Hapana, mimi na wewe ni kama mbingu na ardhi. Unayoyaamini na kuyatetea toka nikufahamu humu JF hatujawahi kutaka vitu vinavyofanana ila kwa tabia chafu iliyojengeka ndani ya taifa hili ya unafiki, umdhaniye ndiye mara nyingi huwa siye.
Unaona? Kwa unafiki unatetea hata kisichohitaji utetezi. Ama hujui historia ya JPM au kwa makusudi huo ndio upeo wako wa kufikiri pamoja na kuwa kwenye kundi la wanaojiita wasomi, msomi my foot! Unajidhalilisha mdogo wangu...pata japo kaujasiri kadogo wa kuita koleo kwa jina lake rasmi.
Yawezekana? Labda, kwa hiyo hakuwa anaumwa na ndio sababu ya kubugia kikombe cha babu akiwa waziri wa ujenzi katika serikali ya Kikwete?
Hakuna kitu kibaya kama kudhani unafahamu kumbe hujafamu. Hapo tatizo lako moja kwa moja linakuwa kubwa zaidi, pole.
Are you kidding me? Kwamba Rais Mh. Samia Suluhu Hassan hana tofauti na kinyago? Mbona hapa ni kama unamtukana? Ninavyojua Katiba yetu, pamoja na mapungufu yake inaeleza wazi kabisa jinsi Rais atakavyopatikana ikitokea aliye madarakani akaaga dunia.
Kama nilivyosema toka mwanzo na kama madai yako ni kweli, tunalo taifa la wanafiki kuliko wengine tunavyofikiria. Sisi wengine hatushangai CCM ya wadhalimu kurudi madarakani. Mara ngapi wamedai watakaa madarakni hata kwa miaka mia?
Nilicho na hakika nalo ni kwamba hawatakaa madarakani milele...kuna siku wataondoka tu. Hata Kim Jung un wa Korea Kaskazini kuna siku ataondoka tu...mbona jiwe kaondoka?
Nashangaa haya unayajua leo. CCM ni genge kama magenge mengine ya kihalifu yalivyo lakini iko siku wataondoka tu. Kama alivyowahi kuonya Mwalimu, kama hawaondoki kwa amani wataondoka kwa shari. Hii itatokea wakati wake ukifika na si leo wala kesho.
Ukishakua mwana CCM wewe ni mmoja wao hata kama unajidanganya eti uko tofauti.
Huwezi kumtofautisha jiwe na hilo genge, labda walizidiana ujanja tu. Wakati wenzie wanatumia ujanja ujanja na akili yeye alitumia mabavu. Alisema atahakikisha anaua upinzani (utadhani upinzani umewahi kuwa madarakani wakalififikisha taifa mahali ambapo alihitaji kulinyosha).
Uchafuzi wa mwaka 2020 ni ishara tosha kwamba naye alikuwa mwovu tu kama wenzake. Kizazi kipya kitainuka Tanzania ambacho hakitavumilia huu ukondoo wa kijinga wa Watanzania.
Kaniki rangi yake hata ukiifua kwa OMO au JIK haitakati ikawa nyeupe na kumbuka ndege wafananao huruka pamoja. Kaa ukijua kuna Watanzania walioikataa CCM toka inaasisiwa mwaka 1977 ikiwa mikononi mwa Baba wa Taifa.
Jiwe alikuwa katili toka utotoni na hata ubunge wake wa kwanza alishinda kwa mbinde. Hakuwahi hata mara moja kushinda uchaguzi wowote ule kihalali katika maisha yake kwani hakujua kabisa maana ya ushindani.
Hujui chochote unachosema, everything about Magufuli ilikuwa fake. Magufuli naweza kumfananisha na kiongozi wa juzi wa Marekani anayeitwa Trump. Bahati ya Marekani ni kwamba misingi ya utawala iko imara na ingeyumba kidogo tu, Trump hangeachia madaraka kama rafiki yake Putin wa Urusi.
Siku njema
Waberoya.