Rais Samia Mgeni Rasmi Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Songea

Rais Samia Mgeni Rasmi Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Songea

Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi chetu Samia Suluhu Hasssan, Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Tamasha la Kitaifa la Utamaduni litakalofanyika Songea.

Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni linatarajiwa kufanyika katika Mji wa Songea, mkoani Ruvuma, kuanzia tarehe 20 hadi 23 Septemba 2024. Lengo kuu la tamasha hili ni kuwakumbusha Watanzania kuhusu umuhimu wa utamaduni wetu na kuuenzi.

Tamasha hilo la siku nne litafunguliwa rasmi na Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro, huku kilele cha tamasha hilo kikitarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kauli mbiu ya tamasha hilo mwaka huu ni “Utamaduni Wetu ni Utu Wetu, Tuuenzi na Kuuendeleza, Kazi Iendelee”, ikisisitiza umuhimu wa kulinda na kuendeleza tamaduni za Kitanzania.

Soma Pia: Magu, Mwanza: Rais Samia ashiriki Tamasha la Utamaduni, Mila na Desturi za Tanzania, atawazwa kuwa Chifu wa Machifu


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili..
utamaduni ni miongoni mwa tunu za taifa na utambulisho wa utaifa wetu,

kila la kheri Mh.Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais na kipenzi cha waTanzania wote 👊💪
 
Imeandikwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Mhe.Rais Samia.
Siku ya tarehe 23 septemba 2024 mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atashiriki kujionea tamasha la kitaifa la utamaduni mkoani Ruvuma.
Tuenzi utamaduni wa mtanzania ambao mara zote unahusu amani kazi na furaha.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Ahsante

Luhuwiko tulimpokea Baba Mtakatifu Papa Yohane Paul I I

Songea imebarikiwa sana

Wewe ndiwe Petro na Juu ya Mwamba huu nitalijenga Kanisa langu! 😄🌹
 
Back
Top Bottom