Rais Samia na Watanzania naomba mpitie hapa ili Tanzania ipae kiuchumi

Kufutwa itakuwa kazi nzito maana ndio sehemu yao ya kujipatia ulaji ila kama watavifanya viwe vyanzo vyao vya kujipatia mitaji na kuachia madaraka let's say baada ya miaka 2 itapendeza.
 
".......ILI tuendelee tunahitaji; Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora.........." Julius Kambarage Nyerere.
Lakini bila ya kuwa na KATIBA bora sio rahisi kuwa na SIASA SAFI.
Tatizo kubwa tulilonalo kwa muda mrefu sasa ni UWEPO wa katiba bora inayoweza kuhakikisha utu, upendo na haki vinakuwepo na kuheshimiwa ndani ya taifa letu. Tutaepukana na viongozi wanaoona ufahari kufanya lolote, kukandamiza na hata kuua kwavile hawabanwi kisawasawa na katiba na sheria zilizopo.
TUSIJIDANGANYE, hatuwezi kuwa na maendeleo endelevu yenye uimara na kuinua hali za wananchi mahali pasipo na katiba bora.
 
You nailed it bro.
 
Katiba mpya Haiwezi kutuletea maendeleo, Hicho ni kichaka cha wavivu na wasio na Vision....Kazi, mipango ya MDA mrefu, kupiga Vita rushwa...Tanzania kwanza chama Baadae....Hivi ndo Vitaleta maendeleo...Otherwise ni Porojo Tu.
 
Katiba mpya Haiwezi kutuletea maendeleo, Hicho ni kichaka cha wavivu na wasio na Vision....Kazi, mipango ya MDA mrefu, kupiga Vita rushwa...Tanzania kwanza chama Baadae....Hivi ndo Vitaleta maendeleo...Otherwise ni Porojo Tu.
Soma post no 42. Jamaa ostrichegg kaelezea vizuri kwa maneno machache.
 
Mkuu
Umenena vyema, kama unavyoona watu wengi wanakubali kuwa bila katiba bora hakuna kitu hapo. Katiba bora itajenga taasisi imara, ni jambo la kushangaza mtu kusema kuwa katiba si jambo la maana kwa sasa kwa nchi kama Tanzania.

Katiba hii ikiachwa tu bila kubadilishwa hata haya mawazo yako mazuri uliyotoa humu utasikia mtu mmoja anayapinga kwa kiburi na kujitapa kuwa yeye hashauriwi na hapangiwi.

Kama kuna kitu kitamwongezea mama sifa basi kimojawapo ni kuruhusu kumalizika kwa mchakato wa katiba mpya. Akitulia serikalini alifanyie hili kazi. Nina imani naye ya kwamba atalifanya hili wekeni kumbukumbu hii.

Tuongee tu ukweli, vyeo hivi vya RC, RAS, DC, DAS nk. Vinafurahiwa kwa sababu CCM wapo madarakani, ila ingetokea chama kingine kikashika hatamu, wao (CCM) wangekuwa wa kwanza kuzipinga nafasi hizi. Rai yangu walizungumze kichama ili waliondoe wao wenyewe.

Kuhusu elimu yetu, bado sana. Nimesikia kuna mpango wa kuisuka upya acha niishie hapa kwa sasa.

Mwisho, mkuu kama unaweza weka mawazo yako katika kitabu, tena kwa lugha yetu ya kiswazi. Tumia lugha nyepesi, mawazo yako yataishi milele. Ipo siku hata kama si leo mtu mmoja atayafanyia kazi.

Asante
 
Shukrani mkuu kwa mchango wako. Kuna post ya namba 42 kutoka kwa ostrichegg imeongelea kiufasaha umuhimu wa katiba mpya japo ametumia maneno machache.
 
unazunguka mbuyu dawa ni katiba mpya bila katibba mpya hakuna uchumi maana ccm ni walewale mchwa.
Katiba ni moja ya nyezo ya kufikia hayo ila sio dawa ya kila kitu (Katiba,Viongozi bora na Wananchi wenye uzalendo) huu ndio mwarobaini wa matatizo yetu tofauti na hivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu
 
Mzee hapa..umerocha..inamaana hujui why hio sheria imewekwa..bila hiyo si wakora watakuwa wanawatia wanafunzi mimba kila mwaka..sasa..inamaana tutakuwa na Taifa linalosomesha wajawazito..lakn pia unachotaka kinakinzana na ulichosema kutilia mkazo kwenye elimu..huwezi kutoa elimu ..hapo hapo uruhusu wanafuzni wanyanduane ...

