Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Pumba tupu; kwani hujasema ni miradi gani isitishwe.Kuna watu watashangaa sana kwa kulisema hili, lakini sijakosea kusema hivyo! Nina maanisha
Sioni ulazima wa Mh Rais kubebeshwa mzigo ambao haku uasisi yeye, hata hayati Magufuli kuna miradi iliyoasisiwa na mtangulizi wake Mh Kikwete lakini yeye alivyoingia madarakani akaachana nayo, Yes tunatambua alikuwa Makamu wa Rais lakini siyo kweli kila alichopanga aliyekuwa Rais wa JMT hayati JPM basi Mama Samia nae aliridhia.
Mh Rais sasa ndio wakati wake wa kufanya lile analoliamini na kutambua lipo ndani ya uwezo wake ,
Watanzania watamkumbuka kwa yale atakayoyafanya na kuyakamilisha, Rais kuamua kuendeleza miradi mikubwa ambayo pengine hakuiridhia tunaweza kusema anajiingiza mtegoni pasipo kufaham kwani muda aliopewa kama Rais ni mchache sana na pengine asi accomplish hata asilimia 30% ya miradi aliyoiacha Magufuli.
Mh Rais chagua tena upya miradi michache uipe kipaumbele na ukiamini inatekelezeka katika mfumo wa makusanyo halali ya kodi,
Miradi mingi mtangulizi wako aliitekeleza kwa kodi nyingi za kubambikiza ambazo sasa wewe umeshasema wananchi wasibambikiziwe kodi, miradi mingi imetekelezwa kwa faini ya makosa ya uhujumu uchumi ambazo ni kesi zilizokuwa na chembe ya uonevu pia vilevile.
Miradi mingi aliyoiasisi mtangulizi wako haitegemei kodi halali za watanzania, inachochea deni la Taifa kupaa kila kukicha.
Narudia tena kukushauri Mh Rais fanya machache na wananchi watakukumbuka nayo;
Kwa mfano
1.Boresha Kilimo cha Mtanzania ikiwemo upatikanaji wa Maafisa ugani,Pembejeo za kilimo pamoja na masoko ya uhakika
2.Bima ya Afya kwa Kila Mtanzania, hili lipe uzito kamili
3.Utawala Bora wa Sheria na Uwajibikaji
4.Boresha miundombinu ya Hospitali kila mkoa, wilaya na kata
5.Boresha mazingira mazuri ya Kibiashara na Uwekezaji
6.Boresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama
7.Imarisha Demokrasia nchini
8.Dhibiti mfumuko wa bei hasa bidhaa za vyakula na ujenzi
9.Suala la KATIBA lipe kipaumbele na historia itakukumbuka Mh Rais
Kuna tofauti kabisa kati ya kurithi majadiliano na kurithi miradi iliyokwisha anza. JPM alirithi Uwanja wa JKN na ulikuwa katika hali mbaya sana financially hadi karibu mkandarasi ajitoe lakini yeye akauendeleza. Alirithi mradi wa Kigamboni nao ukiwa katika financial troubles akauokoa. Alirithi majadiliano ya Bandari ya bagamoyo, hakuridhiana nayo na bado majadiliano yalikuwa yanandelea hadi anatangulia mbele ya haki. Tofautisha miradi iliyokwisha anza na miradi ambayo bado iko kwenye majadiliano