Rais Samia nakushauri ufute safari za nje

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Nampongeza Chakwela kwa kufuta safari zote za nje hadi March 2024, wote walioko nje matembezi kurudi nyumbani, kupunguza matumizi ya Serikali pamoja na ma-allowance za wabunge na mawaziri ili kubalance uchumi wa Nchi yake. Mama Samia nakushauri na wewe uchukue uamuzi huo, safari za nje zina gharama kubwa na umaskini wetu hauwezi kwisha kwa kutembeza bakuli.
 
Hata huyo Chakwela wamalawi walianza kupaza sauti zao mwaka jana 2022 na aligoma, si hizo safari tu bali na misururu ya magari 80! yanayomsindikiza akienda saiti.
 

Itakuwa habari mbaya sana hii Kwa mwamba wa Msoga na yule mwenye wajomba zake Oman
 
Safari ni muhimu lakini sharti ziratibiwe, sasa ukiwa vasco da Gama zama hizi jau matumizi huwa ni makubwa sana
 
Yani serikali ambayo ipo kwa ajiri ya viongozi kutawala wananchi(sio kuwatumikia) wataanzaje tena kufikiria kupunguza matumizi ya serikali?
Ndiyo kwanza wanaongeza matumizi makubwa misafara sijui ya Rais, Makamu, PM, Naibu PM, Spika, Jaji, CDF, IGP, KM wa CCM, Msemaji wa CCM, Wastaafu n.k
 
Magufuli alisema kuwa atakumbukwa kwa mambo mazuri, mojawapo likiwa ni hili la kupunguza gharama zisizokuwa za msingi kwa serikali. Zambia wanazingatia hili, Malawi nao pia wamelianza.
Gharama gani alipunguza? Mbona mwenge aliuacha na hauna faida!! Maposho ya wabunge hakupunguza. Balozi zilikua zinafuja pesa, CCM ilikua inatumia ma V8 hata 30 kwenye msafara let alone rais akiwa na ziara mpaka aende na serikali nzima kumbuka msafara mrefu, helicopter juu n.k!! Haya akienda mkoani wanachukua kabisa ndege ya ATCL ile kubwa kuzunguka nayo badala ifanye business routes. Kumbuka hapo bado walikua na fungu la kununua wapinzani, kuwalipa kina Halima mdee ambao hawapo bungeni kwa mujibu wa sheria, na bado alinajisi uchaguzi uliotumia mabilioni!! Lakini bado tunaambiwa alipunguza matumizi?

Nilichogundua JPM alikua muigizaji mzuri, yaani unapunguza gharama zinazoonekana wazi ila zile za siri siri zinaendelea kutumika. That's politics.
 
Magufuli alisema kuwa atakumbukwa kwa mambo mazuri, mojawapo liigahilikupunguza gharama zisizokuwa za msingi kwa serikali. Zambia wanazingatia hili, Malawi nao pia wamelianza.
Nabii hakubaliki kwao
 
At least huyo akijatahidi hata kuthubutu!..

Vipi hawa wa sasa hivi?
 
NCHI INA BALOZI KILA NCHI LAKINI MISAFARA HAIKOMI KILA SIKU VIONGOZI WAPO ANGANI KAMA POPO

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
KUFUTA SAFARI NI UPUMBAVU WA KIJINGA KABISA HAJUI BINADAMU TUNATEGEMEANA.
 
Magufuli alisema kuwa atakumbukwa kwa mambo mazuri, mojawapo likiwa ni hili la kupunguza gharama zisizokuwa za msingi kwa Serikali. Zambia wanazingatia hili, Malawi nao pia wamelianza.
Hao wanajianda kwa uchaguzi wacha waende wakirudi waanze ujenzi na ss tupate pesa
 
Sijui kama utaeleweka,waliomzunguka ni wanufaika wakubwa kwa hizo safari
 
Lini utajifungua mimba ya Magufuli?[emoji6]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…