Rais Samia: Nashangaa Umeme kukatika Marekani!

Rais Samia: Nashangaa Umeme kukatika Marekani!

Umeme hua haukatiki hovyo hovyo huko.

Walimzimia tu umeme ikiwa ni kama ishara ya kumwambia muda wa kukaa huko umepita aondoke.
Haaaaa umepiga,Ila maza bwana ilibidi akaushe tu,upon ugenini unasema eti hata huku mnakulaga viwavi
 
Asitake kujustify ujinga.

Unajua vita ya 2025 ndani ya CCM na makundi yake ni kubwa kuliko vita ya Russia na Ukraine? what we see is just a tip of an iceberg! jaribu kufuatilia kauli zao, teuzi zao katika nafasi nyeti, mikataba inayosainiwa hivi sasa, watu wanaochukua fomu za kuomba uongozi ndani ya CCM hivi sasa, kutumbuliwa Spika, Polepole, Kabudi, Lukuvi, Bashiru, Kurudisha baadhi ya watu wa awamu ya nne ambao hawakukubalika na mwendazake, unaweza kuta walilipia umeme ukatwe kwa sekunde 3 ili wapitishe propaganda yao hii
 
Rais Samia alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi huko Marekani[ U.S.A.] alipata wasaa wa kuwahutubia waTanzania wanaoishi huko.

Alipokuwa anatoa hotuba yake palitokea tukio moja lililomfanya akumbuke nyumbani; ingawa alikuwa ughaibuni nalo lilikuwa pale UMEME ulipokatika wakati akitoa hotuba!!

Mheshimiwa Rais ikabidi aweke kibwagizo kuwa kumbe hata huku UMEME unakatika, ingekuwa nyumbani tukio kama hili January angesulubiwa!!

Tukumbuke tu kuwa tatizo la ukatikaji wa Umeme nyumbani sio sawa na ughaibuni; kwanza ule Umeme ulipokatika pale Nadhani Ilikuwa tatizo la switch ambapo Umeme ulirudi baada ya muda mchache tu ili hali sisi nyumbani umeme ukikatika unakatika kweli , kunasehemu watu wanakosa umeme wa kufanyia kazi hata wiki nzima hivyo hatuwezi kufananisha matatizo yetu ya umeme na wenzetu.

January ni lazima afanye kazi yake kwa weledi ingawa mfano ya Samia inaonesha kama vile kumkingia kifua kuwa hata Marekani pia unakatika, lakini umeme wa Marekani unarudi saa hizo hizo kwahiyo asilaze damu kwani atasulubiwa hata kama atakingiwa kifua mpaka hapo watu watakapopata huduma jinsi zinavyostahili!

Mama kasema kuwa yeye huwa hawakemei vijana wake bali husema nao kwa kuwapiga macho basi tunangojea kama January ataelewa mara atakapopigwa jicho!
Kwani hafanyi kwa weledi? Unaweza eleza ni wapi hajafanya kwa weledi?

Huwa kuna uzushi mwingi Sana wa wapuuzi Kwamba US na Ulaya huwa haukatiki hata Kwa sekunde na ikitokea eti wahusika wanajiudhulu 🤣🤣🤣
 
Mama wa porojo
Ndio hivyo ila ukweli huo..

Kwa porojo hizi Bora aendelee kupiga porojo 👇

20220423_125515.jpg

20220414_122051.jpg

20220414_122046.jpg

Screenshot_20220427-204254.png

Screenshot_20220419-201714.png
 
January na genge lako mtahangaika sana kujitetea lakini kazi imekushinda na wewe ni mmoja mtakaochangia kumuangusha Chief Hangaya!!
Mimi sio January,wewe na genge lako ndio mtahangaika kwa sababu hamueleweki mnashindania nini
 
Mimi sio January,wewe na genge lako ndio mtahangaika kwa sababu hamueleweki mnashindania nini

Wewe kama ni January au Chawa wake utajijua mwenyewe; lakini wananchi wanataka wapate huduma ya umeme ya uhakika, kama kazi imekushinda ni busara kuachia ngazi mtu mwingine aifanye.
 
Wewe kama ni January au Chawa wake utajijua mwenyewe; lakini wananchi wanataka wapate huduma ya umeme ya uhakika, kama kazi imekushinda ni busara kuachia ngazi mtu mwingine aifanye.
Una uhakika tukikuteua wewe umeme utakuwa wa uhakika?
 
Una uhakika tukikuteua wewe umeme utakuwa wa uhakika?

Kuna wataalam wa haya mambo wamejaa hapo bongo lakini kwa vile mnateuana kwa vilemba vyenu ndio maana hakuna umeme wa uhakika na kutoa sababu chungu nzima!! Mimi sina utaalam wa Umeme lakini wenyewe wapo bongo!!
 
Wataalamu ndio mawaziri? Kama wakina nani?
 
Back
Top Bottom