Rais Samia na Watanzania naomba mpitie hapa ili Tanzania ipae kiuchumi

Unadhani nini kifanyike turudi tena huko? Unadhani nini kifanyike Tanzania tufike level za mataifa ya ulaya ya magharibi?
Ile nguvu iliyotumika kuzalisha zao la mkonge itumike kuzalisha mazao ya chakula yatakayo uzika Afrika na duniani. Tuwatumie wataalamu wetu wa kilimo kuwafikia wananchi na kuwapa mwongozo wa kilimo bora.

Kuwe na biwanda vya packaging ambavyo vitaweka ubora wa mazao katika madaraja. Hivi vitazalisha ajira nyingi hasa kwenye distribution.

Wataalamu wa masoko washirikiane na mabalozi wetu kutafuta masoko nje ya nchi.

Wanaosababishia kampuni hasara wafukuzwe. Ingependeza kama kampuni za kilimo au packaging zingemilikiwa na vyama vya siasa au watu binafsi.
 
TUSIJIDANGANYE, hatuwezi kuwa na maendeleo endelevu yenye uimara na kuinua hali za wananchi mahali pasipo na katiba bora.
Kwa tafsiri pana, mstari wako huu unasema kweli.

Maana hata uwe na kila aina ya mavitu, mabarabara, mareli, madege na takataka zote, lakini kama huna HAKI/UHURU, ukweli ni kuwa huna maendeleo.
Lakini labda nitoe mfano mwingine: Hakuna katiba mpya nzuri inayotupa 'uhuru na haki', lakini kwa bahati yetu nzuri tukawa na kiongozi ambaye hana hizo sifa za ukandamizaji, yeye akajikita kwenye, kwa mfano kuimarisha elimu yetu ikawa bora kabisa; akahimiza wananchi wetu na kuwaelimisha juu ya kufanya kazi zao kwa weledi, iwe kilimo, uvuvi, ufugaji, n.k., na wananchi wakaitikia wito wake; na nchi kwa neema za Mwenyezi Mungu ikazalisha, mvua nzuri, miundombinu ya umwagiliaji, n.k.

Kiongozi huyu, pia akahakikisha kwamba juhudi za wananchi wake hazihujumiwi (rushwa, na mauchafu mengine akayadhibiti)

Na usisahau kwamba, nchi yake hiyo pia, haikwarudhani na nchi nyingine bila ya sababu za msingi, kwa hiyo mashirikiano na nchi nyingine ni mazuri, na biashara zinafanyika vizuri

Siwezi kuorodhesha mambo yote muhimu anayoweza kuyafanya kiongozi huyo hapa, lakini tuseme tu anajitahidi kwenye maeneo yote hayo.

Sasa swali ni hilo: nchi hii haiwezi kuwa na sura tofauti, hata kama bado haina katiba mpya na nzuri? Na hapa sisemi kwamba hilo si tamanio. Tamanio hilo lipo, lakini ni kwamba bado halijatekelezwa tu.

Kuna nchi zimewekwa kama mifano kwenye uzi huu, ambako hawakusubiri wawe na katiba nzuri ndipo wageuze hali za maisha ya wananchi.
 
Ndugu,
Kiongozi huyo umsemaye labda awe Malaika ndio atakamilika kwenye sifa hizo. Kama atakuwa ni mwanadamu kama sisi wenye nyama na damu, kwa kutumia utashi wake anaweza akajitahidi kuanza vizuri, lakini atakuja pwaya na hatimae kuwa kero.
Kwanza atakujajikuta yuko peke yake na maono yake (binafsi). Lakini baya zaidi, katika changamoto za uendeshaji, ataanza kuingiza hisia zake na huku akiyumbishwa na presha za wanandugu, marafiki, wapenzi, washikaji, matapeli na hata majambazi wakitumia maeneo ya udhaifu wake kama binadamu.
Hii itatoa fursa kwa shetani kumchota na kumfanya dikteta anaewaogopa na kuanza kupambana/kuwadhuru hata wananchi wake.
Yanayokea sehemu mbalimbali yanapaswa kuwa mafunzo kwetu.
Bila uwepo wa katiba bora itakuwa sio rahisi kwa kiongozi kujenga mifumo, sheria mbalimbali na taasisi imara endelevu za kuwezesha kujenga na kusimamia nchi na taifa kwa haki na uhuru wa wananchi wenye furaha.
Sasa hivi tunayo katiba lakini ina mapungufu mengi. Yatakiwa katiba BORA itakayo wezesha kudhibiti yeyote hata KIONGOZI aliye madarakani atakapoacha njia.
AMEN
 
