BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Akizungumza kutoka katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), #RaisSamia amesema ongezeko la 23% la Mshahara lililofanyika mwaka 2022 halikuwagusa Wafanyakazi wote akiwemo yeye.
Amesema lengo la nyongeza hiyo ilikuwa kuwainua Wafanyakazi wa Kima cha Chini huku ikiongeza Posho kwa Wafanyakazi wenye Mishahara mikubwa ambao hawakufaidika na nyongeza ya 23%.
Aidha, ameongeza kuwa baadhi ya Taasisi hazikuweza kulipa Nyongeza na Posho hizo kutokana na kuwa Bajeti zao zilikuwa zimeshapitishwa, hivyo malipo hayo yatafanyika mwaka huu (2023).