#COVID19 Rais Samia: Kwenye hili janga la Corona dunia imekubaliana na philosophy ya Magufuli

Wewe hukuwa unamuelewa au ni kuamua tu.
JPM hakupinga barakoa ila alipinga barakoa za nje na kupendekeza watu wajishonee.

Chanjo hakupinga ila alitahadharisha kupewa chanjo Bila kujiridhisha,ndiyo maana akaunda kamati ya Corona juu ya chanjo ipi itafaa kulingana na mazingira yetu.

Alisema kweli wanapochanjwa ndo Corona inaongezeka,waulize Rwanda,Uganda yanayowapata.
 
Alisema kweli wanapochanjwa ndo Corona inaongezeka,waulize Rwanda,Uganda yanayowapata.

..kama Magu alisema hicho ulichosema hapo juu maana yake alikuwa anapinga chanjo.

..Na mitizamo ya Magu ndio imesababisha shida na ugumu kwa serikali ya awamu ya 6 kuwashawishi wananchi kuchukua hatua za kujilinda.
 
..SSH katoka kudungwa chanjo halafu anasema amekubaliana na falsafa ya Magufuli kuhusu covid 19!!
Una uhakika gani kama kachomwa chanjo au kachomwa placebo acha ujinga, hizi mambo za siasa achana nazo.
 
Mbowe mwenyewe alianzia ccm… Msipoke tu

slaa had a strong vision ya chama na nchi

Dj squint ana vision moja tu, kukamua Pesa za wafadhili wake
Toa ushahidi wa Mbowe akiwa CCM, unadhani traitor kama Slaa mtu ambaye hakuwa akiamini katika kupigania demokrasia mpaka mwisho angeweza kuvumilia economic sabotage kama anayofanyiwa Mbowe.
Ukiona mboga mboga wanamsifia mtu ujue hana nia njema au hakuwahi kuwa na nia njema na kupambania demokrasia kwa dhati, bare that in your mind, jinsi mboga mboga wanavyochukia mageuzi then wamsifie mwana mageuzi au aliyewahi kuwa mwana mageuzi uliiona wapi hiyo. That shit can't be real.
No pindi ukiona mboga mboga wanamchukia mtu wa opposition ujue huyo ni real deal and he/she is the pain in their goddamn ass buts.
 
Umeanza vizuri.
Umemaliza kwa kuingiza siasa kwenye suala la kisayansi.
 
Unayemuita traitor alikiacha chama na wabunge zaidi ya 100
Alikikuta na akakiacha, ni chama na hakuna mtu ambaye singlehandedly alifanya kila kitu.
Huwa kuna behind the scene strategists na kuna watu wa majukwaani lakini opportunists na traitors huwa wanajidhihirisha wenyewe as the going gets tough.
 
Kaka habari unapata wapi?? Au unajipikia mwenyewe??
Pale ambako wengi wamepata chanjo vifo vimepunga saaaana pamoja na watu kupelekwa hospitali. Sana! Hii ni siri ya nchi nyingi za Ulaya kuachana na vizuizi siku hizi.
Maambukizi bado yapo, yanapanda na kushuka na kupanda na mawimbi ya virusi, lakini hutokea kati ya
a) watu waliokataa kuchanja
b) vijana wadogo ambao bado hawakupewa chanjo
c) watoto chini ya umri wa miaka 12 kwa sababu chanjo hadi sasa hazina data za kutoshu kuhusu kundi hilo.

Ila kundi a) inazidi kupungua, makundi b) na c) hawaathiriwi mno kama wazee, maana mara nyingi wanaona dalili za mafua tu.
Isipokuwa vifo hutokea hata haoa.
 
Magufuli anaichojoa nguo dunia nzima na chadema ndio kinazidi kufubaa.


NB:MIMI NI TIMU MAGUFULI JANA,LEO,KESHO NA HATA MILELE.ameni!

Wala usijishangae Gwajiboy anaiita hali hiyo kuwa ni Stockholm syndrome
 
Hukuona habari za Seychelles iliyokuwa ikongoza kwa kuchanja watu wake mlipuko uliotokea?
Sisi hatujawahi kuwa na lockdown na hatujachanjwa na maisha yanaendelea unasemaje hapo?

Maadam chanjo wameleta wazungu hata Kama haileti tija lazima itumike tu.
Nyerere angekuwa na akili Kama zako angedai Uhuru?
 