Kiongozi huyo umsemaye labda awe Malaika ndio atakamilika kwenye sifa hizo. Kama atakuwa ni mwanadamu kama sisi wenye nyama na damu, kwa kutumia utashi wake anaweza akajitahidi kuanza vizuri, lakini atakuja pwaya na hatimae kuwa kero.
Hapana, sio malaika, ni mtu dhaifu kama tulivyo wote, ila awe anaongozwa na kulipenda taifa lake tu basi. Awe ni MZALENDO wa nchi hii, hiyo ni sifa tosha kabisa.
 
Ipo mifano mingi hai
Mwanamapinduzi Sekou Toure wa Guinea alianza kama mzalendo aliyekataa kabisa ukoloni mamboleo wa Ufaransa. Kwa hasira Ufaransa iling'oa hata reli wailiyoijenga kabla ya huru. Aliishia kuwa dikteta aliyeogopwa na wananchi nahata Kwameh Nkrumah aliyekuwa ukimbizini huko. Kaisome itakufungua.
 
Hapana mkuu bado nipo sahihi kwa hili. Swala la kufanya mapenzi halitakiwi kuadhibiwa kwa adhabu kali kama hii. Okay hebu jaribu kuliangalia kwa hii angle: mkipeana mimba nani anaathirika? Jaribu kutafakari nje ya box. Halafu mbona nchi zilizoendelea hazina sheria kali kama hii? Kufanya mapenzi hakurudishi maendeleo nyuma na pia hakuna mtoto wa kike anayefurahia kupata ujauzito kabla hajawa tayari kuwa na familia, ujauzito ni adhabu tosha kwa wahusika. Nchi zote zilizoendelea hazina sheria kama hii. Hii ni sheria ya kikandamizaji na imepitwa na wakati katika huu ulimwengu wa watu wastaarabu.
Nchi unazosema za nnje ukiangalia Kama si Raia mmoja mmoja ama Taifa kwa ujumla wameendela na pengine Kuna funds za kuhudumia vitu Kama hivyo..bosi kwa mengine unaweza kuwa right Ila kwenye suala la kuruhusu mimba shuleni..big no..utakuwa na Taifa la wajinga wanaojifunza kungonoka kuanzia darasa la nne mpaka chuo kikuu..kila wakikutana nyeti zinawasha...muda wa Kazi wanakuja kushtuka mtu Ana miaka 45 huko..watoto wamejazana wasio na baba wala ndugu..umaskini unazidi kuongezea na gharama za maisha kuwahudumia hao watoto zinakuwa nyingi..so dawa ya hiyo..ni kifungo cha miaka 100 kabisa..hii itasaidia kuwafanya mabazazi kuacha hizo tabia ..lakni mtoto wa kike kujua kuwa anapasawa kusoma Kama kufeli afeli kwa mengine na sio mapenzi ama ujinga ujinga wa ngono.....
 
mkipeana mimba nani anaathirika?
Mzee.kwenye hili wacha Kama Taifa tupate hasara na sio kuendelea kukumbatia ujinga wa kuangaliana usoni kwa kupoteza muda.bure kusomesha wazazi..ukishakuwa mwanafuzni chagua Moja..kusoma.ama.kukunana nyeti na mwenzako..na kamautaamua vyote mimba uijue na kujikinga nayo..ukipata..hakuna kuvumilia ama.kuchekeana chekeana kwa hadithi tamu tamu za haki za.mtoto kusoma...kamata huyo jamaa..aozewshwe kwa nguvu..akikataa asweke jela maisha..kwa kuharibu future na mwenzake..huyo aliyebeba mimba kwa kujua ama.kutokujua..abaki mtaani akilea mwanae..akitaka kusoma akasome elimu ya memkwa...hii nchi tumechezewa Sana kwa kuendekeza mambo ya haki za binadamu
 
