Rais Samia nakushauri kesho kawatembelee Taifa Stars kambini kwao

Rais Samia nakushauri kesho kawatembelee Taifa Stars kambini kwao

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
6,699
Reaction score
9,323
Rais Samia kesho jioni nenda kambini kwao,ukawatie hamasa vijana ili wacheze kufa kupona na kuifunga Morocco.Vijana wakikuona kambini kwao,watapandisha mori sana
 
Haitasaidia kitu. Kama safari imefika, imefika tu.

Miujiza huwa ipo.
Tuishi kwa matumaini.
Taifa stars inaweza kufanya maajabu.
Tukifungwa kutakuwa na maneno yafuatayo ya kutupooza:

"Vijana wamejitahidi, wamefungwa na timu bora! Ngoja tuangalie tulipoteleza na tujipange kwa AFCON."
 
Vizingiti kwa Tanzania
1. SUDAN
2.KENYA

Refa akiwa fair, Morrocco yeye atakaa mapema tu.
Ila mech kwann isiwe saa 10.
Kenya aliwafunga hawahawa Morrocco saa 9, tena akiwa pungufu toka dakika za nwanzo.

Nasisitiza refa akiwa fair,
Ni kwasabu Morrocco haisemwi vizuri kwa fitina, hila na figisu-figisu.

Tusubiri.
 
Haitasaidia kitu. Kama safari imefika, imefika tu.
Uko sahihi mkuu. Wachezaji wanahitaji morali kutoka ndani yao sio nje, Rais kuwatembelea kutawatia presha kubwa washindwe kuperfom.
 
Hivi kawaahidi nini. Luto kule anawapiga mipunga ya kutosha wachezaji.
 
Rais ana majukumu mengi, anawasaidizi ambao wanaipambania timu. Harafu ikifungwa hamkawii kusema Samia kasababisha
 
Rais Samia kesho jioni nenda kambini kwao,ukawatie hamasa vijana ili wacheze kufa kupona na kuifunga Morocco.Vijana wakikuona kambini kwao,watapandisha mori sana
Sio sahihi, akifuata ushauri wako probability kubwa ni timu kuvurugika. Nyota yake kipindi hiki ipo gizani.
 
Back
Top Bottom