Kinachonipa amani ni kwamba wengine angalau tulifanya jitihada kwa kwanza, kutoa ushauri na pili, kuonesha nia ya kutoa ushirikiano kama ushauri wetu ungetiliwa maanani japo kwa asilimia ndogo.
Kwa bahati mbaya, pamoja na kutoa ushauri kwa moyo safi kabisa, Rais Samia Suluhu Hassan, kwa sababu ambazo tulishindwa kuzielewa awali aliamua kuzingatia ushauri ulio kinyume na ushauri wetu.
Yawezekana tulifanya makosa kuweka matumaini yetu kwa msaidizi mkuu wa mwendakuzimu kwa miaka mitano na kauli yake ya kazi iendelee, ilizima ndoto yetu na matumaini yetu kuyeyuka taratibu.
Kauli huumba na kwa tunayoyashuhudia hivi sasa tuombe Mungu atuepushe na yote sisi wajawa wake.