RAIS SAMIA NI JASUSI WA KIUCHUMI TUMUUNGE MKONO.
Kuna wakati ili Utalii wetu upanuke zaidi tunahitaji jasiri wa kusimamia lakini si kwa kutoa majibu mepesi kwa industry yenye kuhitaji majawabu huru.
Kwa zama hizi, tena kwa kwa utitiri huu wa vyombo vya habari na kuzagaa kwa mitandao kushindwa kutangaza vivutio vyetu huo ni uzwazwa wa hali ya juu.
Tuangalie tunapokwenda kabla ya kutoa majibu mepesi lazima tufikirishe akili kwanza.
Naongea huku nikitanguliza maslahi mapana ya vijana wote wa Tanzania waliojiajiri kupitia Utalii na biashara ya huduma (Tourism and hospitality) nawapenda na kuwaheshimu mno ila niwaambie kuna mahali tulichelewa sana.
Juzi nilisoma kupitia blogs moja hapa Tanzania wakati nipo kwenye Basi naelekea Mbeya. Nilikutana na habari ya kushangaza “Nani mwenye hatimiliki na Filamu ya Tanzania Royal Tour”?
Nilicheka sana kumbukumbu zikanivuta nyuma. hadithi ya sikuelewi ya Majaliwa.
Nikajiuliza kama watanzania tutaanza kuhangaika kwenye vitu vidogo kama mirabaha ya Tanzania Royal Tour tutakuwa taifa mfu. Nani ambaye hakumbuki shida waliyopata wadau wa utali kipindi cha UVIKO19 mamia ya wafanyakazi walipoteza ajira, nchi ilipoteza mapato, wafanyabiashara walipata hasara na sekta ya utalii iliyumba.
Hii imenifikirisha sana kuwa wanasiasa wengi upinzani hawana kesho yao. Pia ni wabinafsi wasiopenda kuona Taifa linasonga mbele kupitia Utalii.
Nikamkumbuka Kagame kimoyomoyo na uwekezaji wa utalii pale Rwanda nikajisemea ama kweli kwenye miti hapana wajenzi kumejaa wakata mkaa watupu.
Kagame Mwaka 2018 baada ya kuingia mkataba na klabu ya Arsenal kuhusu utalii wa Rwanda aliona hiyo haitoshi aliamua kuwekeza na PSG ya Ufaransa kwa ajili kutangaza Utalii.
Kwanini tutafute majibu mepesi kwa ajili ya utalii wetu? Lipo tatizo mahali kwa kipindi cha miaka 5 nyuma iliyopita nchi yetu Mahusiano ya kidiplomasia yaliyumba, Tishio la UVIKO19 lilipoteza nuru ya Taifa hili kupitia Utalii.
Kupitia Uwekezaji wa Kagame kuutangaza Utalii wa nchi yake Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniuliza swali hivi RWANDA kuna kivutio gani kikubwa cha kushawishi hadi waende kuitangaza Rwanda kwenye jezi ya club kubwa kama PSG timu anayocheza Lionel Messi mtu maarufu ulimwenguni? Wanavitu gani ambavyo Tanzania hatuna hadi waende kufanya promo kubwa kama hii?
Huenda maswali haya ya namna hii yalikuwa kichwani kwa Rais Samia kwa awamu hii ya sita ni faraja kwetu sisi watanzania kuamua kutumia muda wake na nafasi ya kutangaza vivutio vya nchi hii si jambo la mchezo.
Rais ameona tukiendelea kufanya mchezo tutaachwa mbali bora atoke na kutangaza Utalii wetu kuwavutia wawekezaji watu kama kina Rihanna, JayZ, Beyonce, David Beckham, Jeff Benzo, Ellon Musk n.k watu ambao wakija Tanzania dunia itaangalia itapata attention kuijua Tanzania ipo sehemu gani Na kuzifahamu fursa zilizopo hapa.
Shughuli za utalii zinaendana sana na utamaduni wetu pamoja na sanaa yetu hivi vitu vimeshikana ndiyo maana Rais Samia amevibeba vyote kwa pamoja.
Kazi kwenu kwa wadau wa utalii, sanaa na wasanii kushirikiana kuhakikisha jambo hili alilolifanya Mhe. Rais linaleta matokeo chanya Rais Samia ametupatia promo ya kutosha tuboreshe Customer care na huduma zetu ziwe na viwango jukumu letu kulinda jina letu juu ya utalii.
Narudi tena kuwaambia mkae na msikie kila nchi ina vivutio vya vyake vya utalii na ina namna yake ya kutangaza huu Utalii.
Kenya ilipoanza kutumia jina la Mlima Kilimanjaro na kuutangaza kuwa ni mali yao tatizo lilikuwa ni Rais Samia.? Utagundua jibu ni hapana na tulikuwa nyuma kwenye kuitangaza nchi yetu hasa kwenye Utalii.
Rais anapofanya Royal Tour anabeba vitu vingi vijana watapata ajira wanazozililia, Royal Tour hii itakuza uchumi wetu kwa kuongeza watalii hela za kigeni zitaongezeka na huduma za kijamii zitaongezeka.
Kama watanzania na wadau wa Utalii tunapaswa kumuombea na kumtia nguvu Rais wetu kwa jitihada anazofanya juu ya Taifa letu.
Tanzania hii yenye utitiri wa vivutio, hifadhi na mbuga za wanyama mbalimbali kushindwa kusonga mbele kiuchumi haiwezekani hata kidogo. Madini yapo lakini yana ukomo Utalii upo leo kesho na hata milele.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.