Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Kwa heshima na taadhima, Mhe Rais kuna kila dalili za upigaji katika Mamlaka hii. Kuna tetesi za chini kwa chini kuwa NCAA imewalipa waandishi wa habari pesa nyingi wakiongozwa na Maulid Kitenge chini ya Uratibu wa mmiliki wa gazeti la Jambo la habari ndugu Mchange. Nguvu wanayotumia ni kubwa sana waandishi hawa ili kuhalalisha maamuzi ya watu wachache kutaka kuihamisha Jamii ya Wamasai ndani ya hifadhi hiyo.
Hili suala Waziri analijua fika yupo kimya na pia kuna tetesi kuwa ametoa baraka zote kwa shughuli hii kufanyika. Kiukweli kabisa inaonekana wamelipwa pesa nyingi kwa kazi hii, kama hivyo hii bajeti imetoka wapi na kwa ridhaa ya nani? Mhe Rais mchunguze Waziri huyu na watendaji wote wa juu Wizara akiwemo Karibu mkuu na watendaji wa Mamlaka.
Haiwezekani na haitowezekana kumuondoa Mmasai kwenye eneo lake la asili, zaidi kinachotafutwa ni ugomvi na migogoro isiyoisha baina ya serikali na jamii ya Wamasai Waziri na watendaji wake wanataka kuamsha migogoro hii hatutofika. Maana ya hifadhi ya Ngorongoro ni pamoja na uwepo wa jamii ya Wamasai na mifugo yao na siyo wanyama pori tu.
Wizara hii ina tatizo Mama imulike kwa jicho kali, kuna uwezekano mkubwa wa pesa za umma kuliwa hapa.