Rais Samia nakukumbusha kuwa siku hazigandi, zayoyoma. Samaki mkunje angali mbichi, akikauka hakunjiki

Hivi katiba mpya imo kwenye ilani ya CCM yenye kurasa Mia tatu na ushee? Au una matakwa yako na wapinzani kidogo walio baki?
 
Tatizo unaandika maneno mengi sana!
 
Nimekusoma kwa taratibu sana ili nikuelewe, kwa sababu naona uwasilishaji wako kidogo ni mgumu kwangu kuuelewa haraka.

Nimechukua sehemu ndogo tu ya andiko lako hapo juu, nilijadili, kwani naona yamo ninayokubaliana nawe, na mengine, ni kama kawaida, sikubaliani.
Mfano mmoja ni kama hayo maneno ya mwanzo: "Kosa la JPM ni kuruhusu baadhi ya watu wake kuwa wababe, na yeye kushindwa kuchukua hatua."
Sasa sidhani kama kweli unayasema haya kwa moyo wa dhati kabisa. Chukulia Mkuu wa Wilaya Hai, Sabaya - huyu kateuliwa kwa maksudi mazima akamshughulikie Mbowe, kwa hiyo hapa unamlaumu mteuliwa na huoni mteuzi ndiye mwenye nia ovu tokea mwanzo.
Mifano ya namna hii ipo mingi.
Ninalokukumbusha hapa ni kwamba, usitafute wa kuwalaumu na kuacha mhusika mkuu ambaye ndiye anayestahili lawama.

Hilo la "kuweka wapinzani wake mbali sana..." Magufuli hakuwa mtu stahimilivu. Tabia hii ameionyesha mara nyingi sana, sio kwa wapinzani peke yake. Hakuwa mtu mwenye ustahimilivu, hata katika mambo ambayo hayana maana sana. Yeye alijua anayo madaraka yote, na mwenye kuonyesha upinzani kwake ni lazima akipate. Hiyo ilikuwa ni tabia yake kama binaadam, na kwa mtu kiongozi, hastahiri kamwe kuwa na tabia ya namna hiyo. Huu ulikuwa ni upungufu mkubwa sana kwake.

Ninapokubaliana nawe moja kwa moja ni katika hili la :
"...Kuumiza CCM, na kukata mirija yao." Pamoja na kufanikiwa katika hili, tatizo ni lile lile la kutokuwa na uwezo kujenga miundo endelevu ndani ya chama ili hata akiwa hayupo pawepo na wafuasi walioelewa alichokuwa akikipigania. Kwa hiyo, hata kama kafanya jambo jema kwa muda huo mfupi aliokuwa akikiongoza chama, kuondoka kwake hakuacha kitu. Aliokuwa amewazibia njia, sasa wapo huru kuendeleza pale walipozibiwa.

Ninakubaliana tena nawe, kwamba tujiandae kuandika na kusoma mengi. Mama huenda hata Kikwete akawa nafuu kwetu.
Hofu kubwa ni kwamba haieleweki kama anajua anachotaka kukifanya katika miaka minne hii!
 
Mzee nwenzangu..Katiba Mpya itakayowaridhisha wapinzani haiwezi kutolewa na chama tawala na haiwezi kupatikana kama hisani.
Kwa ufahamisho tu ndugu yangu Mzee Mwanakijiji, Katiba Mpya haitolewi kama hisani na haitolewi kuridhisha tu sehemu ya jamii bali jamii nzima ya Watanzania na ndiyo maana inaanza kwa kusema Sisi Watanzania tumeamua...

We the people of the United Republic of Tanzania...
 
Mkuu hatuli katiba ,hata ije katiba kutoka kwa malaika kama wanaoongoza hawana utashi na hiyo katiba ni bure kabisa, mfano hai ni hapo kwa jirani zetu Kenya pamoja na kuwa moja ya katiba bora kabisa lakini matokeo yake ni kuongezeka kwa ufisadi,ukabila n.k lakini papo hapo nchi ka Uingereza haina katiba na watu wake wanaishi vizuri sana na hata katiba ya marekani ni ileile ya miaka kibao, huku Afrika ya Kusini wana katiba nzuri lakini bado haiwasaidia wananchi zaidi ya wala keki wa siku zote. Fanya kazi ,omba tuboreshewe mambo ya afya,elimu,miundo mbinu,masoko ya mazao yetu na tuongeza ajira mambo ya katiba ni faida ya wanasias na wateule na familia zao wengine hayatusaidii.
 