Naheshimu mtazamo wako mkuu ila na mimi acha niendelee kuamini swala la mimba ni maamuzi ya watu wawili walioridhia kufanya hicho kitendo hivyo adhabu ya miaka 30 ni uonevu.
 
Hizo pesa za kuwapa watu wale Ili watuandikie Katiba,ni kupoteza pesa ya umma tu,Katiba haileti maendeleo,inahitajika na utashi wa kisiasa,
Kenya Wana Katiba nzuri Afrika,mbona hakuna maendeleo,China,Russia,North Korea hakuna Katiba "nzuri"lakini nchi zimeendelea sana,sie tuna hitaji viwanda,sio vyerehani na upuuzi wa kusema kila mkoa una viwanda 100!!
Kama music industry ilivyofanikiwa,tufsnye na sekta zingine ziwe hivyo,mifsno ya kuiga ipo Mingi,Dubai,Philippine,malaysia,Japan,Korea,china,hii nchi inakosa utashi wa kisiasa tu,
Watu wanapenda chama kuriko nchi.haya mavyeo ya kupeana hayawezi kutusaidia,kwanza inabidi yafutwe.
RC hana kazi yoyote zaidi ya kuwa nyapara tu,
Tanzania tuliwahi kuwa na viwanda vya radio,betri,sana za kilimo,pale kibaha tulikuwa tuna assembling plant ya scania miaka ya 90!sasa hv tunayo skilled labour kwanini hatuna viwanda vya magari,compyuta,Tunaishia kuagiza china!?
Serikali inabidi isaidie kuanzisha hivi viwanda sio serikali inaenda kuanzisha kiwanda Cha kusaga unga wa lishe!
Usijidanganye boss, katiba nzuri ya kumwahakikishia mtu haki na usalama wake ni muhimu kuliko hivyo viwanda
 
Katiba bora inatoa fursa ya kila raia kupata maendeleo binafsi ya kiuchumi. Katiba bora inatoa fursa kwa nchi kuendelea kiuchumi. Katiba bora inasababisha watu wasione kufanikiwa kwenye maisha sio lazima uwe mwanasiasa. Katiba bora inaleta furaha kwa raia wake. Katiba ni msingi wa sheria zote. Sheria yoyote inayopingana na katiba huwa challenged mahakamani na ikionekana ipo inconsistency na katiba hufutwa, kwa hiyo ikitokea sheria yoyote kandamizi ikatungwa na ikaonekana inapingana na katiba itafutiliwa mbali. So unaweza kuona umuhimu wa katiba bora.
 
Tunaanza lini kupush Kiswahili kitumike kwenye elimu yetu?
Sidhani kama tutakuja kufika dunia ya kwanza kwa kutumia elimu ya sasa ambayo walimu na wanafunzi wanatumia lugha ambayo hawaifahamu vizuri na pia elimu ambayo mahali pake ni shule tu, ukitoka shule haina kazi.
 
Wakati nipo sekondari nilikuwa natamani niwe sehemu ya watunga sera za nchi au kuwa kiongozi serikalini, na hii ilisababishwa na jinsi nilivyokuwa naona mambo yanavyoendeshwa nchini. Niliona bila kuingia ndani ya siasa siwezi kubadirisha chochote, nitabaki kuwa mtazamaji tu, kama kuna mambo hayapo sawa na ninahitaji kuyabadirisha sina budi kuingia jikoni na hii ndoto nahisi siku moja itakuja kutimia. Mniombee.

