkuu mwenyewe alipendela kusikia watu kama yule Askofu Simama ambaye ni dhahiri haelewi kitu...
Ukiangalia takwimu ya vifo ktk Afrika vinavyohusiana na Covid , Afrika Kusini inaongoza kabisa!
View attachment 1922484
Kwa nini??
a) wana asilimia kubwa ya watu wenye umri wa juu
b) wana mfumo wa afya unaoweza kupima (tofauti na hapa)
Linganisha umri South Africa / Uganda (Tanzania sijapata sasa)
View attachment 1922469
Lazima tatizo ni kubwa zaidi kuliko kwetu (nahisi tuko sawa na Uganda). Kule Ulaya ni kali zaidi, pia kisiasa kwa sababu wazee ni sehemu kubwa ya wapiga kura. Afrika Kusini nadhani tatizo ni tabianchi pia, hapa TZ mji mkubwa ni Dar, watu wenmgi hawaishi katika vyumba vulivyofungwa, wengi wana madirisha bila kioo, hewa inapitapita; Afrika Kusini tofauti wana madirisha ya kioo, hewa inabaki ndani pamoja na pumzi lenye virusi.
Ila: kufikiri hapa hakuna tatizo - ni ujinga. Mara hospitali zinajaa, hakuna nafasi ´kwa wagonjwa wa kawaida. Maisha yanaendelea, na mazishi yanaendelea yakiongezeka. Si kama Ulaya, lakini wazee wanakufa, wenye magonjwa mbalimbali ya awali maisha yanafupishwa.