Rais Samia na Serikali yake wamefanya lipi jema mpaka sasa?

Rais Samia na Serikali yake wamefanya lipi jema mpaka sasa?

Tuambiwe hadi leo chini ya Utawala wa CCM kwa kipindi hiki kipya cha Rais huyu mtarajiwa kwa njia ya kupigiwa kura hapo 2025, lipi alilolifanya hata Wananchi wamchague 2025 awe Rais wao?

Kwa upande wangu naona mambo ni valuvalu tu hayana muelekeo wa kuonyesha ameleta unafuu wa maisha kwa mwananchi. Kama yapo tuambiwe hili na lile, miamala tozo, umeme gesi na vingi kwa mlaji vimeshuka bei na sasa Mwananchi wa Tanzania anapata milo mitatu kwa siku na wale wanaokula daku hawakwangui masufuria ili kura zetu tumpe.

Zaidi naona ni mtafaruku ndani ya chama chao na pia kujiwekeza kwa kupambana na wanaodai Katiba na wapinga chanjo bila ya kuviacha vyama vya siasa.

Rais ili ajikwamue aurudishe na kuumalizia ule mchakato wa Katiba Mpya kwa pale ulipobakia tutamuelewa.

Kuachana na propaganda za nyungu na kupunguza ubabe wa mamlaka zikiwamo TRA, Polisi na TAKUKURU. Japo kuna ka kupumua kidogo - bado haitoshi.

Ukiukaji wa haki za watu uko pale pale na huu utaendelea kumgharimu.
 
Hyo shida ni ya nan? mfano anakuja gavana wa bot na ushauri wa kiuchumi, unataka rais alete ujuaji wakati kuna wasomi na wabonezi kwenye fani husika. sema watz uwajibikaji zero, mnataka rais awe mjuaji Kama bwana yule mchumi,mwanasheria,mkandarasi,askari ni yeye tu ndyo mjue mna rais
Watalaam wapo, sheria + kanuni + taratibu pia zipo, kwa nini mambo hayaendi? Mamlaka na madaraka ya kuhakikisha mambo yanaenda amekasimiwa Rais, Kikatiba.

Ibara ya 34, Katiba ya JMT, (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
 
Kubwa kuliko yote ni uhuru wa watu kutoa maoni yao bila hofu ya kupotezwa au kukamatwa na kufunguliwa kesi za utakatishaji pesa na uhujumu uchumi. Hata hiki kitendo cha kumjadili mama SSH na serikali yake ya awamu ya sita bila hofu ni kitendo cha maendeleo makubwa

Ingekua ni kipindi cha mwendazake nyuzi kama hizi zingekua zinafutwa tu na mods kwa uoga na hofu tuliojengewa wabongo
Hilo nalo neno,naona washaanza kujisahau kama mwendazake alikua kichaa kwa maoni huru ,ulikuwa kujamba huwezi lazima uangalie kila upande kama huonekani daa dekiii.
 
Tuambiwe hadi leo chini ya Utawala wa CCM kwa kipindi hiki kipya cha Rais huyu mtarajiwa kwa njia ya kupigiwa kura hapo 2025, lipi alilolifanya hata Wananchi wamchague 2025 awe Rais wao?

Kwa upande wangu naona mambo ni valuvalu tu hayana muelekeo wa kuonyesha ameleta unafuu wa maisha kwa mwananchi. Kama yapo tuambiwe hili na lile, miamala tozo, umeme gesi na vingi kwa mlaji vimeshuka bei na sasa Mwananchi wa Tanzania anapata milo mitatu kwa siku na wale wanaokula daku hawakwangui masufuria ili kura zetu tumpe.

Zaidi naona ni mtafaruku ndani ya chama chao na pia kujiwekeza kwa kupambana na wanaodai Katiba na wapinga chanjo bila ya kuviacha vyama vya siasa.

Rais ili ajikwamue aurudishe na kuumalizia ule mchakato wa Katiba Mpya kwa pale ulipobakia tutamuelewa.
Watumishi wa umma wamepandisha vyeo
 
Wewe Muongo wa Kutupwa.
Kubwa kuliko yote ni uhuru wa watu kutoa maoni yao bila hofu ya kupotezwa au kukamatwa na kufunguliwa kesi za utakatishaji pesa na uhujumu uchumi. Hata hiki kitendo cha kumjadili mama SSH na serikali yake ya awamu ya sita bila hofu ni kitendo cha maendeleo makubwa

Ingekua ni kipindi cha mwendazake nyuzi kama hizi zingekua zinafutwa tu na mods kwa uoga na hofu tuliojengewa wabo
 
Eti kesi zilifutwa. Yaani Kesi za misadu kufutwa ndio unaona maendeleo? Na safi sana huyohuyo aliemuona mzuri leo yuko wapi? Hujiulizi. Hakutakiwa kuanza kwa haraka angejifunza kwanza! Akatuelewa Watanzania Bara!
 
Tena mumkome kabisa kama mlivyokoma kunyonya ziwa la mamayenu! May e Rest In Peace. Amen. !
 
Tozo za miamala zimeainishwa kuwekwa kwenye mfuko maalumu utakaokwenda kuchangia maendeleo moja kwa moja bila hatua zozote zinazoonekana kuweka uwazi kwenye mfuko wenyewe.

Kodi mpya ya SIM card kwenye mazingira ambayo sekta ya mawasiliano na teknolojia imewezesha ufanisi mkubwa kwenye maeneo mbali mbali, imekuwa chanzo kikubwa cha ajira za moja kwa moja na indirect, imekuwa ikikua mwaka hadi mwaka na faida nyingine.

Ongezeko la kodi kwenye mafuta, juu ya Ongezeko la bei kwenye soko la dunia, eneo ambalo kihistoria bei zikipanda zinapelekea bei kupanda kwenye maeneo maeneo mengine yanayogusa mwananchi moja Kwa moja.

Na sasa ukusanyaji kwa Kodi ya majengo ambao kwanza, kwa viwango vilivyoweka una discourage ujenzi wa maghorofa mijini, na pili, kwa kukusanya kupitia mita za luku pamoja na kurahisisha ukusanywaji, unaleta uwezekano wa kodi hii kulipwa na wasiohusika kinyume na taratibu za Kodi za majengo. Kwa mpangaji anayelipa pango mwanzo wa mwaka, kiuhalisia ana mwanya gani wa kurudisha anacholipa kwenye kodi ya jengo kupitia manunuzi yake ya umeme Kwa miezi ya mbele kutoka Kwa mwenye jengo?

Pamoja na yote, jambo moja ambalo halijabadilika ni matumizi ya style ya uchaguzi utakaoenda rudiwa Konde.
 
Back
Top Bottom