Rais Samia na Serikali yake wamefanya lipi jema mpaka sasa?

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Tuambiwe hadi leo chini ya Utawala wa CCM kwa kipindi hiki kipya cha Rais huyu mtarajiwa kwa njia ya kupigiwa kura hapo 2025, lipi alilolifanya hata Wananchi wamchague 2025 awe Rais wao?

Kwa upande wangu naona mambo ni valuvalu tu hayana muelekeo wa kuonyesha ameleta unafuu wa maisha kwa mwananchi. Kama yapo tuambiwe hili na lile, miamala tozo, umeme gesi na vingi kwa mlaji vimeshuka bei na sasa Mwananchi wa Tanzania anapata milo mitatu kwa siku na wale wanaokula daku hawakwangui masufuria ili kura zetu tumpe.

Zaidi naona ni mtafaruku ndani ya chama chao na pia kujiwekeza kwa kupambana na wanaodai Katiba na wapinga chanjo bila ya kuviacha vyama vya siasa.

Rais ili ajikwamue aurudishe na kuumalizia ule mchakato wa Katiba Mpya kwa pale ulipobakia tutamuelewa.
 
MAMA NA CCM BADO ASEE KAMA HATA KULIPA WASTAAFU MAFAO YAO MPK LEO BADO TU..BA HII CORONA IKIKUNASA JAU HUCHUKUI HATA ROUND
 
Mengi tuu hasa upande wa watumishi wa umma,watu wa biashara nk..kwa upande wa wanaojiita wanyonge Mazao yao yanauzika ila bei ndio sio rafiki na vitu vingi vimeenda juu.

Ukipata mwingine wa kumchagua hiyo 2025 mchague tuu usiwaze mkuu ila sisi tunaenda na SSH.

Kwa mfano sisi tulio kwenye Ukandarasi tunaelewa nini tunaongea yaani tunapata Kazi kama zote.

Kingine ulichomiss wewe na propaganda na majigambo ya uzinduzi,matamko ya udharirishaji nk ndio maana unaona kama kimya.
 
Kosa kubwa wanalolifanya CCM ni kufikiri kuwa uwepo wa vyama dhaifu ya upinzani hapa nchini ama kuviminya fursa ya kujiimarisha ndicho kitu pekee kinawafanya waonekane kuwa wao ni imara. Hawatambui umuhimu na mchango mawazo mbadala kama mojawapo ya njia na fikra pevu za kuweza kuindesha nchi kwa umakini mkubwa.

Hawaoni pamoja na kujitwalia kwa hila nafasi karibu zote zilizotokana na chaguzi za 2019 na ule wa 2020, lakini bado wanazidi kuhangaishwa na "trivial things". Badala ya kujikita katika mambo makubwa yaliyo na tija katika nyanja za kiuchumi ili kuchochea maendeleo, wao wanafikiria sifa pekee ni kubakia madarakani kwa gharama yoyote ile.

Ndiyo maana kitu pekee imebaki kwao ni kutegemea vyombo vya dola ili kuendelea kubakia madarakani. Kamwe haiwezekani akili ndogo ikaendesha akili kubwa na kutarajia matokeo makubwa.
 
Amefanya vizuri kwenye mambo madogo ila makubwa anakosea, hajali haki za binadamu, na anawanyima wengine uhuru wao wa kutoa maoni.
 
Hamna kitu. katiba irekebishwe ikitokea Rais alieko madarakani anafikwa na la kufikwa uitishwe uchaguzi maana inaonekana kwa katiba ya sasa Rais alieko madarakani anateua makamu wa Rais goigoi kwa sababu wanazojua wao.
 
Tuambiwe hadi leo chini ya Utawala wa CCM kwa kipindi hiki kipya cha Rais huyu mtarajiwa kwa njia ya kupigiwa kura hapo 2025, lipi alilolifanya hata Wananchi wamchague 2025 awe raisi wao?

Kwa upande wangu naona mambo ni valuvalu tu hayana muelekeo wa kuonyesha ameleta unafuu wa maisha kwa mwananchi. Kama yapo tuambiwe hili na lile, miamala tozo, umeme gesi na vingi kwa mlaji vimeshuka bei na sasa Mwananchi wa Tanzania anapata milo mitatu kwa siku na wale wanaokula daku hawakwangui masufuria ili kura zetu tumpe.

