Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka machifu nchini kote kujenga mvuto ili watu wakimbilie kwao wanapokuwa na migogoro badala ya kila kesi kupelekwa polisi na kisha mahakamani.
Amesema ili jamii iwakimbilie ni muhimu wajenge mazingira ya uadilifu, uaminifu na kutenda haki na kwamba anaamini jambo linaloamliwa na viongozi wa kijamii linakuwa na mazingatio pia kwa jamii.
Halikadhalika amewataka machifu kusimamia amani katika maeneo yao pamoja na kuhakikisha mazingira hayaharabiwi hovyo.
“Dhamana yetu kubwa sisi machifu ni kuona Watanzania wanaishi kwa amani na pia kuona mazingira yanalindwa,” amesema Rais Samia anayejulikana pia kama Chifu Hangaya.
Amewashangaa machifu kuona mambo kama ugomvi wa wakulima na wafugaji unatokea hadi watu kuuana katika maeneo yao wakati wao machifu wapo. Hivyo amewasihi kwenda kusimamia hilo.
Amewasisitiza kuwa watu wenye maadili na waaminfu katika jamii na kwamba haipendi kuona chifu anakamatwa na polisi kwa makosa mbalimbali kwa kuwa ni kiongozi wa jamii anayepaswa kujijengea heshima pia kutokana na kufanya matendo mema.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Rais Samia: Machifu waambieni wanasiasa ukweli vyeo havipatikani kwa kuua watu