Nikiwa naangalia mpira natamani niwatoe wote nicheze peke yangu huku nikiamini matokeo yatakuwa bora zaidi

Rais huwa wanapimwa kwa miaka [emoji817] sasa methali kibao siku 40
 

Fact ni JPM kafariki๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ alikuwa mbaya, mzuri watu wako watakaompenda na kumchukia ...ni asili

Kikubwa ni kuwa tunawaza tofauti

Kuna watu ni wapinzania weledi na wanataka mabadiliko sana

Hawa weledi nao washajibatiza uweledi na wakiona mwingine anadai kilekile anakuwa hatakiwi kwa sababu approach na mitazamo imetofautiana

kwa style ya kupambana na adui mmoja CCm ili hali wanaoipiga wametofautiana na tena kwa kudhalilishana....CCM will stay there

Ndio maana demokrasia bado ngumu afrika,,maana hata wale waumini wa demokrasia hawataki approach au mawazo tofauti kwa sababu wao ni wapinzani kweli kweli

Nadhani kipimo cha imani fulani ni matokeo au mabadiliko au mwamko...
 
Umeandika vizuri ila huja fijian pitching ya andika lako
 
Kwangu mpk sasa bado naona bla bla bla tu.
Na ndiyo maana tunampa tahadhari kama hizi...akilegalega asitegemee kupata ushirikiano wa baadhi yetu tuliounga mkono kwa asilimia 100% kuheshimiwa kwa Katiba na hivyo kumwezesha yeye kuukwaa Urais ingawa hatukubaliani katika mengine mengi.

My advice to President Samia Suluhu Hassan...to be a good leader always be a first-rate version of yourself, instead of a second-rate version of somebody else!
 
"Samaki mkunje angali mbichi, hata akiwa kakauka mkunje mpaka anye"
 
Huenda toka nianze kukuona humu JF, sijawahi kukusoma ukitoa mawazo kwa makini kama haya, hata kama sikubaliani na kila kitu kilichoandikwa.

Umuhimu na uzuri wa katiba ni pale tu wanaoitumia na kuyaheshimu; wanafuata maelekezo ya katiba hiyo. Pia, ni lazima pawepo na mihimili na taasisi zinazosimamia na kuhakikisha kuwa katiba inafuatwa, na haikiukwi na yeyote, hata Rais, asiwe juu ya katiba.

Hapo, kuwa na katiba nzuri (inayojitosheleza kwa sehemu kubwa) ni jambo la muhimu.
Tumeona hapa mfano wa marehemu Magufuli akikanyaga hata hiyo iliyopo, pamoja na kwamba haikumruhusu aikanyage.

Lakini kilichonivuta hasa niku'quote' ni mistari hii ifuatayo:
Fanya kazi ,omba tuboreshewe mambo ya afya,elimu,miundo mbinu,masoko ya mazao yetu na tuongeza ajira mambo ya katiba ni faida ya wanasias na wateule na familia zao wengine hayatusaidii.
Haya maneno haya ni maneno yasiyofaa kabisa. Tumwombe nani..., anatufanyia hisani? Hawa viongozi sio tunaowaweka sisi hapo walipo ili watutumikie? Hapa unataka "tuwaombe", kama tunavyoomba na kugalagala chini ili tupate katiba mpya?

WaTanzania tutakapojitambua na kujua kwamba sisi ndio wenye mamlaka hapo ndipo katiba itakapokuwa na maana kubwa kwetu.

Huko kote ulikotaja, Marekani na Uingereza, wananchi wao hawaombi, wanaamuru. Hii ndiyo tofauti kubwa ya wao na sisi.
 
๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š๐Ÿค๐Ÿค
 
Ninaloweza kusema hapa ni kwamba, 'I am perplexed'.

Sijui neno zuri kueleza hali hiyo kwa lugha yetu adhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