Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza umemtupia zigo la lawama? Elewa tu watu wanaamini ana baraka zako

Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza umemtupia zigo la lawama? Elewa tu watu wanaamini ana baraka zako

[emoji16]
AYrClH.jpg
 
Rais Samia napenda kukushauri, kwa sababu katiba ndo ilikupa hiyo nafasi na wala hukuwa potential candidate kwenye nafasi ya urais hata kama magufuli angemaliza muda wake, ni bora ungejikita kuweka misingi ya kiuongozi ambayo inaleta maelewano na kupunguza vurugu na chuki miongoni mwa jamii. Misingi hiyo ni pamoja na katiba mpya inayoridhiwa na makundi yote ya wananchi ambayo italeta tume huru ya uchaguzi isiyopendelea upande wowote. Usijaribu kukumbatia mifumo ambayo inakupa nguvu za kutawala kimabavu ili uendelee kukumbatia madaraka maana inaweza ku back-fire ikakuondolea credibility yako uliyoanza kuijenga kama kiongozi unayejali na kusikiliza changamoto za makundi yote ya watu katika jamii na utaishia kuingia kwenye kundi la watawala wakandamizaji jambo ambalo siyo zuri ukizingatia pia na jinsia yako....
 
Njia aliyoitumia Mbowe haikuwa muafaka wa kutoa kauli kama zile. Rais alionyesha kuwa licha ya kwamba alikuwa ni msaidizi wa aliyepita lakini kuna mambo alikuwa hafurahishwi nayo kwa kuwa mamlaka hakuwa nayo ilibaki kuwa kama ilivyokuwa ijapokuwa CCM bado ni CCM.

Kawatoa watu magerezani na kuwafutia kesi wakiwemo wapinzani. Wafanyabiashara ile task force iliyokuwa ikitumika kuchukua kodi ameivunja vunja na mengineyo tofauti tofauti. Ubabe wa viongozi kwa kiasi fulani umepungua na Uhuru kwa kiasi chake umerudi.

Sasa ni nini kilichomfanya Mbowe na Chadema kutoa kauli kali za namna ile? Kisa kuambiwa nipeni muda? Kwa nchi yetu ilivyokuwa ilikuwa inahitaji kushtuka Rais aliposema nipeni muda?
Acha ujinga muda wanini tangu Uhuru tunamiaka mingapi kama Taifa na hatusogei Kisha unaleta blah blah za muda
 
Yaani aiseee, mie nilipoona ile hotuba aliyoitoa Mama njiani Morogoro na kuwaonya wananchi kwamba' wasijejikuta wakaingizwa mkenge'.. basi nikajuwa tu yale matazamio chanya aliyowapa mwanzoni, sasa kibao kimegeuka na inabidi wawe wapole tu....... kazi iendelee.
Hawakusoma alama za nyakati
 
Of course, LAZIMA atakuwa na baraka za rais directly or indirectly! Lau kama asingekuwa na hizo baraka, hivi sasa ingekuwa ameshatoa agizo la watu wao kuachiwa mara moja!!

Ninachoona haya ni maagizo ya rais moja kwa moja! Na hata kama rais hakuagiza moja kwa moja, kufumbia macho matendo ya kishenzi kama hayainakuwa anatoa ujumbe kwa polisi kwamba waendelee kukamata raia wasio na hatia!

Na hapa kuna tatizo lingine... insecurity!!

Kwa kawaida, baadhi ya wanawake wakipata madaraka huwa wanasumbuliwa sana na hili suala! Katika hili, baadhi yao, tena kwa wingi tu hudhani jambo fulani linafanywa dhidi ya mamlaka yao kwa sababu wanaofanya wanamdharau kwa kumuona yeye ni mwanamke tu!!

Mtu anapokuwa na mawazo mabovu kama hayo, mara nyingi hufanya maamuzi ya ovyo kama defensive mechanism ya kutaka ku-prove "she's tough"!

Sijui ni lini Mwenyezi Mungu atatuondolea Janga la CCM na Watu wake!!!
Usikute rais hata hajui Kama mwenyekiti wenu yuko ndan yy yuko busy na eid
 
Chadema ni kama mtoto wa mwisho yani anadeka deka tuuu kutwa kulia lia tuuuu dah alafu mwanaume ndo wanalia zaidi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mbowe anatangaza kuwa kuna Corona then yeye mwenyewe ndo anataka kukusanya watu
Kwa hiyo corona inabagua?kusanyiko likiwa LA ccm hakuna corona....TUMIA AKILI,ACHA KUTUMIA MAKALIO
 
Ni makosa makubwa kuzuia mifumo rasimi ya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba. Mambo ya Mwendazake amani na kuaminiana kwa Watanzania kulipungua Sana.
 
Vuguvugu hili lipo kwenye mitandao ya simu ambao hao ni makada. Ukija mtaani raia hawana habari na hili mnalolipigania kwenye mitandao na Chama kama Chama.

Unadhani tatizo ni nini?
Binafsi huwa najiuliza Chadema wana lengo gani hasa na Harakati zao hizi za Siasa. Huwa nawaza mambo mawili, Aidha wanafanya siasa zao kwa lengo la kuwaridhisha watu fulani ambao wanawafadhili ili waendelee kuwapa fedha au Hawajui watanzania ni watu wa namna gani inapokuja suala la Siasa.

