benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius Ndejembi,
amesema serikali imedhamiria kujenga shule za sekondari katika kata zote nchini awamu ya pili.
Alisema shule hizo zitajengwa katika halmashauri zote 184 nchini na kila halmashauri itapata shule moja.
Ndejembi alisema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Maimuna Mtanda (Viti Maalumu).
aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga shule za sekondari katika kata ambazo wanafunzi wake wanatembea umbali
mrefu, akitolea mfano Chilangala na Mukomatu zilizopo Jimbo la Newala Mjini.
Aidha, katika swali la pili, alitaka kujua mkakati wa serikali wa kupeleka walimu katika shule hizo. Akijibu maswali hayo, Ndejembi alisema dhamira ya serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu ni kujenga shule katika kata zote nchini.
"Niwatoe shaka waheshimiwa wabunge kwamba, serikali imedhamiria kwenda katika awamu ya pili ya kujenga shule hizi katika kata, muda siyo mrefu, mtaanza kuona zikijengwa katika halmashauri zote 184 katika nchi yetu, kila halmashauri itapata walau shule moja katika awamu ya pili,"alisema.
Ndejembi akijibu swali la pili la mbunge huyo, alisema serikali imetangaza ajira 21, 200 kuajiri walimu na watumishi wa sekta ya afya. Alisema ajira hizo zitaziba mapengo ya walimu ambao wanahitajika katikamaeneo hayo.
Akijibu swali la msingi la Anastazia Wambura (Viti Maalumu), aliyetaka kujua shule ngapi za sekondari zimejengewa katika Mkoa wa Mtwara ambao una zaidi ya kata 50 ambazo hazina shule.
Ndejembi akijibu swali hilo, alisema mradi serikali kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari, imejenga shule 231 za kata na shule 10 za wasichana za kitaifa katika mikoa 10. Kwa mujibu wa Ndejembi, hiyo ni awamu ya kwanza ya ujenzi kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari ambapo tayari Mkoa wa Mtwara umeshajengewa shule 10 za kata katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa wanafunzi