Kwa sasa kila nikiiangalia nchi yangu naona inahitaji viongozi wenye maono na mikakati isiyoyumba ili kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kwanza. Nchi za Ulaya na Amerika ya kaskazini hazijaamuka tu siku moja zikawa pale zilipo. Viongozi wake walikuwa na maono na mikakati isiyoyumba, na kila rais au kiongozi aliyekuwa anapata dhamana ya kuongoza alikuwa anatembea mle mle kwenye yale maono na mikakati iliyowekwa na watangulizi wake. Kama wao waliweza kuwa ulimwengu wa kwanza kwa nini sisi watanzania tushindwe ukizingatia sisi tuna rasimali za asili nyingi kuwazidi wao, tuna hali ya hewa nzuri, tuna ardhi inayomea kila aina ya mmea.

Natamani Tanzania iwe nchi ya kwanza Africa kufikia uchumi wa kwanza. Hili lipo ndani ya uwezo wetu watanzania, ni swala la kuamua tu na kujifunga mkanda.

Naomba tujadili kidogo nini kifanyike, hii ni nchi yetu, hatuna nchi nyingine zaidi yahii.

Binafsi vifuatavyo ni baadhi ya mambo ambayo yakifanyika Tanzania inakuwa ni miongoni mwa nchi za ulimwengu wa kwanza.

