Rais Samia: Mishahara ya wafanyakazi wa CCM imepanda kwa 84% kwa watumishi wa chini na 25% kwa wale wa juu. TOT nao mishahara juu

CCM ina miradi kila kona vikiwemo viwanja vya michezo.

Lakini inapokea ruzuku pia kama Chadema!
Viwanja vya michezo ccm wameviteka. Vilitakiwa viwe viwanja vya serikali maana vilijengwa wakati wa mfumo wa chama kimoja na vilijengwa na serikali.

Kama wana ubavu wa kujenga mbona hawajajenga kiwanja chochote tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa miaka 30 iliyopita
 
Mwenyekiti wa CCM mh Samia Suluhu Hassan ambaye pia ndio Rais wa JMT amesema mishahara ya watumishi wa CCM imeongezeka kwa kuanzia 25% kwa watumishi wa ngazi za juu hadi 84% kwa watumishi wa ngazi za chini...
Na sisi wanachama wa CCM Nchi nzima tumepunguziwa mfumuko wa bei na makali ya maisha.
 
Mwenyekiti wa CCM mh Samia Suluhu Hassan ambaye pia ndio Rais wa JMT amesema mishahara ya watumishi wa CCM imeongezeka kwa kuanzia 25% kwa watumishi wa ngazi za juu hadi 84% kwa watumishi wa ngazi za chin...
Chadema Hela zote wanampa Lema,Mbowe na Mnyika
 
Wanajamvi, jana mama alisema ameongeza mishahara ya watumishi kwa asilimia 89 na 25 kwa wenye mishahara mikubwa. Je hii ni kweli? Kama ni kweli mbona mimi na jamaa zangu hatujaiona hiyo nyongeza? Au anaongelea mwaka huu ndo ataongeza?

Naomba ufafanuzi kwa aliyemwelewa mama yetu mpendwa.
 
Hizo ni "fix" tu........

Kwani bado hujawaelewa Hawa jamaa zetu maSisiem??
 
Nitazimia
 
Sikuelewa hotuba ya jana kwa kweli ilinisikitisha.
 
Watumishi walioongezwa mishahara na wa CCM,anapalilia njia yake ya 2025.

Watumwa wa umma wameifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati chini ila nyongeza ya mishahara kwa siyo muhimu na wanatakiwa kuchapa kazi inayoendelea.Hawana madhara kwenye kufanikisha uchifu wa Hangaya.

Hakuna maswali mengine?
 
Hujaelewa nini sasa!
Ameongeza kwa watumishi/viongozi wa Chama Chetu cha Mapinduzi.

KAZI IENDELEEEEE!
 
Kumbe taswira halisi ya kuufungua uchumi wa Tanzania tunaipata kwa kupitia mishahara ya wafanyakazi walioajiriwa na CCM na wala siyo tena kwa watumishi wa umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…