#COVID19 Rais Samia na Serikali, chanjo ya Johnson & Johnson inahitaji mtu apate tena booster

#COVID19 Rais Samia na Serikali, chanjo ya Johnson & Johnson inahitaji mtu apate tena booster

Usishangae taarifa hii kufutwa soon, serikali haiko rafiki na genuine challenges. Inapenda habari ya kuisifia hata kwa mabovu.
Ila hata wakifuta naamini wapo wenye akili huwa wanatafuta habari na watazipata tu.
Hii chanjo ya Johnson and Johnson hata US wamechanja watu wachache sana, 2.4% ya wamarekani
Wamarekani wengi wanachanja Pfizer na Moderna
 
Kuhusu chanjo ya Johnson and Johnson, Leo nimesikiliza vizuri Serikali ikizungumzia hili suala na Mh. Raisi amezungumza kuwa unapata chanjo moja tu.

Hapa kuna jambo halipo sawa, kwa taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari ambavyo ni credible Kama New York Times, Reuters, daily mail vinasema chanjo moja ya Johnson and Johnson haiwezi kupambana na virusi vipya vya corona hivyo inahitaji watu wapate booster.

Hizi ni taarifa muhimu ambazo zimeripotiwa na vyombo vikubww vya habari, wamesema wazi kuwa hii chanjo ya J and J ipo less effective kwenye hivi virusi vipya.

Hvyo kwa unyenyekevu nikiwa Kama mtanzania ambae napenda kukosoa kwa staha naomba serikali iangalie hili kwa kuwa isije baadae mkawaambia tena watu kuwa wanahitaji hizo booster ikiwa sasa mmeshawaambia chanjo moja inatosha.
Chini nimeweka taarifa hizo kutoka kwenye hivyo vyombo vya habari

N.B
Naiomba pia Serikali iache watu wahoji wasiwasi wao kwa kuwa hili suala la wasiwasi wa chanjo lipo dunia nzima.

Hata huko US (Marekani) wanapotengeneza hizo chanjo Kuna watu wengi tu wamezikataa.

Report zinasema 20% ya wamarekani wamekataa hizi chanjo.

20% ya wamarekani ni sawa na watu milioni 65, hivyo Kuna watu millioni 65 Marekani wamekataa chanjo. Taarifa ipo chini
Hivyo suala la kukataa chanjo halipo tu Tanzania bali hadi huko.

Pia ni kweli kuwa wapo waliopata chanjo na bado wakapata corona na wakafa pia lakini si number kubwa(rare cases).

Hivyo kwa unyenyekevu niombe serikali iache watu wenye wasiwasi wawe huru, Ila wakipata elimu kwa ridhaa yao wataenda kupata chanjo.

UWEZI KUWA NA CHANJO YA KWELI KWA KIRUSI CHENYEKUBADILIKA KWA HARAKA KAMA COVID watachomana chanjo mpaka akili ziwakae awa
 
Arusha jana na leo kuna wahindi wengi wamechanja ASTRAZENECA...
Wamekichanga kwenye jumuia zao wameagizia mzigo
 
Soma vizuri Reuters na daily mail wameeleza vizuri tu.
Ndio maana unaona mwisho wakasema experts already taking
Siyo mara ya kwanza kusoma haya. Hakuna hata makala moja inayo speculate udhaifu wa Janssen ambayo ni peer reviewed. Na mamlaka za kitaalamu zote hazijakubaliana na hiyo speculation. By the way ukisoma bila upendeleo utakuta kuwa hata moderna na pfizer zinasemwa na wengine kuwa hafifu dhidi ya Delta. Ni uoga mzuri wa wanasayansi fulani, lakini haujathibitika.
 
Ndo Ujue hawajui wanaloliongea ,wanasoma script,Pfizer na Moderna na wenyewe wataongeza booster ya tatu hivi karibuni,,,,Viongozi wetu wapo out of phase sanaaa
Kwani hizo booster zikijakuhitajika baadae tatizo liko wapi hapo? Hata chanjo za watoto mbona zinakuwaga na booster?
 
Ila hata wakifuta naamini wapo wenye akili huwa wanatafuta habari na watazipata tu.
Hii chanjo ya Johnson and Johnson hata US wamechanja watu wachache sana, 2.4% ya wamarekani
Wamarekani wengi wanachanja Pfizer na Moderna
Mlisema marekani ilipigwa marufuku haitumiki. Saivi mmebadilisha gia mnasema wanaochoma ni wachache sana lakini bado watu wanachoma. Hamkosi visababu

Mnachoshindwa kuelewa ni kuwa j and j imeanza kutumika baadae sana ukilinganisha na Pfizer na moderna

Yote kwa yote chanjo ni hiari sasa sioni shida inatokea wapi
 
Kwani hizo booster zikijakuhitajika baadae tatizo liko wapi hapo? Hata chanjo za watoto mbona zinakuwaga na booster?
Mkuu Mimi Sina shida na hiz booster Ila nilichofanya ni kukumbusha tu kuwa chanjo moja haitoshi, so nakosoa walivyosema chanjo moja inatosha
 
Maigizo ya kuchanja yataanza upya na sie wakuzoom tutazoom tu tujue ukweli.
 
Back
Top Bottom