  • Lazima tupate katiba nzuri inayokwenda na wakati tulionao
  • Kwenye katiba kuanishwe malengo ya muda mrefu na ya muda mfupi.
  • Moja ya malengo ya muda mfupi yanaweza kuwa mengi ila nitataja machache ambayo tunaweza kuanza nayo kama nchi, i. kuhakikisha serikali inakuja na sera za kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana. Hapa serikali inatakiwa kuja na mikakati ya kuchochea uwekezaji kutoka ndani na nje. Kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ili kutengeneza ajira. Serikali inaweza kutoa incentives kwa wawekezaji. Hii inaweza kuwa katika mfumo wa kupunguza kodi au kupunguza gharama za uagizaji wa mitambo ya viwandani, au serikali inaweza kutoa asilimia fulani ya kusaidia manunuzi ya mtambo wowote utakaonunuliwa na muwekezaji atakayekuwa tayari kujenga kiwanda fulani. Kwa mfano serikali inahitaji muwekezaji kwenye kiwanda cha mafuta ya kupikia au sukari kwa sababu kuna upungufu wa hizo bidhaa nchini. Serikali inaweza kutangaza kwamba muwekezaji mzawa atakayejenga kiwanda cha sukari au mafuta ya kupikia, serikali itachangia asilimia 25 ya gharama ya huo mtambo. Au serikali inaweza kutangaza kwamba kampuni yeyote itakayoweza kuajiri wafanyakazi kuanzia 20,000 haitalipa tozo ya Skill Development Levy (SDL). Hii ni mifano tu, watunga sera watatakiwa wewe wabunifu wa kubuni njia ambazo zitasaidia kuchochea ajira
  • ii. Lengo jingine la muda mfupi linaweza kuwa hili; Hizi nafasi za uteuzi zenye mishahara mikubwa kama ukuu wa mikoa, ukuu wa wilaya, ukatibu mkuu, ukatibu tawala na zingine zote zinazoshabihiana na hizi zitumikiwe kwa miaka miwili tu ili kuwapisha wengine. Sio mtu mmoja anakuwa kwenye hizo nafasi kwa muda mrefu. Wewe kama upo kwenye hizo nafasi na let’s say unapata mshahara wa milioni 4 kwa mwezi kwa muda wa miaka 2 utakuwa umetengeneza 96,000,000. 96,000,000 inakutosha sana kwenda kuanzisha biashara au uwekezaji na ukasaidia kutoa ajira kwa wengine. Kufikia uchumi wa duania ya kwanza sio lelemama hivyo uwajibikaji inabidi uanzie kwa viongozi wenyewe. Kwa hiyo kukiwa na utaratibu wa kuachiana madaraka na kwenda kuanzisha biashara baada ya kuachia madaraka kunakuwa na multiplier effect kwenye uchumi hususani kwenye kutengeneza ajira maana watanzania wengi wataajiriwa kwenye hizo nyadhifa na pia watanzania wengi wataajiriwa kwenye hizo ajira zitakazotengenezwa na hao viongozi walioachia madaraka baada ya miaka miwili.
  • iii. Lengo jingine la muda mfupi ni hili, au linaweza kuwa la muda mrefu inategemea litadumu kwa muda gani; kwa mfano kwa sasa bei ya sukari na mafuta ya kupikia yamepanda bei karibia 60% hii ilisababishwa na serikali kupiga marufuku uagizwaji wa hizi bidhaa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani ilihali viwanda vya ndani havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya ndani. Madhara yake ni bei ya sukari na mafuta imepanda bei na imeshindwa kushuka licha ya matamko ya viongozi kuwa bei ishuke, na hii bei inamuumiza mlaji wa mwisho. Kama hakuna muwekazaji, serikali inaweza kuanziasha kilimo cha alizeti na karanga na kujenga kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia. Serikali inaweza kuanzisha mashamba ya miwa na kujenga kiwanda cha sukari. Tanzania tuna ardhi yenye rutuba kila mkoa hivyo serikali ikiamua kutatua hii changamoto ya sukari na mafuta ya kupikia haishindwi. Natambua kiuchumi sio afya kwa serikali kujihusisha moja kwa moja kwenye biashara lakini kuna exceptional cases kama hizi, sidhani kama kutakuwa na madhara kama serikali itachukua jukumu la kuzalisha bidhaa ambayo private sector imeshindwa kuzalisha kwa kiwango kinachohitajika nchini. Nadhani huu uwekezaji kwenye hizi bidhaa ni wenye tija zaidi kwa watanzania kuliko uwekezaji wa kwenye ndege. Ndege wanapanda watanzania wachache wenye uwezo lakini sukari na mafuta ya kupikia yanatumiwa na watanzania wote, hivyo unaweza kuona manufaa kwa watanzania kama serikali itaamua kuwekeza kwenye bidhaa ambazo sector binafsi imeshindwa kukidhi mahitaji ya walaji. Pia kama serikali itawekeza kwenye hii miradi itasaidia kutengeneza ajira hivyo tatizo la ajira litazidi kupungua maana kwenye hayo mashamba ya miwa, karanga na alizeti watanzania wataajiriwa, kwenye hivyo viwanda vya sukari na mafuta pia watanzania wataajiriwa.
  • Malengo ya muda mrefu
  • Malengo ya muda mrefu yatakuwepo mengi kulingana na ubunifu wa watunga sera wetu watakaopewa hii dhamana, ila hapa nitataja machache ambayo yanaweza kuwemo kwenye hayo malengo
  • i. Elimu,
  • Hakuna nchi yeyote katika ulimwengu wa kwanza iliyoendelea kiuchumi bila kuweka mifumo mizuri ya elimu, na zaidi ya yote bila kuwekeza kwenye masomo ya sayansi na hesabu. Elimu bora ndio kila kitu kwenye maendeleo. Sasa hivi dunia ipo kwenye ulimwengu wa sayansi na tekinologia, bila elimu tutabaki kuwa wachuuzi tu, hatuwezi kumiliki na kuendesha viwanda vyetu. Kuna rafiki yangu ni raia wa Canada ila ana asili ya kieritrea, ana ndugu zake wa damu Ujerumani na nchi za Scandinavia. Nchi zote hizo amefika na kukaa kidogo. Aliniambia “Africa bila kuwekeza kwenye elimu tutabaki kuwa nyuma siku zote, Africa itapiga maendeleo makubwa ya kiuchumi kama itawekeza kwenye elimu hasa masomo ya sayansi na hesabu”. Alinitolea mfano nchi ya Sweden kama sikosei au the Netherlands ilikuwa masikini sana lakini serikali ilitunga sera na sheria kuhakikisha masomo ya sayansi na hesabu yanakuwa ya lazima, na kuhakikisha wanafunzi kutokea elementary school hadi chuo wanafundishwa vyema, wanapikika na kuiva kwenye hesabu na sayansi. Yalikuwa ni malengo ya muda mrefu lakini baada ya muda matunda yalionekana, na sasa kama mnavyoona hiyo nchi ipo ulimwengu wa kwanza. Anasema hiyo nchi walimu wanaongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa. Kwa hiyo sisi watanzania kama tunataka kufika huko lazima tuwekeze kwenye elimu, hakuna short cut ya maendeleo, lazima tuwe na mipango ya muda mrefu ambayo tutakuwa na uhakika kuwa baada ya muda flani tutakuwa level nyingine. Natambua tunaweza kuwa na changamoto ya kupata walimu wa hesabu na sayansi kukidhi mahitaji ya shule zetu lakini tukiamua hii changamoto tunaishinda. Kuishinda hii changamoto serikali inaweza kutangaza nafasi za kazi za ualimu wa hayo masomo duniani. Mtu yeyote kutoka nchi yeyote anayeyamudu hayo masomo aruhusiwe aje apate kazi, na viza yake isiwe na urasimu kuipata. Kuwe tu na screening ya uhakika ili isitumike kama uchochoro wa raia wa nchi zingine kuja kufanya yao Tanzania.

