Mara kadhaa, mama Samia anasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Huenda ni watu aina moja kwa sababu wametokana na uchaguzi mmoja.
Ukifuatilia kauli zake hasa katika hotuba ya leo, dira ya Taifa katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo na Ilani ya CCM vinaonyesha tofauti kubwa katika utekelezaji wake.
Mama Samia anakiri kwamba;
Ukifuatilia kauli zake hasa katika hotuba ya leo, dira ya Taifa katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo na Ilani ya CCM vinaonyesha tofauti kubwa katika utekelezaji wake.
Mama Samia anakiri kwamba;
- Viongozi waliopita walifanya kazi nzuri na mema yao yanastahiki kuendelezwa. Hapa aliwataja kwa majina kuanzia Nyerere mpaka JPM. Haamini katika maneno ya kwamba nchi hii ililiwa sana huko nyuma. Hataki kuonesha kwamba yeye na mwenzake wanaanza upya katika mapambano ya wizi na ufisadi. Anawaheshimu waliopita.
- Mama Samia anakiri wazi kuwa sera zetu juu ya uwekezaji hazitabiriki, kodi haileweki na pia kuna bureaucracy ya kutosha kwa wawekezaji. Hii ni kwamba anaona ni namna gani serikali iliyopita ilivyokuwa ikipuuza uwekezaji na kuamini itakuwa dona kantry katika mazingira ya kujitegemea peke yake.
- Mh. Rais amekiri wazi kuwa uwekezaji ulizorota na akasisitiza kuweka ile Wizara chini ya ofisi ya Waziri Mkuu ili kazi ifanyike. Hili ni eneo lililo tofauti sana na mtangulizi wake. Awamu ya tano, wawekezaji walikimbia kodi nyang'anyi, vitisho na kubadilikabadilika kwa Sera.
- Amewaita wapinzani kufanya nao mazungumzo. Licha ya kwamba hili linahitaji tahadhari kwa sababu ni mwanzo, ameonyesha yupo tayari huenda hata kuondoa vikwazo vya wanasiasa kukutana na wapenzi na wanachama wao.
- Rais Samia, ametambua licha ya kwamba utambuzi wake unaendelea, Corona ipo na anahitaji ufanyike utafiti wa kina ili kuweza kukabiliana nayo kama Taifa. Hakuamua kwenda kupima papai au kupuuza chanzo. Hatari ya kukanusha dawa za Kisayansi zilikuwa zinaenda kufanya jamii isiamini katika tiba za aina zozote ikiwamo zile za kufubaza virusi vya ukimwi, chanzo za TB nk.
- Mama Samia ametamka wazi uchumi kusuasua kwa kutaja ukuaji wa asilimia 4.7. Huko nyuma takwimu zilikuwa hazieleweki na hata wataalam wa IMF na World Bank hawakupata fursa ya kuhakiki hali ya uchumi. Kiujumla hali ya ukuaji wa uchumi ni mbaya na lazima tukubali tupo hapo ili tuweze kusonga mbele. Huenda kuanzia sasa tutaona takwimu zinazoakisi uhalisia katika maeneo yote.
- Kwenye uwekezaji wa kwenye ndege, amehitaji uboreshaji. Hiki ni kiashiria kwamba, nchi itajikita kwenye kuweka mifumo imara na wataalam ili kuongeza tija na si ndege.