Rais Samia na Watanzania naomba mpitie hapa ili Tanzania ipae kiuchumi

Unadhani nini kifanyike turudi tena huko? Unadhani nini kifanyike Tanzania tufike level za mataifa ya ulaya ya magharibi?
Ile nguvu iliyotumika kuzalisha zao la mkonge itumike kuzalisha mazao ya chakula yatakayo uzika Afrika na duniani. Tuwatumie wataalamu wetu wa kilimo kuwafikia wananchi na kuwapa mwongozo wa kilimo bora.

Kuwe na biwanda vya packaging ambavyo vitaweka ubora wa mazao katika madaraja. Hivi vitazalisha ajira nyingi hasa kwenye distribution.

Wataalamu wa masoko washirikiane na mabalozi wetu kutafuta masoko nje ya nchi.

Wanaosababishia kampuni hasara wafukuzwe. Ingependeza kama kampuni za kilimo au packaging zingemilikiwa na vyama vya siasa au watu binafsi.
 
TUSIJIDANGANYE, hatuwezi kuwa na maendeleo endelevu yenye uimara na kuinua hali za wananchi mahali pasipo na katiba bora.
Kwa tafsiri pana, mstari wako huu unasema kweli.

Maana hata uwe na kila aina ya mavitu, mabarabara, mareli, madege na takataka zote, lakini kama huna HAKI/UHURU, ukweli ni kuwa huna maendeleo.
Lakini labda nitoe mfano mwingine: Hakuna katiba mpya nzuri inayotupa 'uhuru na haki', lakini kwa bahati yetu nzuri tukawa na kiongozi ambaye hana hizo sifa za ukandamizaji, yeye akajikita kwenye, kwa mfano kuimarisha elimu yetu ikawa bora kabisa; akahimiza wananchi wetu na kuwaelimisha juu ya kufanya kazi zao kwa weledi, iwe kilimo, uvuvi, ufugaji, n.k., na wananchi wakaitikia wito wake; na nchi kwa neema za Mwenyezi Mungu ikazalisha, mvua nzuri, miundombinu ya umwagiliaji, n.k.

Kiongozi huyu, pia akahakikisha kwamba juhudi za wananchi wake hazihujumiwi (rushwa, na mauchafu mengine akayadhibiti)

Na usisahau kwamba, nchi yake hiyo pia, haikwarudhani na nchi nyingine bila ya sababu za msingi, kwa hiyo mashirikiano na nchi nyingine ni mazuri, na biashara zinafanyika vizuri

Siwezi kuorodhesha mambo yote muhimu anayoweza kuyafanya kiongozi huyo hapa, lakini tuseme tu anajitahidi kwenye maeneo yote hayo.

Sasa swali ni hilo: nchi hii haiwezi kuwa na sura tofauti, hata kama bado haina katiba mpya na nzuri? Na hapa sisemi kwamba hilo si tamanio. Tamanio hilo lipo, lakini ni kwamba bado halijatekelezwa tu.

Kuna nchi zimewekwa kama mifano kwenye uzi huu, ambako hawakusubiri wawe na katiba nzuri ndipo wageuze hali za maisha ya wananchi.
 
Ndugu,
Kiongozi huyo umsemaye labda awe Malaika ndio atakamilika kwenye sifa hizo. Kama atakuwa ni mwanadamu kama sisi wenye nyama na damu, kwa kutumia utashi wake anaweza akajitahidi kuanza vizuri, lakini atakuja pwaya na hatimae kuwa kero.
Kwanza atakujajikuta yuko peke yake na maono yake (binafsi). Lakini baya zaidi, katika changamoto za uendeshaji, ataanza kuingiza hisia zake na huku akiyumbishwa na presha za wanandugu, marafiki, wapenzi, washikaji, matapeli na hata majambazi wakitumia maeneo ya udhaifu wake kama binadamu.
Hii itatoa fursa kwa shetani kumchota na kumfanya dikteta anaewaogopa na kuanza kupambana/kuwadhuru hata wananchi wake.
Yanayokea sehemu mbalimbali yanapaswa kuwa mafunzo kwetu.
Bila uwepo wa katiba bora itakuwa sio rahisi kwa kiongozi kujenga mifumo, sheria mbalimbali na taasisi imara endelevu za kuwezesha kujenga na kusimamia nchi na taifa kwa haki na uhuru wa wananchi wenye furaha.
Sasa hivi tunayo katiba lakini ina mapungufu mengi. Yatakiwa katiba BORA itakayo wezesha kudhibiti yeyote hata KIONGOZI aliye madarakani atakapoacha njia.
AMEN
 
Kiongozi huyo umsemaye labda awe Malaika ndio atakamilika kwenye sifa hizo. Kama atakuwa ni mwanadamu kama sisi wenye nyama na damu, kwa kutumia utashi wake anaweza akajitahidi kuanza vizuri, lakini atakuja pwaya na hatimae kuwa kero.
Hapana, sio malaika, ni mtu dhaifu kama tulivyo wote, ila awe anaongozwa na kulipenda taifa lake tu basi. Awe ni MZALENDO wa nchi hii, hiyo ni sifa tosha kabisa.
 