Zaidi naona ni mtafaruku ndani ya chama chao na pia kujiwekeza kwa kupambana na wanaodai Katiba na wapinga chanjo bila ya kuviacha vyama vya siasa.

Rais ili ajikwamue aurudishe na kuumalizia ule mchakato wa Katiba Mpya kwa pale ulipobakia tutamuelewa.
mm nasema toka 1961 mpaka leo ni lipi ccm la kheiri walilofanya ?
 
Kubwa kuliko yote ni uhuru wa watu kutoa maoni yao bila hofu ya kupotezwa au kukamatwa na kufunguliwa kesi za utakatishaji pesa na uhujumu uchumi. Hata hiki kitendo cha kumjadili mama SSH na serikali yake ya awamu ya sita bila hofu ni kitendo cha maendeleo makubwa

Ingekua ni kipindi cha mwendazake nyuzi kama hizi zingekua zinafutwa tu na mods kwa uoga na hofu tuliojengewa wabongo
 
Tuambiwe hadi leo chini ya Utawala wa CCM kwa kipindi hiki kipya cha Rais huyu mtarajiwa kwa njia ya kupigiwa kura hapo 2025, lipi alilolifanya hata Wananchi wamchague 2025 awe raisi wao?

Kwa upande wangu naona mambo ni valuvalu tu hayana muelekeo wa kuonyesha ameleta unafuu wa maisha kwa mwananchi. Kama yapo tuambiwe hili na lile, miamala tozo, umeme gesi na vingi kwa mlaji vimeshuka bei na sasa Mwananchi wa Tanzania anapata milo mitatu kwa siku na wale wanaokula daku hawakwangui masufuria ili kura zetu tumpe.

Zaidi naona ni mtafaruku ndani ya chama chao na pia kujiwekeza kwa kupambana na wanaodai Katiba na wapinga chanjo bila ya kuviacha vyama vya siasa.

Rais ili ajikwamue aurudishe na kuumalizia ule mchakato wa Katiba Mpya kwa pale ulipobakia tutamuelewa.
Ameongeza bajeti ya Tarura kutoka bil 200 mpaka billioni 900(ref Umi mwalimu), bajeti ya maji kaongeza maradufu mpaka b680 ili kumaliza kero za maji(ref waziri wa maji),bajeti afya , diplomasia-wawekezaji,fedha za wahisani zimeachiwa, wanaongezeka,pia kurudisha sekta binafsi.Pia anaprogram kubwa ya ku-rebrand Tanzania ambapo atavutia wawekezaji wengi sana.hayo ni machache dhidi ya mengi.
 
Suala la mtafaruku ndani ya chama tangu enzi za Jiwe, tena enzi za Jiwe mtafaruku ulikuwa mkubwa.
Jiwe angewapoteza endapo wangeunua shingo zao kama nungunungu.
Samia kalete tozo ambayo inachukua fedha mtaani gradually na kuzipeleka serikalini kimyakimya.
Mwisho wa picha mtaani kutakuwa hamna pesa.
Binafsi kaniongezea mshahara. Yule ibilisi alininyima mshahara mpya kwa miaka 6.
 
Tuambiwe hadi leo chini ya Utawala wa CCM kwa kipindi hiki kipya cha Rais huyu mtarajiwa kwa njia ya kupigiwa kura hapo 2025, lipi alilolifanya hata Wananchi wamchague 2025 awe raisi wao?

Kwa upande wangu naona mambo ni valuvalu tu hayana muelekeo wa kuonyesha ameleta unafuu wa maisha kwa mwananchi. Kama yapo tuambiwe hili na lile, miamala tozo, umeme gesi na vingi kwa mlaji vimeshuka bei na sasa Mwananchi wa Tanzania anapata milo mitatu kwa siku na wale wanaokula daku hawakwangui masufuria ili kura zetu tumpe.

Zaidi naona ni mtafaruku ndani ya chama chao na pia kujiwekeza kwa kupambana na wanaodai Katiba na wapinga chanjo bila ya kuviacha vyama vya siasa.

Rais ili ajikwamue aurudishe na kuumalizia ule mchakato wa Katiba Mpya kwa pale ulipobakia tutamuelewa.

2877438_photo_2021-08-11_09-06-26.jpg
 
Labda kumkamata Sabaya.
 
Back
Top Bottom