Kuongezea tu..hapo..inafaa as Taifa kwa Kila Raia tubadili mitazamo yetu ijielekeze kwenye mikakati..huwezi Serikali unafanya jitihada ..mwananchi anacheza baikoko na singeli...ama.wananyandua na kuendelea starehe....
 
KILA raisi uja na yake kwa kuponda ya mtangulizi wake hayo maendeleo tuyapate wapi
 
Hapana mkuu bado nipo sahihi kwa hili. Swala la kufanya mapenzi halitakiwi kuadhibiwa kwa adhabu kali kama hii. Okay hebu jaribu kuliangalia kwa hii angle: mkipeana mimba nani anaathirika? Jaribu kutafakari nje ya box. Halafu mbona nchi zilizoendelea hazina sheria kali kama hii? Kufanya mapenzi hakurudishi maendeleo nyuma na pia hakuna mtoto wa kike anayefurahia kupata ujauzito kabla hajawa tayari kuwa na familia, ujauzito ni adhabu tosha kwa wahusika. Nchi zote zilizoendelea hazina sheria kama hii. Hii ni sheria ya kikandamizaji na imepitwa na wakati katika huu ulimwengu wa watu wastaarabu.
 
Hayo yote si lazima yaainishwe kwenye katiba boss, hakuna utashi wa kisiasa bila kuwa na katiba ambayo inaelekeza namna ya utashi unavyotakiwa
 
Unajua maana ya katiba au unaongea tu.Au kwavile kuna viongozi wanadharau katiba nawewe unaona katiba sio jambo la msingi.Kajielimishe upya.
 
Unaipondea katiba alafu wakati huo huo unataja nafasi ambazo kimsingi ziko kikatiba.Hao ma Rc wako kwenye katiba na hizo kazi unazoziona azina maana ndiyo majukumu yao kikatiba.Hiyo katiba ya kenya sio lazima uone manufaa yake leo ndo maana ata hii yakwetu wakati inaanza kutumika ilionekana haina mapungufu ila kwa kadri zama zinavyobadilika ndivyo ambavyo inaonekana ina mapungufu kama haya uliyoyaona ya wakuu wa mikoa.Hizo nchi zote ulizozitaja zimepiga hatua kwasababu ya miongozo bora waliyojiwekea na msingi wa muongozo kwa nchi ni katiba.Utashi wa kisiasa wa kiongozi yoyote ule lazima uwe ndani ya taratibu na kanuni zitakazompa dira ya nini chakufanya,kwasababu ata kama atakua mwema vip kuna mambo ambayo yatamfanya akwame kwa baadhi ya mambo na kamwe hauwezi kuongoza nchi kwa mawazo yako toka kichwani.ndo maana wenye akili waliweka katiba ili iwe ndio muongozo wa jinsi tunavyotaka tuenende.Ukiwa na katiba nzuri iliyogusa mahitaji yote ya jamii ni rahisi kufanya maendeleo kwasababu kutakua na kanuni,sheria na taratibu zitakazokua zinaelekeza nini chakufanya kwenye kila eneo tofauti na hapo tutakua tunalalamika kila leo kwanini hili kwanini hili bila kujua kua miongozo tuliyonayo inahitaji mabadiliko makubwa.
 
Katiba mpya Haiwezi kutuletea maendeleo, Hicho ni kichaka cha wavivu na wasio na Vision....Kazi, mipango ya MDA mrefu, kupiga Vita rushwa...Tanzania kwanza chama Baadae....Hivi ndo Vitaleta maendeleo...Otherwise ni Porojo Tu.
Hakuna maendeleo utakayoyapata bila muongozo kwasababu binadamu ili aende lazima awekewe kanuni na sheria.Sasa kama huna katiba bora hizo sera za uchumi,sheria za kodi na uwekezaji utazilinda vip kama hakuna sheria mama inayoziguide hizo sheria ndogo ndogo zakutekeleza hayo.
 
Unajua watu wanaongea halafu hata wanachokiongea hawakijui. Mtu analalamikia uwepo wa maRC hapo hapo anasema katiba mpya sio muhimu wakati hao maRC wapo kwa mujibu wa katiba.
 
Una hoja nzuri sana mkuu. Hebu pendekeza mbinu tutakayotumia ili katiba ya Warioba ipitishwe.
Tuache kudai katiba mpya bali tuwadi tuliowapa jukumu la kuirasimisha Rasimu ya Katiba Mpya tuliyoiandaa chini ya uenyekiti wa Mh. Jaji Warioba. La hawaitaki watuambie sababu za msingi za kuyakataa matakwa wa wenye nchi. Tukiridhika na sababu zao tutakubaliana nao, vinginevyo tutakuwa tumeshindwana na hivyo itabidi watuachie wenyewe tuteuwe au tuwape wengine watakaokubaliana nasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…