Idadi ya watu ndio jambo la kwanza na pili Nguvu ya Uchumi/Mapato
Aisee! Ridiculous!
1.Idadi kubwa Sana ya Watu Siyo kigezo Cha maana Sana kwenye suala hili.
Mji unaweza kuwa na idadi kubwa sana ya Watu lakini mji husika ukakosa kabisa sifa za kuweza kuwa Jiji, badala yake unaendelea kubaki kuwa na hadhi ya kuwa mji au hadhi ya kuwa 'Kijiji', baadhi ya nchi za barani Asia kama vile India, Bangladesh, Sri Lanka zina vijiji na miji mingi sana yenye scenario ya namna hii. Unaweza ukaona Kijiji kina Wakaazi wengi sana ambao wamerundikana kwenye eneo lenye makazi duni kabisa yasiyopangilika, "shacks" au "favelas".
2. Nguvu ya Uchumi/Mapato katika mji au nchi yoyote ile hapa duniani hutegemea zaidi sana kwenye:-
(I) Ubora wa akili walizonazo Watu/Wananchi waliopo kwenye eneo husika. Mfano, mji unaweza kuwa na idadi ya Watu laki tatu wenye akili/elimu kubwa zaidi na unaweza kuwa na Uchumi mkubwa kuuzidi mji au jiji lenye Watu wajinga wapatao Milioni Tisa.
(ii) Shughuli za Uchumi
(iii)Miundombinu msingi ya kujenga na kukuza uchumi, Mfano, viwanda, Makazi Bora na miundombinu mingine yenye kuambatana na Makazi Bora, Upatikanaji wa Nishati, n.k, n.k,
Kwa hiyo, suala hili la Mipango-miji au kupangilika kwa mji ni kigezo MUHIMU zaidi na cha lazima kabisa katika kuainisha mji kuweza kuwa Jiji.