Rais Samia: Lazima tukusanye Pesa zetu za ndani huko nje masharti yamekuwa yakiongezeka

Hapa kuna luga gongana, mawaziri wake wanasema tunapata mikopo yenye mashart nafuu, bibi anasema mashart ni magumu, sasa tuwe upande wa bibi au mawaziri wetu
 
Tupambane wenyewe kwakweli
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ndo kastuka sasa hivi Baada ya kuyakogoroga kwahiyo sasa hivi hata safara zitakuwa hamna
 
Mheshimwa Raisi punguza matumizi ya Serikali kama kununua magari kila mwaka,posho kubwa na mishahara mikubwa ya viongozi!Haiwezekan zaidi ya nusu bajeti inaenda kwenye kulipana mishahara na anasa za viongozi!Bila hivyo utatukamua lakin hatutofika!
 
Hivi watanzania tulimkosea nini Mungu?
 
Kama Kuna mtu anamuelewa huyu basi peponi atapasikia
 
My Take
Na hili Machadema yatapinga na kuanza kutukana hovyo πŸ˜πŸ˜πŸ‘‡πŸ‘‡
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa Watanzania kujiamini kwa kujitegemea kiuchumi badala ya kutegemea misaada ya nje, akisisitiza kuwa nchi inaendelea kufanya vizuri kiuchumi licha ya changamoto za kidunia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Simiyu, Rais Samia alisema hali ya kiuchumi duniani imeyumba kutokana na migogoro, vita na kushuka kwa uchumi, hali inayozifanya nchi wahisani kuwa na masharti magumu ya misaada.

"Ukitegemea msaada, dunia yote sasa ipo juu chini... Ulaya na Marekani kwa sasa hawafanyi vizuri kiuchumi kama tunavyofanya sisi hapa Tanzania," alisema Rais Samia.

Aliitaka TRA kukusanya kodi kwa njia rafiki, akieleza kuwa watoza kodi wanapaswa kushirikiana na wafanyabiashara badala ya kuwa maadui. "Mwite mfanyabiashara, zungumza naye, muulize anaweza kulipa kiasi gani. Serikali inapata hata kama ni kidogo," alieleza.

Hata hivyo, alionya kuwa kwa wale wanaokaidi kulipa kodi kwa makusudi, hatua kali zitachukuliwa. "Wapo wengine wana viburi – hao tunashughulika nao," alisema.
Your browser is not able to display this video.
 
..tulipe kodi ili Samia na genge lake waishi maisha ya fahari.

..CAG kasema serikali ilitumia billion 500+ ktk mambo yasiyo na faida kwa nchi.
 
Hela nyingi zpo local government authority nazo zitoe Gawio sio Kila wanachokusanya wanakula tu

Watumishi wa TRA wapunguze kukaa ofcn una kadiriaje biashara ya mtu bila kufika site ? Kodi nyingi sana zinapotea watu hawalipi uhalisia
 
Vile vikosi kazi vya 'kukwapua' fedha za watu benki nahisi vitarejea hapo mwakani.

Dhuluma za kisiasa zimerndelezwa, dhuluma za kiuchumi zinakaribia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…