Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,467
- 1,697
Kusema kweli leo nimesikitika sana kuona aina ya muundo wa treni ambayo serikali yetu imeweka mkataba na kampuni ya Hyundai-Rotem ni treni zenye mwonekano wa ki-Hitler!
Mimi nilifikiri tunaondokana na treni zenye muundo wa kutisha za enzi za George and Robert Stephenson na kuingia kwenye era ya treni za umeme zenye kuburudisha macho kwa design kama za wenzetu wajerumani.
Mama samia Suluhu Hassan Rais wetu nani kakupa ushauri wa kutua saini ya makubaliano ya kununua treni za aina hiyo? Mimi sitaki kuamini na sikutegema kama aina ya treni ambazo zitatereza kwenye reli yetu zingekuwa na mwonekano huo kwenye hiyo picha ya taarifa tuliyoipata kwenye Website ya hiyo kampuni iliyo shinda zabuni ya Hyndai-Rotem. Mbona inatisha?
Nitashangaa sana kama upande mmoja tumejitahidi kutengeneza Stations nzuri, za kisasa na zenye mwonekano mzuri na wa kupendeza na kupata system yenye technology mpya, alafu leo tunaambiwa kuwa tunapata treni zenye vichwa na mabehewa ya enzi za Hitler? Ama kweli Tanzania tunawatu ambao kweli hawajui kwenda na na wakati. Watu wasiokuwa na test ya biashara. Mnategemea nani mtampata kwenye kwenye hayo ma-wreck yenu?
Mkurugenzi Kadogosa hii sio treni ambazo models zake mtangazaji wako Beni Mwanantala amekuwa akituonyesha kwenye maonyesho uwanja wa sabasaba kurasini.
That's awful! Are you really serious with this mkurugenzi?
Sasa naomba niambie kuna tofauti gani na SGR ya kenya kimwonekano? Inamaana mnatufanya sisi ni masokwe mpaka mnatuletea matakataka kama haya ambayo hakuna mtu anaye yataka?
Waziri wa Ujenzi na uchukuzi hivi ni sahihi kweli sisi watanzania mtusweke kwenye ma-wagon yanayo onekana kama treni za kusafirisha mizigo na wanyama kama haya ambayo hata hayavutii? Mmepewa bure nini? Ama ndiyo tuseme mmedhamiria nini kutuletea? Tuambieni?
Nilipokuwa kwenye jengo lenu la maonyesho ya sabasaba mwaka jana na kujionea mwenyewe models za treni na mabehewa ambayo Mr. Mwanantala alitupa maelezo yake, aisee, nilifarijika sana sana moyoni na niliwaombea baraka nyingi kwa muumba wetu za kuwaongoza vizuri katika shughuli zenu za kuwatumikia Watanzania.
Sikutegemea kabisa kuwa leo ingekuwa siku ya majonzi makubwa kwa kuona au kusikia mashine zitakazo tereza kwenye reli yetu ya kisasa ya SGR kumbe ni madudu ambayo yamepitwa na wakati na yasiyo na mvuto hata lidogo. ES IST SCHRECKLICH!
Hyundai Rotem wins contract to deliver trains to Tanzania - Fuentitech
The 97 cars operate at a top speed of 160km / hr. Credit: HYUNDAI ROTEM COMPANY. South Korean-based company Hyundai Rotem has won a $ 295.65 million (335.4 billion won) contract from the Tanzania Railways Limited (TRC) to deliver eco-friendly rail vehicles. Under the contract, TRC will receive $...
UP DATE:
Waziri wa Ujenzi na Mkurugenzi wa TRC wametoa clip ya kuonyesha baadhi ya treni tulizo nunua. Mungu ibariki Tanzania treni za kisasa za nyoka nazo zipo. Hongereni!!!
Nawashukuru wote walioshirikiana nami kwenye kutoa michango yao ya hoja.
Mungu awabariki wote na tuendelee kupigana kwa ajili ya maendeleo yetu na vizazi vyetu vya baadae.
Ningeona ajabu sana kama Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi wetu Kadogosa wange mwangusha Hayati Magufuli na vijana wetu ambao walijitokeza kwa wingi sabasaba mwaka jana kuupokea na kuuunga mkono mradi wetu kutoka kwa Hayati Rais wetu mpendwa Magufuli.
Leo ni siku ya furaha sana kwangu. Siku hizi zote nilikuwa silali vizuri ile report ya Hyundai- Rotem iliniumiza sana.
Na natoa pongezi kubwa sana na shukran nyingi kwa viongozi wetu wote waliohusika kwenye kuufanikisha huu mradi kwa mategemeo yetu na kusikiliza vilio vyetu vya kupata taarifa sahii juu ya mradi wetu huu. Mungu awabariki sana.
SGR IS OUR BABY!!!!!
Watanzania tuna sababu zote za kuwa proud of ourselves. Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe.
Watanzaniaaa tunapata pia Double Decks Tains. Oooh wie schΓΆΓΆΓΆΓΆΓΆΓΆn!!![emoji122][emoji122][emoji122]
Na kwa hali hiyo napenda kusema kuwa Mjadala wetu umefungwa.