Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 46,405
- 138,158
Kwanza anatakiwa atambue yeye ndiyo sababu kuu/chanzo kikuu cha hiyo misaada kuondoka.Rais Samia Suluhu, amewataka Watanzania na viongozi kukaza buti na kufunga mikanda kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yanayoendelea duniani, amesema hayo Agosti 3, 2026 katika uzindizi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 pamoja na kushiriki katika Mkutano wa Mazungumzo Maalum na Sekta Binafsi kuhusu Utekelezaji wa Dira 2050, Agosti 03, 2026
''Misaada na mikopo tuliyo izoea inaendelea kuondoka tukaze buti "
Jambo la pili anatakiwa atambue Kiongozi siku zote unatakiwa kuonesha mfano. Atuambie yeye kama yeye amekaza wapi hilo buti? Kuwataka wananchi pekee kukaza buti wewe kiongozi na wateule wako mkiendelea kujineemesha, haileti mantiki.