Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Leo kwenye mkutano huko Malawi alipoenda mama yetu raisi wetu amesema lengo ni wananchi wote wachanjwe. Sasa najiuliza ni ndani ya huu mwezi mama alisema chanjo ni hiari anayetaka atachanja na asiyetaka hatachanja.
Ipo hivi kwenye Jambo lolote lile hata liwe la umuhimu kiasi gani ni lazima kuwe na pande mbili, ndio maana unaona Kuna watu wapo wengi tu hawaamini uwepo wa Mungu.
Hivyo hata kama chanjo zingekuwa na faida kiasi gani ni lazima Kuna watu wengi tu wangekataa, sasa hili suala la kusema wananchi wote wachanjwe itawezekana vipi?
Au Kuna mipango ya kuanza kuweka vikwazo kwa wasiochanjwa? Je ile hiari ambayo mmekuwa mkiisema ipo wapi?
Lakini pamoja na yote hayo nina uhakika bado hamtaweza kuchanja watu wote, hata zitumike mbinu za aina gani. Tusubiri muda
#mbowe sio gaidi#