  • Nchi ya Korea ya kusini ina utaratibu wa watu kutoka mataifa ambayo English ni lugha ya nyumbani kuruhusiwa kwenda kufundisha kiingeeza huko. Ukiwa na passport ya hizo nchi unapata viza ya kwenda kufundisha kiingereza. Kwa nini Tanzania tusifanye hivyo.

  • Malengo ya nchi, rais akiingia madarakani lazima ayafuate.
  • Kwa sababu tumeamua kama nchi kufikia uchumi wa juu, itungwe sheria ya kumtaka kila rais anayeingia madarakani ayatekeleze malengo ya nchi. Rais hatakuwa na uwezo wa kuiendesha nchi anavyotaka yeye. Awe na job description kabisa kwamba watanzania wamejiwekea malengo haya hivyo ukiingia madarakani lazima uyatekeleze, ukienda kinyume na hayo malengo bunge linakutoa kwenye hicho kiti cha urais na makamu wa rais anachukua usukani au uchaguzi mwingine unafanyika. Katiba itaweka wazi kipi ni bora zaidi kati ya kufanya uchaguzi au makamu wa rais kushika madaraka.

  • Ili kuhakikisha hili linafanyika, inaweza kuundwa taasisi huru ambayo itakuwa inahakikisha rais anafuata katiba. Unajua sisi watanzania ni wapole sana. Tunaweza kuwa na katiba bora kabisa ambayo imeainisha mambo yote yanayotakiwa kutekelezwa na rais, na tukawa na taasisi amabayo jukumu lake ni kuhakikisha katiba haivunjwi. Lakini pamoja na kuwa na hivi vyote unaweza kukuta rais bado anavunja katiba na hiyo taasisi iliyoundwa kumuwajibisha rais haimfanyi chochote, na raia nao washatishwa kupigwa kipigo cha mbwa koko wamefyata hata kuandamana kushinikiza katiba ifuatwe hawawezi. Sasa nini kifanyike, labda inaweza kutungwa sheria inayotambua huu woga na udhaifu wa watanzania ikasema kwamba “Pale rais au kiongozi yeyote wa juu serikalini anapovunja sheria au anapoenda kinyume na mipango iliyaoanishwa kwenye katiba, raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki ya kufungua kesi katika mahakama za kimataifa ili kushikikiza katiba ifuatwe na kumwajibisha rais au kiongozi aliyevunja katiba au aliyeenda kinyume cha malengo yaliyoainishwa kwenye katiba”

  • Kwa muktadha huu mahakama za kimataifa zitakuwa zimearifiwa kuhusu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo zitakuwa na mamlaka yaku-prosecute kesi ya namna hii itakapoletwa mbele yake. Kuna watu wataanza kusema Konda msafi wewe sio mzalendo, rais wetu ashitakiwe nje tena? hapana mimi ni mzalendo, najaribu tu kuwa realistic. Haya ni mawazo tu ambayo yanaweza kufikiriwa kuingizwa kwenye katiba na sio lazima yaingizwe, huenda kukawa na mawazo bora zaidi ya haya ambayo yatasaidia kuhakikisha katiba inalindwa na malengo tuliyojiwekea kama nchi hayatelekezwi.