Unapojiita chama ambacho ni cha kuwasemea watanzania, na unaitisha Maandamano au uko kwenye kuonewa na dola na unaitisha Maandamano lakini watu hao hawajitokezi, lazima ujiulize mara mbili, nini shida? Je, ninachokipigania ndicho wanachokihitaji? Je, njia ninayoitumia ndio wanayoitaka? Je, wako tayari kujitolea kiasi gani? Mimi nina aamini Chadema ni chama kikubwa kioganaizesheni, hivyo kinafanya tathmini na tafiti na kujua nini hasa watu wanataka.

Ukisoma mitandaoni juu ya katiba, unaona mjadala huu unazungumziwa zaidi Twitter, ukichunguza mitandao ya Instagram au Facebook ni nadra kukuta mjadala huu. Je, watanzania wanagapi wanatumia Twitter? Hao wanaotweet kuhusu Katiba ni watu wa kundi lipi? Je, ukifanya reflection huku mtaani Katiba inazungumziwa? Pita kwenye vijiwe, pita sokoni, nenda kwenye mabaa, zungukia kwenye makusanyiko ya harusi au misiba, je kuna mjadala wa katiba? Kama upo inajadiliwa katiba kama hitaji au kama tukio la mvutano wa kisiasa? Ukitathmini yote unaona kuna disconnect kubwa kati ya kinachodaiwa na Chadema na wananchi wenyewe huku mtaani.


Mwaka jana Lissu alizuiwa Kiluvya, jana yake alikuwa na kusunyiko kubwa la watu, lakini hawakujitokeza kupingana na Polisi, Mikutano yote Lissu alikuwa na 'mafuriko' ya watu, lakini alipoitisha Maandamano ya amani Nov 2, 2020 hata wanachama wa chama chake hawakujitokeza. Haya ndio mambo yanaleta maswali juu ya approach ya Chadema kwenye siasa za Tanzania.
Screenshot_20210721-122745.jpg
Screenshot_20210721-122506.jpg
Screenshot_20210721-122342.jpg
Screenshot_20210721-122258.jpg
Screenshot_20210721-120811.jpg
 
Chama Cha Mapinduzi Ni kioga Sana.

CCM wakisikia neno katiba mpya wanakonda Sana kwa mawazo.

Wanajua fika katiba mpya itaweka usawa wa kila kitu.

Na CCM usawa wa kila kitu ndo hawataki kwa sababu siku zote huwa wanaingia madarakani kwa unyang'anyi.
Mfano Ni huu uchaguzi uliopita.

Wakiruhusu katiba mpya maana yake wameruhusu tume yenye usawa,na tume yenye usawa maana yake CCM kwa heri.

Hofu imewatawala hawana namna nyingine Ni kuzuia mikutano ya kudai katiba mpya.

CCM Ni waoga Sana,pamoja na kuwatumia TISS JW PT na wengine kama hawa lakini hawajiamini.

CCM Ni waoga na waongo,wanajinasibu kuwa wanashindaga kwa kishindo maana yake wanapendwa.Sasa kama wanapendwa wanaogopa Nini kuruhusu kelele za hao wanaoitwa wachache ili waendelee kuwashinda na wakose Cha kusema?
Wajisifu kuwa waliomba katiba mpya tumewapa na uchaguzi tumewashinda.wanaogopa Nini sasa?
CCM Ni waoga sana,kwa hofu hii ya kudai katiba mpya,presha zikizidi mnaweza kuwakuta CCM wote wamekufa kwa usiku mmoja tu.
Ni waoga hatari.
Sawa kabisa mkuu.
 
Vuguvugu hili lipo kwenye mitandao ya simu ambao hao ni makada. Ukija mtaani raia hawana habari na hili mnalolipigania kwenye mitandao na Chama kama Chama.

Unadhani tatizo ni nini?
Kama mtaani raia hawana habari, sasa hao police wa nini?
Si wangewaacha CDM wakutane, waongee then warudi makwao.
Maana wanainchi hawana habari.

Sasa Police na Serikali wana hofu gani na kongamano la Katiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vuguvugu hili lipo kwenye mitandao ya simu ambao hao ni makada. Ukija mtaani raia hawana habari na hili mnalolipigania kwenye mitandao na Chama kama Chama.

Unadhani tatizo ni nini?
Hivi kwako tafsiri ya "raia mitaani" ni ipi? Hao wanaoingia kwenye hizo kumbi hawatoki mitaani wanatoka wapi Mkuu?
 
Kama mtaani raia hawana habari, sasa hao police wa nini?
Si wangewaacha CDM wakutane, waongee then warudi makwao.
Maana wanainchi hawana habari.

Sasa Police na Serikali wana hofu gani na kongamano la Katiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali haifanyi kwa kuigopa Chadema ukiliangalia hili suala kwa mapana yake. Serikali inafanya kutokana na kauli ya CHADEMA, nayo Serikali imeamua iwatunishie msuli.
 
Jeshi la Polisi lilimkamata Lowassa wakati fulanl. Lowassa alikamatwa na Polisi au na Makonda?
Inawezekana hapa Mbowe ametekwa alipokywa mikononi mwa Polisi?
 
Back
Top Bottom