Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Binafsi, kama ilivyo kwa wengi, siamini Mbowe ametenda kosa lolote la ugaidi, bali naamini mashtaka haya ni ya uongo na ni ya kisiasa zaidi chanzo kikiwa ni yeye kuongoza harakkati za kudai Katiba Mpya kupitia chama chake(CHADEMA).
Rais Samia na wasaidizi wako, naomba niwambie tu kuwa Katiba ambayo Mbowe na chama chake wanaipigania, inaweza kuja kuwa msaada kwa watoto na wajukuu zenu kuliko hata kwa watoto au wajukuu wa Mbowe mwenyewe.
Tambueni, kwa Katiba hii, kesho anaweza kuja Mtawala ataeamua kuwanyang'anya mali mlizonazo kwa kuwatuhumu tu kuwa mali hizo mlizipata visivyo halali kupitia nafasi zenu kama viongozi wakuu wa nchi hii.
Hilo au lingine lolote la kufanana na hilo lkitokea, watao-suffer zaidi ni watoto, wajukuu au vitukuu wenu, na wala si watoto, wajukuu au vitukuu wa Mbowe.
Kumbukeni Sumaye kulalamika kuporwa mashamba yake wakati wa Magufuli na wengine kuambiwa wanawashwawashwa, hivyo kesho inaweza kuwa ni zamu yenu.
Katiba yetu ni mbovu kupindukia na ni katiba hii ndio ilipelekea watu kubambikiziwa kesi kitendo ambacho wewe kama Rais, ulikiilalamikia hadharani na ukaagiza kesi za aina hiyo zifutwe.
Jambo lingine,nyie kuwa wana-CCM, haimanishi kuwa watoto, wajukuu au vitukuu wenu watakuwa wana-CCM au wataiva na watawala wajao, hivyo kuna hatari watoto,wajukuu au vitukuu wenu kuja kutofautina na mtawala wa wakati huo na akawashughulikia kama jinsi ambavyo Mbowe leo hii anashughulikiwa.
Utawala wa Magufuli unapaswa kutufunza watanzania ubaya na hatari wa hii katiba, na tusipojifunza, iko siku tutakuja kupata Mtawala ambae tutamuona hata Magufuli alikuwa nafuu.
Maneno haya mnaweza msiyapende, ila iko siku mnaweza kuyakumbuka na tambueni leo nafasi zenu, hakuna anayeweza kuwaambia maneno kama haya isipokuwa sisi wananchi wa kawaida kupitia mitandao kama nilivyofanya kupitia hapa JamiiForums.
Kumbukeni huu msemo: Majuto ni mjukuu.