MAisha yanaendelea, pamoja na mazishi yaliyoongezeka.
HApa hali ni tofauti kuliko kwa mfano Ulaya. Sababu ni muundo tofauti wa umri wa wananchi. Kama wengi ni vijana (kama TZ), "lockdown" si lazima. Lakini kuwaelimisha watu kuepukana na msongamano usio lazima na kuvaa barakoa ni lazima.
Seychelles ni nchi ndogo, watu chini ya lakhi 1. Kwa hiyo wanaweza kupima wengi sana,m wana data. TZ ni nchi kubwa, mahali pengi hawawezi kupima, na siasa imeamua kuficha data. Hadi leo.
Swali kuu si idadi ya maabukizi pekee, lakini idadi ya watu wanakuwa wagonjwa vibaya na wanaokufa. Pia wangapi wanafika hopsitalini, kwa sababu wagonjwa wa ugonjwa wa mlipuko wanajaza nafasi maana wengine wanakosa matibabu au wanachelewa kuyapata.

Nisipokosei si Wazungu walioleta chanjo, bali ni wenyeji walioomba kuipata wakaichukua. Kinyume chake Wazungu waligoma mwanzoni kutoa chanjo kwa nchi za Adrtika kwa sababu walitaka kuchanja watu wao kwanza. WHO wamelalamika mara kwa mara. Soma habari, nduhu!!!
 
Kwa sehemu uko sawa lakini tatizo la Corona tunalazimishwa liwe kubwa Afrika wakati si kubwa hata kidogo.
Fikiria watu zaidi 4m.waliokufa duniani Afrika Labda Sasa ndo imefika laki tatu.
Tatizo wazungu wanataka kujenga hofu dunia yote kuwa corona ni hatari tujifungie waendelee kuzikopesha Serikali kuhudumia watu wake,kununua vipimo vya Corona,mask, chanjo nk.

Umewahi kujiuliza kwanini nguvu haelekezwi kwenye dawa ambazo zimewaidia watu wengi kupona baada ya kuugua?.
Badala yake inavyopigiwa debe utafikiri ukiugua tu lazima ufe.
Tatizo Sasa hata mwenye Asthma,kifua kikuu,au ugonjwa wowote unaohusisha mfumo wa upumuaji ataingizwa ni mgonjwa wa Corona ili kuhalalisha kuendelea kupata mikopo mizuri ya kupambana na Corona.
 
Samahani hapa sioni mantiki. Nani analazimishwa, na nani, kwa njia gani? Wale wanaopiga alarm si "wazungu", ni Waafrika katika kitengo cha Afrika ya WHO.
“It’s a sad day for Africa. Our hearts go out to everyone who has lost friends and loved ones. Deaths have peaked week-on-week on the continent and after a slight dip, COVID-19 cases are surging again. The latest data tells us that Africa is still on the crest of the third wave, still recording more cases than in any earlier peak, and that we cannot take anything for granted,” said Dr Phionah Atuhebwe, New Vaccines Introduction Officer at WHO Regional Office for Africa. Record weekly COVID-19 deaths in Africa
Nakubali kwamba nchi kadhaa waliona wanakili tu chochote kutoka Ulaya, ambayo haikuwa chaguo zuri. Lakini kwa bahati mbaya hapa TZ siasa ilishindwa na hofu-ya-hofu, yaano hofu kwamba watu hawaelewi kitu watapaniki. Labda mkuu mwenyewe alipendela kusikia watu kama yule Askofu Simama ambaye ni dhahiri haelewi kitu...
Ukiangalia takwimu ya vifo ktk Afrika vinavyohusiana na Covid , Afrika Kusini inaongoza kabisa!


Kwa nini??
a) wana asilimia kubwa ya watu wenye umri wa juu
b) wana mfumo wa afya unaoweza kupima (tofauti na hapa)
Linganisha umri South Africa / Uganda (Tanzania sijapata sasa)

Lazima tatizo ni kubwa zaidi kuliko kwetu (nahisi tuko sawa na Uganda). Kule Ulaya ni kali zaidi, pia kisiasa kwa sababu wazee ni sehemu kubwa ya wapiga kura. Afrika Kusini nadhani tatizo ni tabianchi pia, hapa TZ mji mkubwa ni Dar, watu wenmgi hawaishi katika vyumba vulivyofungwa, wengi wana madirisha bila kioo, hewa inapitapita; Afrika Kusini tofauti wana madirisha ya kioo, hewa inabaki ndani pamoja na pumzi lenye virusi.

Ila: kufikiri hapa hakuna tatizo - ni ujinga. Mara hospitali zinajaa, hakuna nafasi ´kwa wagonjwa wa kawaida. Maisha yanaendelea, na mazishi yanaendelea yakiongezeka. Si kama Ulaya, lakini wazee wanakufa, wenye magonjwa mbalimbali ya awali maisha yanafupishwa.
 
Duh
 

Kuna mahali Magufuli au serikali hii wametamka neno "janga?"

"... Magufuli kuwa ugonjwa wa Corona ni janga .."

Msimuwekee shujaa aliyeidharau korona maneno mdomoni, nayo ikamdharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…