Rais Samia na CCM mnaharibu Soka nchini

Rais Samia na CCM mnaharibu Soka nchini

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Screenshot_20241120_084428_Gallery.jpg

Rais, chawa wako na CCM hamuoni kama mnazidi kuididimiza soka mwishowe na yenyewe iwe kama ilivyokuwa ngumi kipindi kile?

IMG_20241120_084036_975.jpg

TUmefikia hatu tunaombea tufungwe ili tu kuwakomoa CCM, lakini ukweli ni kwamba mnawaumiza hawa vijana na wengine wengi nyuma yao wanaotegemea soka kama sehemu yao kuu ya kujiingizia kipato na kuendesha maisha yao.

Screenshot_20241120_084205_Gallery.jpg

Watu wamepambana kufunga eti, "Tunamshukuru Rais Samia kwa kufuzu AFCON"🤨🤦‍♂️🤦‍♂️ kwani ye ndio aliingia kusakata kabumbu? Mwana FA toka nawe umezidi kuwa mpuuzi, a dissapointment kwa vijana na wanamichezo waliokuwa wanategemea mengi kutoka kwako.

Pia soma: Rais Samia aipa Taifa Stars Milioni 700 kufuzu AFCON

Kufunga kazi unatoa rushwa wazi wazi na hao wapuuzi wengine TAKUKURU wapo tu! Sio tu siasa zinazidi kuwa za kupuuzi lakini tunaharibu sekta nyingine kwa kufumbia macho haya mambo, mwisho wa siku kutakuwa hakuna mchezo wa maana ambao unaweza kuwainua vijana kiuchumi wala kutuwakilisha vema kimataifa.

TFF wameufyata, hao FIFA waje watunyooshe tuu labda itasaidia kutuamsha!

Pia soma: Siasa kuingia kwenye michezo na wanamichezo kutumika kisiasa hatujali kuibomoa sekta hii?
 
Hapa hauna hoja mbona rais anajitahidi sana upande wa michezo mkuu
 
Katoa milioni 700, nchi ina kero kibao.. Kariakoo siku 5 bado wanaokoa watu, jengo la ghorofa 4 tu.. Vifaa changamoto

Jana tu mtu kalalamika muhimbili kitanda kwa siku ni 50 elfu.
 
CCM inafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha inatufarakanisha.
 
Back
Top Bottom