Rais Samia: Marehemu Magufuli alinifundisha mambo mengi na dhamira yake niliielewa vizuri. Dhamira ni ileile

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo Rais Samia yuko mkoani Geita na ameendelea kusisitiza wembe ni uleule kama awamu iliyopita.

=======

Rais Samia: Awamu iliyopita nilikuwa makamu wa Rais chini ya kaka yangu marehemu John Pombe Magufuli, alinifundisha mambo mengi sana, niliisoma dhamira yake vizuri sana jinsi ya kupeleka nchi hii. Niwahakikishie dhamira ile tunakwenda nayo.

Serikali yetu ya chama cha mapinduzi yeyote anayekaa kuongoza Serikali lengo ni kuhudumia wananchi na kupeleka maendeleo.
 
Mama keshawajulia mburula wa Sukuma gang 😆😆
 
Huyo ni MNAFIKI namba moja akiwawakilisha walamba Asali popote pale walipo nchini na watoto wao huko Diaspora.
 
Anasemaje kuhusu wanaosema nchi haikuwa na amani kipindi cha kaka yake? Na wale wanaosema watalii walikimbia kwa maelfu anawambia nini wana chato?
 
Ndio maana napenda siasa,, hadi raha
 
Angalau anatumia uwanja wandege wanaoubeza nyumbu humu,na ndege pia.
 
Alipokua nje ya nchi alimkana,daah meko anapigwa matukio hukohuko kaburini,mwingine alisema alikua na file LUTINDI HOSP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…