Rais Samia: Majengo 122 yamejengwa nchini kuboresha huduma kwa Wananchi!

Rais Samia: Majengo 122 yamejengwa nchini kuboresha huduma kwa Wananchi!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ziara ya Rais Samia Lushoto - Tanga Februari 24, 2025


"Nimekuja kuangalia matumizi ya fedha mbalimbai zinazoletwa kuondoa shida za wananchi, nimekuja kuangalia kama kweli zimeondoa shida za wananchi, nami sitaki nilaumu nataka niseme kwa kiasi kuubwa jana na leo nimeona fedha zimetumka vizuri"

"Leo katika kuanza siku yangu nilikuwa Bumbuli ufungua Jengo la Halmashari, ni jengo nzuri na jengo linalfurahisha machoni, lakini madhumuni ya jengo lile ni kusogeza huduma karibu na Wananchi na huduma zote za Halmashauri ziwe ndani ya jengo moja. Lengo kubwa ni kuimaisha utawala bora, Litumieni jengo lile kwa huduma mnazozitaka, jengo ni mali yenu litunzeni"

"Wafanyakazi wa ndani ya lile jengo, jengo lile ni nzuri kwa nje nataka pia liwe nzuri kwa ndani kwa huduma zinazotolewa kwa Wananchi, sio tu kuingia pale raha na viyoyozi zilivyomo mle ndani halafu huduma kwa wananchi hakuna...[hapana]"

"Katika kipindi hiki tumejenga majengoya aina ile katika michoro mbalimbali kuingana na mazingira ya sehemu, kwa Tanzania tumejenga majengo 122 katika kpindi hiki cha miaka 4, Halmashauri 122 zimepata majengo mapya na mazuri"
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa wilayani Lushoto katika muendelezo wa ziara yake mkoani Tanga tarehe 24 Februari, 2025.
 

Attachments

  • VID-20250225-WA0000.mp4
    20.6 MB
Back
Top Bottom