Hapana, sio malaika, ni mtu dhaifu kama tulivyo wote, ila awe anaongozwa na kulipenda taifa lake tu basi. Awe ni MZALENDO wa nchi hii, hiyo ni sifa tosha kabisa.
Ipo mifano mingi hai
Mwanamapinduzi Sekou Toure wa Guinea alianza kama mzalendo aliyekataa kabisa ukoloni mamboleo wa Ufaransa. Kwa hasira Ufaransa iling'oa hata reli wailiyoijenga kabla ya huru. Aliishia kuwa dikteta aliyeogopwa na wananchi nahata Kwameh Nkrumah aliyekuwa ukimbizini huko. Kaisome itakufungua.
 
Nchi unazosema za nnje ukiangalia Kama si Raia mmoja mmoja ama Taifa kwa ujumla wameendela na pengine Kuna funds za kuhudumia vitu Kama hivyo..bosi kwa mengine unaweza kuwa right Ila kwenye suala la kuruhusu mimba shuleni..big no..utakuwa na Taifa la wajinga wanaojifunza kungonoka kuanzia darasa la nne mpaka chuo kikuu..kila wakikutana nyeti zinawasha...muda wa Kazi wanakuja kushtuka mtu Ana miaka 45 huko..watoto wamejazana wasio na baba wala ndugu..umaskini unazidi kuongezea na gharama za maisha kuwahudumia hao watoto zinakuwa nyingi..so dawa ya hiyo..ni kifungo cha miaka 100 kabisa..hii itasaidia kuwafanya mabazazi kuacha hizo tabia ..lakni mtoto wa kike kujua kuwa anapasawa kusoma Kama kufeli afeli kwa mengine na sio mapenzi ama ujinga ujinga wa ngono.....
 
mkipeana mimba nani anaathirika?
Mzee.kwenye hili wacha Kama Taifa tupate hasara na sio kuendelea kukumbatia ujinga wa kuangaliana usoni kwa kupoteza muda.bure kusomesha wazazi..ukishakuwa mwanafuzni chagua Moja..kusoma.ama.kukunana nyeti na mwenzako..na kamautaamua vyote mimba uijue na kujikinga nayo..ukipata..hakuna kuvumilia ama.kuchekeana chekeana kwa hadithi tamu tamu za haki za.mtoto kusoma...kamata huyo jamaa..aozewshwe kwa nguvu..akikataa asweke jela maisha..kwa kuharibu future na mwenzake..huyo aliyebeba mimba kwa kujua ama.kutokujua..abaki mtaani akilea mwanae..akitaka kusoma akasome elimu ya memkwa...hii nchi tumechezewa Sana kwa kuendekeza mambo ya haki za binadamu
 
Naheshimu mtazamo wako mkuu ila na mimi acha niendelee kuamini swala la mimba ni maamuzi ya watu wawili walioridhia kufanya hicho kitendo hivyo adhabu ya miaka 30 ni uonevu.
 
Usijidanganye boss, katiba nzuri ya kumwahakikishia mtu haki na usalama wake ni muhimu kuliko hivyo viwanda
 
Usijidanganye boss, katiba nzuri ya kumwahakikishia mtu haki na usalama wake ni muhimu kuliko hivyo viwanda
Katiba bora inatoa fursa ya kila raia kupata maendeleo binafsi ya kiuchumi. Katiba bora inatoa fursa kwa nchi kuendelea kiuchumi. Katiba bora inasababisha watu wasione kufanikiwa kwenye maisha sio lazima uwe mwanasiasa. Katiba bora inaleta furaha kwa raia wake. Katiba ni msingi wa sheria zote. Sheria yoyote inayopingana na katiba huwa challenged mahakamani na ikionekana ipo inconsistency na katiba hufutwa, kwa hiyo ikitokea sheria yoyote kandamizi ikatungwa na ikaonekana inapingana na katiba itafutiliwa mbali. So unaweza kuona umuhimu wa katiba bora.
 
Tunaanza lini kupush Kiswahili kitumike kwenye elimu yetu?
Sidhani kama tutakuja kufika dunia ya kwanza kwa kutumia elimu ya sasa ambayo walimu na wanafunzi wanatumia lugha ambayo hawaifahamu vizuri na pia elimu ambayo mahali pake ni shule tu, ukitoka shule haina kazi.
 
Good read
 
Utoto utoto mwingi kwenye huu uzi.

Yaani Katiba iweke mpango wa maendeleo ya Taifa wa muda mfupi??

Si tutakua tunafanya amandment Kila mara??

Hoja nyingine zote ni marudio tu ambazo hakuna haja ya kuweka kwenye katiba.

Wakati mwingine inapaswa tunafahamu kwamba sio Kila jambo linatakiwa kuwekwa kwenye katiba

Na sio kila suluhu ya tatizo ni katiba.
 
GOOD
 
Wewe jamaa nadhani una shida mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…