Rais Samia mtumie Profesa Assad akusaidie kwenye Uchumi

Rais Samia mtumie Profesa Assad akusaidie kwenye Uchumi

Babe la mji

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2019
Posts
983
Reaction score
2,058
. Ni mkweli
. Sio mnafiki
. Anasimamia ukweli
. Ni mcha MUNGU
. Hajipendekezi
. Na kubwa Zaidi ni mbobevu na bingwa kwenye mambo ya uchumi.

Kama tunahitaji watu wa kulisaidia Taifa basi tuwatumie watu wa aina hii.

Sina maslahi nae nimetoa ushauri tu na hii ni kutokana na weledi wake.
 
Mh Rais tunakupenda sana.

Wazo hilo litakosha Watanzania wengi.

Prof Assad safiii.

Kipengele cha katiba asiteuliwe kirekebishwe,hawa ndio wazalendo

Mama tupo chini yako
 
Ila Ndugai/Acksonishisit watupishe kwanza.ASAD apige mzigo
 
Huyo Assad anaonekana kafisa mfia dini huyo ataharibi nchi yetu nzuri. Yule labda awe Katibu wa Bakwata
 
Rais Samia anaweza kumteua Dk Semboja kwenye eneo hilo badala ya prof Assad ambaye kikatiba haruhusiwi
 
Msichanganye uchumi na accounts/finance..maswala ya uchumi si moja wapo na areas of expertise ya prof Assad.

Wapo wataalam wa uchumi na yeye si mmoja wapo japo anaweza kuwa na ka idea.
 
Katiba hairuhusu ateuliwe tena.

Sent from my Redmi Note 7 Pro using JamiiForums mobile app
Kwani katiba iliruhusu bwana yule aongezewe muda wa kutawala? Si alikuwa akifanyiwa janjajanja aongezewe?
basi na kwa Assad ifanyike hivyo.

Mtoa mada yupo sahihi, mama SSH anaweza amuweke prf Assad awe mshauri wake wa uchumi ikulu.. na sio kuacha madini yake yapotee
 
Hamna mtu hapo zaidi ya kiburi na unafiki.
kwa sababu aligundua madudu ya yule bwana na kuyaweka hadharani?

inaonyesh kuna kikundi ndani state kunachojiona kina haki ya kipekee kula keki ya taifa, hivyo yeyote anaye kosoa uozo anakuwa sio mzalendo?

hana kiburi, anasimamia sheria na ni mzalendo wa kweli
 
Mama alishaweka wazi, atafanya kazi na mtu yoyote hata kama ni mpinzani ikiwa tu amethibitisha kuwa mtu huyo anaweza. Kama mama atamuhitaji atamuita na kumpa majukumu yake.

Ila tutambue Tanzania hii tuna akina Professor Assad wengi sana, tuwaache na wengine waonyeshe vipaji vyao kulitumikia Taifa lao pendwa la Tanzania.
 
Back
Top Bottom