Rais Samia Mgeni Rasmi AGM ya TLS: Wanasheria Tumweleze Ukweli Kuhusu Ubatili wa Katiba Yetu na Sheria Zetu, Turudishe Haki Kuu ya Msingi

Rais Samia Mgeni Rasmi AGM ya TLS: Wanasheria Tumweleze Ukweli Kuhusu Ubatili wa Katiba Yetu na Sheria Zetu, Turudishe Haki Kuu ya Msingi

Wanabodi,


Utambulisho

Mimi pia ni mwanasheria, ni member wa TLS, na wakili wa kujitegemea pia kwa kujitolea, ila mimi sijiiti wakili msomi, wala sijaanza kwenda mahakamani, namalizana kwanza na sekta ya habari ndipo niugeukie uwakili active, hivyo kwa sasa mimi ni wakili mtangazaji, niliyejikita kwenye utoaji wa elimu ya katiba, sheria na haki, kupitia makala zangu kwenye magazeti ya Nipashe kila Jumapili, na Mwananchi kila Jumatano, na pia nina kipindi cha TV on Channel Ten kinachoitwa KMT kinachorushwa kila siku za Jumapili, saa 3:00 usiku. Kikizungumzia, katiba, sheria na haki.
Paskali.
Baada ya TLS mbili oga zilizotangulia, nina imani na Mwabukusi, TLS hii ya sasa ni TLS moto!, tutampelekea moto wa haki, hadi huu ubatili wa Katiba na Sheria batili ziondoshwe.
Hongera Sana Wakili Boniface Mwabukusi
P
 
Baada ya TLS mbili oga zilizotangulia, nina imani na Mwabukusi, TLS hii ya sasa ni TLS moto!, tutampelekea moto wa haki, hadi huu ubatili wa Katiba na Sheria batili ziondoshwe.
Hongera Sana Wakili Boniface Mwabukusi
P
CCM huwa wanataka TLS wapeleke mapendekezo halafu " yataangaliwa", ndicho kitafanyika. wataambiwa wapeleke mapendekezo ya sheria zinazohitaji kurekebishwa baada ya hapo ni same old stuff.
 
Wanabodi,
Leo asubuhi nimeamka na habari njema sana kuhusu Mkutano Mkuu wa TLS.

Sasa maadam imejitokeza fursa ya TLS kuhutubiwa na Rais Samia, hii ni fursa adhimu na adhimu, kwa TLS tumweleze Rais Samia kuhusu ubatili wa katiba yetu unaonyima haki ya Watanzania kuchagua na kuchaguliwa! ambao wasaidizi wake hawamwambii, serikali yake imetutungia muswada batili wa sheria ya uchaguzi, Bunge likapitisha muswada huo, hivyo kukutungia tena sheria batili, na yeye akaisaini ianze kutumika na ubatili wake hivyo hivyo.

Sisi hatumlaumu Rais Samia kusaini sheria batili, kwasababu yeye sii mwanasheria kuujua ubatili huo, lakini wasaidizi wake ni wanasheria wanaujua fika ubatili wa katiba yetu na sheria zetu, , lakini hawamwambii, hivyo hii ni fursa, kwa TLS kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kumweleza ukweli Rais Samia, kuwa ni lazima tufanye kwanza mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms, ndipo twende kwenye uchaguzi.

Tumshauri Rais Samia kuwa Uchaguzi wa serikali za mitaa uhairishwe kwanza, tuondoe kwanza ubatili wa katiba, tufanye marekebisho ya sheria, ndipo twende kwenye uchaguzi, na uchaguzi huo wa serikali za mtaa, ufanyike siku moja na uchaguzi Mkuu na kusimamiwa na Tume moja huru na Shirikishi ya Uchaguzi!.

Paskali.
Wanabodi,
Nimekumbuka enzi zangu za kipindi cha Kiti Moto, mwisho wa kipindi tulikuwa tunataja anayefuata na kuweka heading tutamuuliza nini, kuna watu walikuwa wanaingia mitini, wanakula kona kwa kuogopa kukalia Kiti Moto.

Hivyo usikute ni bandiko hili, limesababisha .... naomba nisiendelee...

Mchana mwema.

P
 
Mwabukusi,mgeni akija piga spana, ni ushindi wako ndio umewafanya wachanganyikiwe na kuanza kuonea Vijana wa Mbeya na Viongozi wa CHADEMA.
 
Wanabodi,

Zawadi yangu kwa Birthday ya Mama nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.


Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
HBD Rais Samia!.
P
 
Back
Top Bottom