Rais Samia: Lazima tukusanye Pesa zetu za ndani huko nje masharti yamekuwa yakiongezeka

Rais Samia: Lazima tukusanye Pesa zetu za ndani huko nje masharti yamekuwa yakiongezeka

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi, akiwahimiza wafanyabiashara na wananchi kutambua kuwa kodi ndio msingi wa uendeshaji wa Taifa.

"Ndugu zangu wafanyabiashara, lazima tulipe kodi. Hamna nchi inayoendeshwa bila kodi. Hata hao wanaotusaidia, pesa wanazotupa ni za walipa kodi wao,"

"Mwanaume mzuri ni yule anayeendesha vizuri nyumba yake. Sisi kama Serikali lazima tukusanye kodi ili tuiendeshe nyumba yetu vizuri, na wananchi waridhike na huduma tunazowapa." amesema Rais Samia

Pia amewakumbusha wananchi kuwa bila ukusanyaji kodi Taifa haliwezi kusimama, kwani kodi ndio maendeleo na Serikali ikishindwa kukusanya kodi wananchi watakuwa watumwa.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Juni 16, 2025 wilayani Bariadi mkoani Simiyu, wakati akizindua jengo jipya la ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani humo.

 
Rais Samia Suluhu amesihi wafanyabiashara kulipa kodi ipasavyo ili kukusanya fedha nyingi za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ili nchi ipunguze kukopa.

ni muhimu sana na ni jambo la maana sana kujifunga mkaja na kujitegemea kiuchumi, kijamii na kisiasa, na huo ndio msingi imara sana wa taifa letu kuhemishika zaidi duniani.

well done Dr Samia suluhu Hassan kipenzi cha waTanzania wote 🐒
 
Rais Samia Suluhu amesihi wafanyabiashara kulipa kodi ipasavyo ili kukusanya fedha nyingi za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ili nchi ipunguze kukopa.

Lakini tulikuwmbia mama ulipoanza ukatupuuza na kuwasikiliza hao Chawa ambao Leo umeingizwa kwenye mtego wanakuacha peke yako

Huwezi kuendeleza nchi na hao Chawa ambao hawajui hata jinsi ya kuzalisha zaidi ya kutumia mikopo hiyo kujinufaisha binafsi na familia zao ...Ifikie hatua useme pia kuwa ajira zinatengenezwa na serikali siyo kazi ya Vijana kujiajiri, hiyo lugha ni potofu na hasara Kwa nchi.

Ajira zinazoratibiwa na serikali zinawezesha matumizi bora ya ujuzi na nguvu kazi ya Vijana. Ukitaka tutoke huko kubali kuacha teuzi zembe watu wapewe nafasi kwakushindanishwa na wale wenye mawazo chanya wapewe nafasi kuongoza maendeleo, otherwise utaishia kulazimisha mambo Kwa nguvu ya Dola badala ya ridhaa za wananchi
 
Rais Samia Suluhu amesihi wafanyabiashara kulipa kodi ipasavyo ili kukusanya fedha nyingi za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ili nchi ipunguze kukopa.

ITAFIKA KIPINDI WAFANYA BIASHARA WATALIPIA KODI YA "BUSINESS PLAN"
WASHAKOPA KIASI KWAMBA WANAONA AIBU KUONGEZA DENI!!
HIZO KODI WALIZOKATA MIAKA YOTE WAKIONGOZA HII NCHI PLUS NA MADENI WALIOKUWA WANAKOPA MIAKA YOTE!!
KODI ZETU WANALIPIA MISHAHARA NA KUJAZAA MATUMBO MIKOPO WANATUMIA KWA MATUMIZI BINAFSI ASILIMIA CHACHE ZINAENDA KWAAJILI YA MAENDELEO
VIONGOZI WANAJUA WANANCHI NI WAJINGA SANA
 
Rais Samia Suluhu amesihi wafanyabiashara kulipa kodi ipasavyo ili kukusanya fedha nyingi za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ili nchi ipunguze kukopa.

Mpumbavu ni Mpumbavu tu watu walipo sema hivi alipinga ...kaona jumuia za kimataifa wamesha mjua kuwa ni mpumbavu ndiyo anajidai kuongea hivyo wakati speaker wa bunge ndugai aliposema hivyo walimwambia aje
 
Back
Top Bottom