Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Rais Samia sikupangii ila inapaswa kumuwajibisha Msemaji mkuu wa serikali na Felchesim Mramba ambae sasa ni kamishna wa umeme na nishati Tanesco.
Kwanini uwawajibishe
Tarehe 10 mwezi huu wa 11, wiki moja iliyopita kulikuwa na mkutano wa waandishi wa habari na mawaziri na watendaji mbalimbali wa serikali wakielezea miaka 60 ya uhuru.
Hawa watu walisema sasa hivi tunazalisha umeme megawati 1607, huku mahitaji yakiwa megawati 1237. Hivyo tuna ziada ya umeme karibu ya megawati 400.
Siku jana Tanesco wametoa taarifa kuwa tuna upungufu wa uzalishaji kwenye umeme. Ina maana haya mapungufu yametokea ndani ya wiki 1 tu?
Sina chuki wala wivu kwa Gerson Msigwa wala Mramba, ila anza na hao ili kuonyesha uwajibikaji wao.
Mama Samia ukweli hatuwezi kwenda kwa style hii ya watendaji wakubwa wa serikali kwa kuongopea umma.
Na Kama wao wanasema ukweli kuwa tunazalisha sana umeme kuliko mahitaji basi unapaswa kumuwajibisha mkurugenzi wa Tanesco kwa kuongopa kuwa Kuna upungufu wa uzalishaji.
Ukiiacha hali hii kuendelea basi kuna hatari zaidi inakuja.