Rais Samia alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi huko Marekani[ U.S.A.] alipata wasaa wa kuwahutubia waTanzania wanaoishi huko.
Alipokuwa anatoa hotuba yake palitokea tukio moja lililomfanya akumbuke nyumbani; ingawa alikuwa ughaibuni nalo lilikuwa pale UMEME ulipokatika wakati akitoa hotuba!!
Mheshimiwa Rais ikabidi aweke kibwagizo kuwa kumbe hata huku UMEME unakatika, ingekuwa nyumbani tukio kama hili January angesulubiwa!!
Tukumbuke tu kuwa tatizo la ukatikaji wa Umeme nyumbani sio sawa na ughaibuni; kwanza ule Umeme ulipokatika pale Nadhani Ilikuwa tatizo la switch ambapo Umeme ulirudi baada ya muda mchache tu ili hali sisi nyumbani umeme ukikatika unakatika kweli , kunasehemu watu wanakosa umeme wa kufanyia kazi hata wiki nzima hivyo hatuwezi kufananisha matatizo yetu ya umeme na wenzetu.
January ni lazima afanye kazi yake kwa weledi ingawa mfano ya Samia inaonesha kama vile kumkingia kifua kuwa hata Marekani pia unakatika, lakini umeme wa Marekani unarudi saa hizo hizo kwahiyo asilaze damu kwani atasulubiwa hata kama atakingiwa kifua mpaka hapo watu watakapopata huduma jinsi zinavyostahili!
Mama kasema kuwa yeye huwa hawakemei vijana wake bali husema nao kwa kuwapiga macho basi tunangojea kama January ataelewa mara atakapopigwa jicho!