  • Rais kuachana na mambo ya uchama akiwa madarakani
  • Kwa sababu tumeamua kupiga kazi kwa ajili ya nchi yetu. Uchaguzi ukiisha na rais akatangazwa katiba imzuie rais kushabikia hadharani mambo ya chama chake badala yake awatumikie wananchi. Mambo ya mipasho kuwananga wapinzani yasiwepo, kauli za kuwagawa wananchi kwa misingi ya chama zisiruhusiwe. Rais ni rais wa raia wote na sio rais wa chama kilichompa ticketi ya kuwania urais. Mambo ya chama atayaongea akiwa kwenye vikao vya chama chao lakini anapokuwa nje au kwenye ziara za kikazi hataruhusiwa kuongea mambo ya kichama. Atatakiwa awe na kazi ya kuhamasisha umoja, ushirikiano na uzalendo na kutekeleza malengo yaliyoainishwa kwenye katiba.

  • Sheria kandamizi
  • Ili tufike tunakotaka, sheria kandamizi zote zifutwe. Sheria zina nafasi kubwa sana kwenye kuleta maendeleo. Sheria zote zinazokwamisha maendeleo zifutwe. Sheria zote kandamizi zifutwe. Mojawapo ya sheria kandamizi ambazo binafsi ningependa zifutwe ni hizi: sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF na PSSSF. Kumpangia mtu namna ya kutumia hela yake, hii sheria ni kandamizi. Fao la kujitoa lirudishwe. Mfanyakazi akiachishwa kazi au akiacha kwa hiari yake apewe hela yake ikamsaidie mambo yake. Haya mambo ya kumzuia kuchukua hela yake mpaka uzeeni hayafai. Apewe hela yake ili kama anataka kufanya biashara akafanye akatengeneze ajira. Sheria nyingine kandamizi ni hii ya kufungwa miaka 30 jela ukimpa ujauzito mwanafunzi. Hii sheria ukiachilia kuwa ni kandamizi pia inamnyima haki mtoto atakayezaliwa haki ya kulelewa na wazazi wake wote wawili. Unapomfunga baba wa mtoto huoni kama unakitesa kiumbe kisichokuwa na hatia? Baba ake mmemfunga, huyo mtoto atahudumiwa na nani? Mama mjamzito atahudumiwa na nani? Zaidi ya yote unapomfunga baba wa mtoto unapata faida gani? Sheria kandamizi zipo nyingi, hizi mbili ni mifano tu.
  • Karibuni tujadiliane, ushauri na mapendekezo. Tanzania ni yetu sote. Kazi ieendelee.
Pia kwa kuongezea kama kutunga katiba mpya ni gharama basi zinaweza kutungwa sheria mpya zinazoendana na mipango yetu ya kufikia uchumi wa juu, na sheria kandamizi zikafutwa. Hatutakiwi kuwa na sheria kandamizi kwenye ulimwengu wa sasa uliojaa watu wastaarabu. Katiba ya Jaji Warioba inaweza kutumika ila kukatungwa sheria zingine ambazo specifically kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya nchi.
Good read
 
Utoto utoto mwingi kwenye huu uzi.

Yaani Katiba iweke mpango wa maendeleo ya Taifa wa muda mfupi??

Si tutakua tunafanya amandment Kila mara??

Hoja nyingine zote ni marudio tu ambazo hakuna haja ya kuweka kwenye katiba.

Wakati mwingine inapaswa tunafahamu kwamba sio Kila jambo linatakiwa kuwekwa kwenye katiba

Na sio kila suluhu ya tatizo ni katiba.
 
GOOD
 
Wewe jamaa nadhani una shida mahali.
 
Back
Top Bottom