Binafsi huwa najiuliza Chadema wana lengo gani hasa na Harakati zao hizi za Siasa. Huwa nawaza mambo mawili, Aidha wanafanya siasa zao kwa lengo la kuwaridhisha watu fulani ambao wanawafadhili ili waendelee kuwapa fedha au Hawajui watanzania ni watu wa namna gani inapokuja suala la Siasa.
Unapojiita chama ambacho ni cha kuwasemea watanzania, na unaitisha Maandamano au uko kwenye kuonewa na dola na unaitisha Maandamano lakini watu hao hawajitokezi, lazima ujiulize mara mbili, nini shida? Je, ninachokipigania ndicho wanachokihitaji? Je, njia ninayoitumia ndio wanayoitaka? Je, wako tayari kujitolea kiasi gani? Mimi nina aamini Chadema ni chama kikubwa kioganaizesheni, hivyo kinafanya tathmini na tafiti na kujua nini hasa watu wanataka.
Ukisoma mitandaoni juu ya katiba, unaona mjadala huu unazungumziwa zaidi Twitter, ukichunguza mitandao ya Instagram au Facebook ni nadra kukuta mjadala huu. Je, watanzania wanagapi wanatumia Twitter? Hao wanaotweet kuhusu Katiba ni watu wa kundi lipi? Je, ukifanya reflection huku mtaani Katiba inazungumziwa? Pita kwenye vijiwe, pita sokoni, nenda kwenye mabaa, zungukia kwenye makusanyiko ya harusi au misiba, je kuna mjadala wa katiba? Kama upo inajadiliwa katiba kama hitaji au kama tukio la mvutano wa kisiasa? Ukitathmini yote unaona kuna disconnect kubwa kati ya kinachodaiwa na Chadema na wananchi wenyewe huku mtaani.
Mwaka jana Lissu alizuiwa Kiluvya, jana yake alikuwa na kusunyiko kubwa la watu, lakini hawakujitokeza kupingana na Polisi, Mikutano yote Lissu alikuwa na 'mafuriko' ya watu, lakini alipoitisha Maandamano ya amani Nov 2, 2020 hata wanachama wa chama chake hawakujitokeza. Haya ndio mambo yanaleta maswali juu ya approach ya Chadema kwenye siasa za Tanzania.
View attachment 1862098View attachment 1862099View attachment 1862100View attachment 1862101View attachment 1862102